HESLB yasitisha mkopo kwa waliofanya ukatili

MZALENDO - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi w Elimu ya Juu (HESLB), imesitisha mikop iliyokuwa ikitolewa kwa wanafunzi wann waliosimamishwa masomo kwa kuhusik katika tukio la kumshambulia na kumuumiz mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutw ya Mbeya.

Wanafunzi waliositishiwa mikopo hiy ni Frank Msigwa, John Deo na Evanc Sanga (DUCE), Sante Gwamaka (Chuo ch Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere).

Taarifa ilisema wanafunzi ha walisimamishwa masomo na mamlaka husik kwa utovu wa nidhamu, kwa hiyo wamepotez sifa za kuendelea kupokea mikopo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa n Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Raza Badru, mikataba inayotiwa saini na wanufaik wa mikopo inawataka wanufaika kuzingati masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na nidham na kufuata sheria na taratibu za vyuo n mamlaka halali.

Aidha, kwa mujibu wa taratibu z kukopeshwa, wanafunzi hao watatakiw kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mar moja.

“Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaik wanaoendelea na masomo kuzingatia mashar ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanun taratibu na kuwa mfano mwema katika jamii.”

“Mikopo na ruzuku zinazotolewa na serika ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wem waadilifu na wachapa kazi ili kujenga uchum imara na ustawi kwa wote,” alisema Badru.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.