Ofisi za SENAPA zateketea moto

MZALENDO - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

OFISI ya Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) yaliyoko Fort Ikoma wilayani Serengeti mkoani Mara imeteketea kwa moto.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), moto huo ulianzia katika ofisi ya wanyamapori na kusambaa katika ofisi nyingine.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.

“Taarifa kamili itatolewa mara baada ya uchunguzi kukamilika ikiwa ni pamoja na kujua hasara kamili iliyopatikana na moto huo,” ilisema taarifa hiyo.

Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania hasa mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.

Hifadhi hiyo ina eneo la kilomita 14,763 na kuna idadi kubwa ya wanyapori.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.