Mloganzila kukabidhiwa mwezi huu

MZALENDO - - HABARI - NA JACQUELINE MASSANO

HOSPITALI ya Taaluma na Tiba ya Mlonganzila iliyoko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam inatarajiwa kukabidhiwa rasmi ikiwa vifaa tiba Oktoba 31, mwaka huu.

Aidha, ujenzi wa hospitali hiyo ulikamilika Agosti, 31 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS), Profesa Ephata Kaaya, uwekaji wa vifaa tiba unatarajiwa kukamilika Oktoba 31, mwaka huu.

“Hospitali hii ni ya kisasa na itatoa huduma za Afya za hali ya juu, mafunzo bora kwa wanafunzi wa fani za Afya, Uchunguzi wa magonjwa na tafiti zenye ubora katika fani za afya hapa nchini,” alisema.

Alisema hospitali hiyo itakapoanza kutumika itapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wagonjwa na gharama zinazotumika kuwapeleka nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Profesa Kaaya, alisema hospitali hiyo yenye ukubwa wa vitanda 571 mara itakapopata watumishi, inatarajia kuanza kutoa huduma Januari, mwakani.

Hata hivyo, alisema katika mpango mkakati wa matumizi ya eneo hilo, chuo kimetenga eneo la uwekezaji katika viwanda vya vifaa tiba, madawa na vitendanishi vya maabara.

“Naomba wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza au kuingia ubia na chuo pamoja na serikali ili kufanikisha malengo haya,” alisema.

Alisema viwanda hivyo ni muhimu kwa chuo ili kuleta ushirikiano kwa wanataaluma na sekta binafsi na kutumika katika mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Famasia, Maabara na Biomedical Engineering ili wajenge umahiri unaotakiwa.

Jumla ya Dola za Kimarekani 94,540,000 zimetumika kwa ajili ya ujenzi, kununua na kuweka vifaa tiba kwenye hospitali hiyo.

SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (wa pili Kushoto), akiwa katika matembezi ya amani yaliyoandaliwa na WaislamuwamadhehebuyaKhojaShiaIthanasheriyaTanzania,kumkumbukayakifochaMjukuuwaMtumeMuhammad(SAW),Imam Hussein, Dar es Salaam. (PIcha na Jumanne Gude).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.