Kigoma wasema wako tayari kujituma kwa bidii

MZALENDO - - HABARI - NA MWANDISHI WETU, KIGOMA

WAKATI msimu mpya wa kilimo ukiwa umewadia, Vijana katika wilaya za Buhigwe na Kasulu, wamesema wanakabiliwa na ugumu wa kutekeleza kaulimbiu ya Rais Dk. John Magufuli ya Hapa Kazi tu kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ardhi kwa ajili ya kilimo.

Vijana hao wameishauri serikali kuhakikisha vijana mkoni humo wanawezeshwa kwa dhamira ya kuwajengea mbinu mpya na uwezo ili wafanye kazi za kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara.

Kutokananahalihiyowamemuomba Mbunge wa Vijana Mkoa wa Kigoma, Zainabu Katimba, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Chipukizi Sekondari na Vyuo, kuiambia serikali kuhusu suala linalohusu kilimo ikiwemo pia changamoto ya upatikanaji pembejeo kwa bei kubwa na kutowafikia kwa wakati.

Aidha, Vijana hao wameaiomba serikali ya awamu ya tano ya CCM, kutekeleza kwa vitendo ahadi ilizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 huku wengine wakibainisha kuwa umeme bado ni changamoto kwa vijana hususan walioko vijijini ili waweze kujiajiri.

Akijibu hoja za vijana hao, Mbunge Zainabu Katimba, alisema amezichukua changamoto zao na kuahidi kwamba ataziwasilisha katika ngazi zinazohusika na kuahidi kufanyia kazi zile zilizo ndani ya uwezo wake.

Alisema jukumu la vijana kujikusanya katika vikundi vya ujasiriamali, saccos au ushirika ninla vijana wenyewe kwa lengo kujikomboa na kadhia ya umasikini.

“Ninezingatia kwa umakini changamoto zilizopo, naahidi kuziwasilisha bungeni ili serikali nayo kwa uzito wake iweze kuzifanyia kazi na kupata ufumbuzi stahili “alisema Katimba

Aidha Katimba alisema anaamini serikali ya awamu ya tano ya ccm ni serikali inayosikikiza, kujali maslahi ya wananchi wake na kuhakikisha yake yote yanayowatatiza wananachi kinsingi yanafanyiwa kazi ipasavyo.

Mbunge huyo wa vijana yuko ziarani mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya vijana ambapo anakutana na vijana katika wilaya za mkoa huo kusikiliza changamoto mbalimbaki ili akazifikishe serikalini pamoja na kuwahamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali waweze kunufaika na fursa za kiuchumi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.