Tangawizi ni dawa kwa wanawake

MZALENDO - - AFYA - NA MWANDISHI WETU

TANGAWIZI ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi. Tangawizi hulimwa katika mikoa ya mikoa ya nyanda za juu Kusini, Kilimanjaro, Manyara na Morogoro. kwingineko nchini. Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida lakini ni tiba kubwa katika mwili wa binadamu.

Tangawizi inaweza kutibu magonjwa mbalimbali yasiyozidi 72 yaliyopo katika mwili wa binadamu.

Unaweza kutumia tangawizi kwa njia mbalimbali lengo likiwa ni kupata nafuu ya maumivu uliyonayo katika mwili.

Tangawizi unaweza kuisaga ikiwa mbichi au kuikausha kwa kuichangaya kwenye maji ya uvuguuvugu yaliyochemshwa halafu kunywa.

Hakuna idadi ya vikombe vinavyotakiwa kutumika katika kunywa bali kunywa uwezavyo kama kama.

Wanawake wengi wamekuwa wakitumia tangawizi kwa ajili ya kupoza maumivu wanapokuwa katika siku zao.

Ukitumia tangawizi ni lazima utapata nafuu na mwili utachangamka na utaendelea na kazi zako kama kawaida.

Tangawizi ni dawa nzuri kwa wanawake kwani ni suluhisho la matatizo ya maumivu na unapoona bado maumivu yapo basi wahi hospitalini kwa matibabu zaidi.

Unatakiwa uanze kunywa siku ambayo umeanza kuona siku zako hadi hapo utakapomaliza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.