Wanawake aliowatomasa wajitokeza hadharani

MZALENDO - - KIMATAIFA -

UCHAGUZI Mkuu wa Marekani, wazidi kuibua vibweka wakati wa kuelekea kufanyika kwa uchaguzi huo, Novemba 6, mwaka huu, ambapo mgombea urais wa Republican nchini humo, Donald Trump amelalamika akisema kuwa yeye ni mwathiriwa wa kampeni chafu katika historia ya Marekani.

Trump, anatoa matamshi hayo, ikiwa ni muda mfupi baada ya wanawake kujitokeza na kumlaumu kwa kuwanyanyasa kwa kuwatomasa sehemu zao za siri, ambapo mgombea huyo wa Republican amejibu na kusema shutuma dhidi yake ni uongo.

“Si vigumu kupata watu kadhaa ambao wako tayari kutoa madai ya uongo kunipaka matope,” anasema Trump katika moja ya mikutano yake ya hadhara mjini humo.

Anasema kwa sasa umebakia mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, na amewaambia wafuasi wake kuwa uchaguzi huo umeibwa.

Mmoja wa wanawake wanaomlamu Trump, Summer Zervos anasema mgombea huyo wa Republican alijaribu kujilazimisha kwake kwenye hoteli ya Beverly karibu muongo mmoja uliopita.

Wakati hayo yakijiri, kura za maoni zinaonyesha mgombea wa chama cha Democratic, Hillary Clinton anaongoza huku umaarufu wa Trump nao unazidi kudidimia katika baadhi ya majimbo yanayoshindaniwa.

Tuhuma dhidi ya Trump, zilizotoka hivi karibuni zimetoka kwa mshiriki wa zamani wa shindano la Apprentice, Kristine Anderson ambaye anasema alinyanyaswa kimapenzi na mgombea huyo.

Akiongea katika jimbo la North Carolina, mgombea huyo wa Republican anasema tuhuma hizo ni za uongo, na wanaozitoa wanalenga kujipatia umaarufu na fedha na kwamba wanaongozwa na siasa.

“Au kwa sababu ya kimsingi tu kwamba wanataka kuzuia wimbi letu, wanataka kusimamisha kampeni yetu. Ni rahisi sana,” anasema.

Jessica Leeds ametoa malalamiko yake kwenye gazeti la New York Times kwamba mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump alimshika kimapenzi bila idhini yao.

Anasema mgombea huyo alimshika matiti na kujaribu kuingia mkono wake chini ya sketi yake wakiwa kwenye ndege miongo mitatu iliyopita huku alikimpiga busu mwanamke mwingine bila yeye kutaka katika jumba la Trump Towers mwaka 2005.

Maofisa wa kampeni wa Trump wameeeleza kuwa “makala hii yote ni hadithi ya kubuni”. na gazeti la New York Times limeanzisha kampeni “ya uongo, na iliyoratibiwa kumharibia jina la Trump”.

Jessica (74), kutoka Manhattan, anasema alikuwa amekaa karibu na Trump sehemu ya abiria wa hadhi ya juu kwenye ndege wakielekea New York pale alipoinua sehemu ya kupumzishia mkono kitini na akaanza kumshika.

Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 38 wakati huo, anaeleza mikono ya Trump ilikuwa kama pweza na ilishika kila mahali na ulikuwa ni unyanyasaji.

JESSICA Leeds

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.