HIVI MBOWE HAJUI DEMOKRASIA

MZALENDO - - MAKALA - Email: eliassabuni@yahoo.com Mobile No. +255756 341989.

“Na Elias Sabuni Asiye jua Maana usimwambie Maanaî Watanzania tumekuwa kwenye kumbukumbu chungu za kuondokewa na Baba wa Taifa letu ambaye kumbukumbu zake si kwa kufariki kwake tu lakini pia ni kukumbuka mema aliyotuachia.

Naikumbuka safari yake ya kwanza mwaka 1958, Mwalimu Julius Nyerere alipoingia mjini Mwanza na kuzuiwa asifanye mkutano wowote, lakini wananchi toka Geita na Mwanza walimshangaza Mkuu wa Mkoa alipoambiwa Uwanja wa Nyamagana umefurika watu wanaotaka kumuona Nyerere.

Alichofanya mkuu huyo ni kuwataka watu warudi kwenye maeneo yao na walipokataa kufanya hivyo mabomu ya machozi yalifuata toka kwa askari wa Fanya Fujo Uone (FFU). Baba na Mjomba wangu yaliwakuta hayo na kukimbia kupanda feri ya Kamanga.

Hata hivyo, RPC alitoa fursa kwa Mwalimu Nyerere kwenda Geita akaonane na hao waliomfuata Mwanza, lakini asifanye mikutano ya hadhara.

Katika lugha ya kisiasa, demokrasia ilitumika kwa kutoa ruhusa hiyo. Dk John Magufuli amebana demokrasia kwa njia ipi hadi Mbowe anadai ataenda mahakamani kudai?

Tunapomkumbuka Baba wa Taifa, tuna mengi ya kumuenzi. Baba wa Taifa alipoona mfumo wa vyama vingi unachelewesha maendeleo, alitoa mwongozo wa kuwa na mfumo wa chama kimoja, lakini kila kiongozi lazima apite kwa kura za wananchi ili aweze kuwa kiongozi.

Maamuzi hayo yalionekana na wale waliokuwa na utamaduni wa kushinda kwa kubishana kwa madai kuwa Mwalimu amekuwa mkomunisti na ameua demokrasia.

Watu hao walieneza maneno yao ya chuki hadi kusababisha Uingereza na Marekani kuondoa baadhi ya misaada kwa kisingizio kama hicho hicho kinachodaiwa na Mbowe kuwa demokrasia imekufa.

Baba wa Taifa, katika kuondokana na siasa ya vyama vingi alilenga kuleta maendeleo haraka, na ndio msingi wa kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa na kujitegemea.

Alitaka kila mtu aweze kuishi na kutumia raslimali za taifa kwa maendeleo ya wote. Mfano unaonikumbusha hili ni mwaka 1974 wakati wa vijiji vya ujamaa, kabila la Wakara watabaki wanamkumbuka Baba wa Taifa pale alipowahamisha baadhi yao kutokana na uhaba wa ardhi yao ya asili na kuwapeleka Sengerema, Kahunda na kujipatia ardhi tele ya kulima, hivyo kubadili maisha yao.

Utawala wa Baba wa Taifa kwa kuliona tatizo la vyama vingi wakati wananchi wakiwa hawaelewi tofauti zake kwenye Katiba ya Taifa kukawekwa kipengele cha kilichosema: ìArdhi ni mali ya taifa.î

Kipengele hiki ndicho kinachotoa nafasi ya serikali kubadili matumizi ya ardhi wakati wowote kwa faida ya taifa. Kipengele hiki ndicho kinachotakiwa kitumike hata sasa katika kumaliza mvutano kati ya wakulima na wafugaji.

Katiba ya Chaga Development Manifesto inaweka wazi kabisa kuwa wakiingia madarakani wataanzisha utawala wa majimbo. Hii ina maana kuwa ule umoja aliouweka muasisi wa nchi, wao hawana habari nao.

Hivi wakisema wanamuenzi Baba wa Taifa ni kwa lipi? Rais Dk. Magufuli ameagiza viongozi wa mikoa nje ya huko kunakofanyika sherehe za kuzima mwenge na kumbukumbu za Baba wa Taifa wasiende huko ili kubana matumizi ya serikali , tayari Mbowe ameshangilia kuwa hiyo ni dalili ya kufuta mbio za Mwenge.

Hivi Mbowe anayo historia ya Mwenge huo? Hivi kama siku umetamani kula nyama, lakini ghafla homa kali imekupata, fedha utanunua nyama au dawa?

Utawala awamu ya tano umetoa mwelekeo wa utawala wake katika ahadi za kuwasaidia wananchi kupata maendeleo.

Jukumu hilo halijakamilika, unawezaje kuaza kununua nyama wakati ugonjwa haujapona. Hivi bila kubana matumizi walimu leo madeni yao yangekuwa yamelipwa?

Moja ya hotuba za Baba wa Taifa ambayo alionekana kuitoa kwa hisia nzito ni ile aliyokuwa akiwaasa Watanzania kuhusu Utanganyika na Uzanzibari.

Mwalimu alisema Tanzania imekuja ndani ya miaka mitatu tu baada ya Uhuru na Zanzibar ni miezi tu, sasa hao wanaodai Utanganyika ni wangapi ukilinganisha na wale waliozaliwa ndani ya Tanzania?

Kauli ya Mwalimu Baba wa Taifa ilionyesha madhara ya kubaguana ambapo mkikubali kufanya hivyo, hatutaishia kwenye Zanzibar na Tanganika, lakini itafika hadi kwenye ukabila.

Mbowe na CHADEMA, utawala wa majimbo unatupeleka wapi? Mbowe, demokrasia unayotaka kwenda kuitafuta huko mahakamani ni ipi? Ama unataka kupata kibali cha mahakama cha kutukana matusi hadi bungeni na bado ukaachiwa kuendelea na ubunge wako?

Au unataka upate kibali cha mahakama cha kukuruhusu kuchochea watu kufanya maasi, hatimaye wakatoana macho hadharani?

Hivi kama kesho Mbowe utakuwa Rais wetu, utatuachia tufanye tunavyokata au utatoa muongozo wa kusema tuishi vipi? Rais Dk. Magufuli amesemaìHapa Kazi Tuî Je wewe unatuambia tuseme nini? “Hapa Chadema Tu” Baba wa Taifa alizikimbia siasa za Kimarekani na Uingereza na kwenda China na Urusi, alikuwa na nia moja tu ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya haraka kwa kuachana na vyama vya upinzani.

Bahati mbaya Mwalimu alikuwa anafanya sawa na mtoto mdogo aliyetegemea kula kwa mzazi wake. Baada ya kuona sasa watoto wamekua na kuwaachia wajitegemee ndio kumeibuka hao wanaodai wamenyimwa demokrasia

Imani ya demokrasia ni sawa na imani ya dini. Imani ya dini ni kutafuta pepo na wakati wote uwe msikivu kwa viongozi wako. Demokrasia nayo ni hivyo lazima uwe msikivu wa wiongoz wako. Zi o aliokosa usikivu akatimuliw CHADEMA na hao hao ambao nao wanakosa usikivu kwa kiongozi wa taif letu leo.

Mbowe na Watanzaania wote, tunamkumbuka Baba wa Taifa si kwa kutangulia mbele ya Haki tu, bali hata angekuwa nasi leo, tungemuenzi kwa kuleta Uhuru wa nchi hii, kuwasha Mwenge wa Uhuru na mbio zake, vijiji vya ujamaa, kuondoa rushwa na kuwek utaratibu wa kupokezana kifimbo ch kuachiana madaraka.

Wapinzani katika haya yote, mnamkumbuka Baba wa Taifa kwa lipi Kutopokezana kifimbo cha uongozi ndicho kinawasibu CUF, NCCR, na karibuni CHADEMA.

Baba wa Taifa ndiye alikuwa mlinzi mkuu wa demokrasia ya Tanzania na Afrika kwa ujumla, Dk. Magufuli sasa amevaa kiatu chake, lakini Mbowe anaona anaonewa.

Mbowe na Ukawa , kumbukumbu y Baba wa Taifa inafaa iwakumbushe moj ya hotuba zake pale alipowakumbusha Watanzania kuwa ìRais, ni Rais wa Tanzania kwa Katiba ya Tanzania, mamlaka yake na sheria zote zipo kwa Katiba ya Tanzania.î

Mbowe nchi hii lazima iongozwe kwa sheria ma katiba. Mamlaka ya Rai ni kulinda katiba, hivyo kama unaenda mahakamani nenda kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

“Mahakama ni sawa na jiko, kila kinachopikwa hupita pale hata kama hakitafaa kuliwa.”

Hapa Chadema Tu” Baba wa Taifa alizikimbia siasa za Kimarekani na Uingereza na kwenda China na Urusi, alikuwa na nia moja tu ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya haraka kwa kuachana na vyama vya upinzani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.