Tambwe kuikosa Azam leo

MZALENDO - - MICHEZO - NA VICTOR MKUMBO

MSHAMBULIAJI mahiri wa timu ya Yanga, Amis Tambwe, leo ataukosa mchezo wao dhidi ya Azam utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Tambwe ataukosa mchezo huo baada ya kuumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar ambao walishinda kwa mabao 3-1, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru.

Nyota huyo aliumia kwenye mchezo huo dakika ya 87 alipogongana na kiungo wa Mtibwa Shaban Nditi na kushindwa kuendelea na mchezo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneje wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema kuwa wachezaji wote wa kikosi chao wapo fiti kasoro Tambwe.

Alisema kuwa Tambwe ataukosa mchezo huo pamoja na kuwa alishaanza matibabu lakini bado hali yake haijatengemaa vyema.

Alisema kuwa wachezaji wengine wapo katika hali nzuri na wataingia kwenye mchezo huo kwa kujihami kwani Azam sio timu ya kubeza.

“Tambwe hatakuwepo kwenye kikosi cha kesho (leo) kwani bado anaendelea na matibabu na hali yake haijarejea kama zamani, hivyo kocha Hans van Pluijm anatarajiwa kutumia wachezaji wengine kwenye nafasi yake,” alisema.

Alisema kuwa wamefanya maandalizi yakutosha na mazoezi ya nguvu kuhakikisha wanashinda kwenye mchezo huo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.