Ndauka awaasa chipukizi

MZALENDO - - MICHEZO - NA ABDUL DUNIA, TSJ

MSANII nyota wa filamu za bongo movie, Rose Ndauka ametoa wito kwa wasanii chipukizi wa tasnia hiyo ya filamu nchini kujituma ili kuweza kufikia malengo yao.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ndauka alisema kuwa wasanii chipukizi wanahitajika kuongeza juhudi kwenye kazi zao ili kujiongezea mashabiki.

Alisema kuwa soko la filamu kwa sasa lina ushindani wa hali ya juu hivyo basi inahitajika wasanii hao kuongeza ubunifu.

Aidha, Ndauka amewataka wasanii chipukizi kutohofia majina makubwa ya wasanii wakongwe kwa kuwa filamu haziangalii uzoefu wa majina.

Pia amewataka wasanii chipukizi kutumia uwezo wao wa kuigiza kuwashawishi wasanii waliofanikiwa kufanya nao kazi pamoja.

Ndauka ni mmoja wa waigizaji wa kike walioweza kufanikiwa kutokana na uwezo wake wa kuigizaji na ubunifu aliokuwa nao.

Msanii huyo ameshawahi kufanya kazi pamoja na wasanii nguli wa Tanzania akiwemo marehemu Steven Kanumba na muigizajia aliyepotea kwenye tasnia hiyo kwa sasa Vicent Kigosi ‘Ray’.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.