BQ Open mguu sawa NA MWANDISHI WETU

MZALENDO - - MICHEZO -

ZAIDI ya wachezaji 60 chipukizi wa tenisi wanatarajiwa kushiriki kwenye michuano ya wazi ya ‘BQ Open’, itakayoanza Novemba 19-20 kwenye Uwanja wa klabu ya Gymkhana Dar es Salaam (DGC).

Michuano hiyo itashirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 6 hadi 18 kutoka katika maeneo mbalimbali nchini na nchi za Uganda na Kenya.

Akizungumza Dar es Salaam, kocha wa vijana wa klabu hiyo, Salum Mvita alisema kuwa, mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yatashirikisha wachezaji kutoka nje ya nchi ili kuwapa chachu wachezaji wa nyumbani.

“Hadi sasa ni Uganda na Kenya ndizo zilizothibitisha kuleta wachezaji,lakini tunazikaribisha nchi nyingine kuja na kushiriki ili tuweze kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana na mchezo kwa ujumla,” alisema Mvita.

Kocha huyo aliongeza kuwa, mashindano hayo yanalenga kuwaendeleza wachezaji chipukizi sambamba na kupata wachezaji wengine wapya kwenye klabu hiyo.

“Tunaendelea kuwasihi wazazi kuleta watoto wao hapa waje kucheza, sisi tunatoa kipaumbele kwa vijana wadogo kwa sababu mchezo huu unafaa kufundishwa mapema na mtoto ataulewa zaidi na kuwa mchezaji hodari akikua,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.