CCM yaomboleza kifo cha kada wake

MZALENDO - - MBELE - NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Mwenyekiti mstaafu wa Chama mkoa wa Iringa, Tasili Mgoda, aliyefariki dunia juzi katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga.

Taarifa iliyotolewa n CCM, jana, kwa vyombo vya habari ilisema enzi za uhai wake Mgoda alishika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TANU, CCM na serikalini.

Ilisema pia, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mafinga, Katibu wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkuu wa Wilaya.

Kinana katika salamu zake za rambirambi, alisema amepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa kifo cha Mgoda ambaye alikuwa ni sehemu ya hazina ya wazee wa Chama.

Alisema anaungana na familia ya marehemu, ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.