Ndege ya kusafirisha damu

MZALENDO - - HADITHI -

UNAWEZA usiamini, Lakini ndo imetokea nchini Rwanda, baada ya Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame, kuzindua huduma ya kusafirisha damu na vifaa vingine vya matatibu kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani.

Mradi huo wa kusafirisha damu kwa kutumia ndege utasimamiwa na Kampuni ya Marekani iitwayo Zipline na ni huduma ya kwanza ya aina yake kufanyika duniani.

Ndege hizo ambazo hazina marubani zitakuwa zikiruka a moja kwa moja hadi eneo ambalo damu itakuwa inahitaji nchini humo na kurejea kituoni.

Hata hivyo, ndege hiyo baada ya kutua, itarusha kifurushi cha damu ardhini kwa kutumia mwavuli au parachuti.

Teknolojia hiyo inaleta matumaini ya kuwasilisha damu haraka na kwa njia salama ikilinganishwa na hapo awali ambapo njia iliyokuwa ikitumia au ikitegemewa ni barabara ambazo hali yake sio nzuri.

Wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ni wahandisi ambao awali walifanya kazi katika kampuni maarufu za kiteknolojia kama vile Space X, Google, na Lockheed Martin..

Awali ndege hizo zitatumiwa kusafirisha damu, maji ya damu na dutu inayogandisha kioevu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.