Itikadi haina nafasi katika siasa Tanzania

Rai - - MAONI/KATUNI -

TANZANIA ilikuwa na jumla ya vyama vya siasa 22, lakini vingine vimefutwa na Msajili. Madhumuni ya kuwa na vyama vingi ni kuwapa nafasi wananchi kuchagua chama cha kujiunga nacho kutokana na itikadi na sera yake.

Wakatiwamfumowachamakimoja, wananchi hawakulazimishwa kujiunga na chama tawala, lakini walikuwa wanajua kwamba chama hicho kilikuwa na itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea.

Mfumo wa chama kimoja ulipofutwa mwaka 1993, vilizuka vyama vingi ili kupambana na chama kilichokuwa madarakani— lakini hakuna chama ambacho kilikuja na itikadi na hadi sasa miaka 30 baadaye, hakuna chama kinachojipambanua kwa itikadi— hata Chama cha Mapinduzi (CCM) chenyewe—hakijasema wazi wazi itikadi yake ni ipi.

Ushindani wa kisiasa uliopo ni mapambano ya sera na mipango ya namna ya kutekeleza sera hizo. Hiki ndicho kinawafanya wananchi wachague viongozi wao kwa matumaini kwamba huenda programu za chama fulani, huenda zikawapam unafuu wa maisha. Na sera zinabadilika kufuata na vipindi vya hali ya kisiasa nchini ikoje.

Jambo la pili ambalo vyama vya siasa vinapaswa kuzingatia, ni kuwa na viongozi wanaotambua kuwa kuongoza ni kutumikia wananchi. Chama ambacho hakina mizizi kwenye ngazi za chini, mara nyingi hakikubaliki. Vipo vyama kwa mfano, ambavyo vinasikika wakati wa uchaguzi tu na katika uchaguzi uliopita, havikufanya kampeni yoyote ya maana.

Chama ambacho Watanzania watakikubali, ni kile ambacho kitazingatia matatizo yao ya msingi— chama ambacho sera yake italenga kupunguza tofauti ya matabaka kati ya walalahoi na walalahai na wenye nacho.

Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi hiki,vyama vyetu vya siasa vitautumia muda huu kujielekeza, sio tu kuongeza wanachama, bali pia kupanga mikakati na programu mahususi zitawafanya wananchi wajione kwamba zinawalenga wao. Kung’ang’ania itikadi hakuwavutii wananchi kwa sababu itikadi ni nadharia ya imani.

Tunakubaliana na dhana kwamba ili chama kionekane kuwapo karibu na wananchi, vyama viache kuiga mfumo wa kuwa na wajumbe lukuki kwenye mikutano ya kikatiba kuanzia ngazi za chini hadi juu—hii itavipunguzia gharama na kuvifanya kuwa na mijadala yenye afya na kutoka na mkakati wa utekelezaji.

Ni vizuri vikao vya juu vya chama chochote cha siasa, viwe vinatoa dira na kwa vile vitakuwa na viongozi wachache wanaoeleweka na wenye kuweka maslahi ya chama chao mbele. Kwa kuwa vyama haviruhusiwi kufanya siasa za uwazi, basi upo umuhimu wa kuweka watu katika ngazi mbali mbali—ambao watafanya kazi kwa ajili ya jamii na miongoni mwa wananchi. Bila hivyo, vyama vichanga vitajikuta vinpigwa bao tena katika duru la Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2020.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.