Magufuli ametekeleza matakwa ya chama

»

Rai - - MAKALA -

anachokitaka. Kwanza ni katika kitabu cha Tanu na Raia—mwaka 1962. Pili ni hotuba yake aliyoitoa kule Mafia, mwaka 1966.

Alibainisha wazi kwamba chama lazima kiwasemee watu. Ile ya mwaka 1962, alisema uongozi unatokana na watu. Akasisitiza uongozi upatikane kwa haki kwani uongozi unaopatikana kiujanja ujanja kwa njia ya rushwa, ghilba, si uingozi unaotokana na watu. Hiyo ilikuwa misimamo ya Mwalimu na ndiyo aliyonayo Rais Magufuli.

Pili linalomfanya Rais Magufuli arandane sana na Mwalimu, kwamba Mwalimu aliwahi kusema kazi ya Serikali inafahamika, kujenga barabara, shule na hospitali kwa sababu mahitaji mengine binafsi kuna namna ya kuyatimiza kuna njia zake. Ninaamini Rais Magufuli anataka Serikali hii iwarejee watu wa kawaida, shida zao za kawaida, kuna mfanano mkubwa sana kati yake na Nyerere.

Katika hotuba ya mwaka 1966, Mwalimu alisema chama lazima kiwasemee watu, na akazungumzia miiko ya uongozi, kipindi hicho ndio kulizuka misamiati ya manaiz, wabenzi na makabwela. Manaizi ni viongozi Wafrika waliochukua nafasi zilizokaliwa na Wazungu, manaiz lilitokana na neno ‘Afrikanisation’, viongozi hao walianza kujibagua. Wabenzi walikuwa viongozi wa Serikali kama mawaziri, kwa sababu walipewa magari aina ya Benzi, basi wakaitwa wabenzi wakati makabwela ni neno la kizaramo likimaanisha wale wa kawaida ambao hawajui hata chakula cha siku kitatoka wapi.

Mwalimu akasema inakuwaje kiongozi DC unakuwa na hekari 3000, hata Rais hawezi kuwa nazo, sasa dhana hii tunaiona kwa Rais Magufuli. Anataka kumaliza matabaka kama alivyofanya Mwalimu Nyerere na kuonesha kuwa uongozi ni utumishi. Ndio tunachokiona kwa Magufuli kwa sababu kipindi hicho hata viongozi wa TANU walikuwa wamepigwa marufuku kuajiri watu kwenye mashamba yao.

RAI: Ni kipi unachoweza kujivunia katika utumishi wako katika Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere?

DK. MUKAMA:

kupokezana

vijiti. Uongozi ni

Mazingira ambayo Mwalimu alipambana nayo, ni mazingira ya ukombozi, kwa sababu yeye na Nkurumah walisema Afrika haiwezi huru kama nchi moja itakuwa chini ya ukoloni. Kwa hiyo, katika kipindi chote cha Mwalimu kuanzia mwaka 1961, 1963 ilipoanzishwa OAU, na 1965 ambapo Dar es Salaam iliteuliwa kuwa makao makuu ya African Liberation Committee, (Kamati ya Ukombozi wa Afrika) mpaka mwaka 1977, mazingiria ya uongozi wa Mwalimu yalikuwa mazuri sana.

Ila kuvunjika kwa EAC (Jumuia ya Afrika Mashariki mwaka 1977), kuliathiri sana uongozi wake, ilibidi tuwe na shirika letu la simu, reli, anga, ikabidi kuwekeza upya, lakini tulikuwa na reserve (akiba kubwa) nyingi ya rasilimali hadi Benki ya Dunia ikasema haitakiwi kwa nchi changa kuwa na rasilimali namna hiyo.

Kutokana na kuvunjika kwa Jumuiya, rasilimali nyingi zilitumika kuanzisha hayo yote. Lakini mwaka 1978, Iddi Amin (wa Uganda), akatuvamia na vita ikatuvuruga sana, tukafunga mkanda, hadi mwaka 1985 ndipo (Mwalimu) akaachia urais. Hivyo niseme kwamba kila kiongozi alikuwa na mfumo wake. Alikuja Ali Hassan Mwinyi tukaenda hivyo hivyo hadi kufikia kiwango cha kutokopesheka, na kuwa nchi masikini zaidi duniani. Alipokuja Mkapa likawa ni jukumu lake kututoa huko.

Ni kwamba Mwalimu alikuwa anajenga utaifa, kwa sababu hapakuwa na Taifa la Tanganyika, na kubwa lililomsaidia ni lugha. Pili akaanza kujenga msukumo wa dhati wa ukombozi, na imetujengea heshima.

RAI: Baada ya kuachia nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM, ilidaiwa kuwa utakwenda kuwa Mkuu wa chuo cha siasa kitakachoanzishwa na CCM, mpango huo umefikia wapi?

DK. MUKAMA:

Ni kweli baada ya Tanzania kuzisaidia nchi za Afrika kujikomboa, nchi za Afrika Kusini, Zimbabwe, Msumbiji, Angola, Namibia na katika hilo kutambua hilo vyama vyao vya ukombozi kusini mwa Afrika, FRELIMO, MPLA, ZANUPF, ANC, SWAPO, vinataka kujenga chuo hapa cha kufundisha viongozi watakaoendeleza hii fikra ya kujiona Afrika ni moja, sisi ni Waafrika. Jukumu hilo tumepewa sisi, na ninasimamia kuanzishwa hicho chuo kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China.

ANC na CCM, vimeshakwenda China na tayari eneo limeshatengwa kule Kibaha, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa chuo hicho mara moja.

Chuo kinaitwa Executive Political Leadership Academy. Kitapokea watu kutoka kwenye vyama mbali mbali na taasisi. Hiki si chuo cha CCM. Ni kama kile cha jeshi ambacho wanakwenda watu mbali mbali kujadili mambo ya nchi kujenga uzalendo.

Kiujumla, chuo hiki tunatarajia kitakamilika ndani ya muda wa

miaka miwili na kuanza kazi.

RAI: Unauzungumzia vipi uongozi wa Rais John Magufuli ambaye ametimiza mwaka mmoja madarakani hivi karibuni?

DK. MUKAMA:

Kuna kitabu cha Mkorea kinazungumzia namna Marekani na Uingereza zilivyotajirika, pia kinazungumzia nafasi ya dola katika kusimamia sekta binafsi. Ninachomshauri ni kwamba Serikali isikae mbali na sekta binafsi, hata kama ni viwanda vyetu, watu wetu wa ndani lazima Serikali ikae nao karibu. Serikali inatakiwa kuwa katika nafasi kubwa kuisimamia. Hata Korea Kusini au Japan, zilikuwa na taasisi zake ambazo zilikuwa zinasimamia sekta binafsi.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani pia, zilisimamia kwa karibu sekta hiyo ndio maana zimeendelea kukua. Zipo nchi za Kiarabu zilidharau zinaendelea kutegemea rasilimali moja pekee.

RAI: Unazungumziaje mabadiliko yaliyoyafanya Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli?

DK. MUKAMA:

Hakika ni mabadiliko mazuri ambayo kila mmoja wetu ameyafurahia. Kwa sababu hata kwenye hali (level) ya vikao—kwa maana ya wajumbe wa Kamati Kuu wamepunguzwa. NEC wanakuwa 158 kutoka 388. Hata katika nadharia na uzoefu, watu wanapokuwa wachache mijadala inakuwa inafanyika kwa ufanisi zaidi.

Unapoboresha muundo ni muhimu sana, lakini mwisho wa yote, viongozi ndio wanaoweka dira, tunaona vikao wamepunguza ili sehemu kubwa itumike kwenda kwenye wanachama kule chini, kwenda kwa watu. NEC ilikuwa na vikao vitatu sasa itakuwa na viwili, na Kamati Kuu ilikuwa na vine, sasa itakuwa na vitatu.

Kwa mfano, suala la kushirikisha vijana katika nafasi mbali mbali ni zuri, kwa sababu unawashilikisha kwa vitendo. Kila mmoja kuna mahala anapoanzia, Wafaransa wana neno la social practice, vijana lazima uwalee uwajenge… safari ya kilomita 1000, lazima uanzie kwa hatua moja. Hata mimi nilienda Kivukoni mwaka 1974, nikiwa mdogo sana nikiwa na umri wa miaka 25, lakini nilikuwa nafundisha wazee.

RAI: Unafikiri nafasi ya itikadi na uenezi bado inatakikana ndani ya CCM, hasa ikizingatiwa kuwa Chama sasa hakijajipambanua kipo mrengo gani?

DK. MUKAMA:

Chama ambacho hakina itikadi kinajitofautisha vipi? Itikadi ni neno la Kimalay, ila limetoholewa. Itikadi ni ile faith (imani), chama ambacho hakina itikadi ni sawa na gulio, kwa sababu itikadi ni kama dini, uislamu, au ukatoliki, una itikadi yake. Hii ndio inatofautisha. Mtakuwa na sera ambazo zinabadilika, ila itikadi ndio inayoongoza. Kwa sababu kinachowaunganisha ni fikra zilizojengwa katika imani fulani, mtatofautiana katika sera ila si itikadi.

RAI: Kwa kuwa ulitumikia nafasi ya ukatibu mkuu ndani ya CCM, ni kipi unachoweza kujivunia baada ya kuachia nafasi hiyo?

DK. MUKAMA:

Chama ni tofauti sana na Serikali kwa sababu serikali ina tabia ya kujenga vitu vinavyoonekana. Ila niseme kubwa ambalo ninajivunia ni kurudisha umoja ndani Chama. Kuwa na uanaCCM, tumefanikiwa katika kipindi chote hicho, ukiangalia 2010, 2012 na 2015 kulikuwa na joto katika kuwatafuta viongozi wa 2015. Joto hilo lilikuwa juu, lakini CCM ilibaki ndani ya umoja bila kuyumba. Hilo ni moja ya mafanikio, kwamba tangu 2007 walipofanya uchaguzi, CCM imeendelea kuwa imara.

Hatukupata watu waliotoka CCM kwenda kuanzisha chama kingine, labda wamekuwa wakitoka kujiunga na vyama vingine, hakuna aliyetoka kwenda kuanzisha chama chake, hata waliotoka kwa sababu tu ya mahitaji ya muda mfupi, kwa ajili ya kuwa wagombea kutafuta nafasi za urais, walidhani wafuasi watawafuata, lakini hilo halikutokea, kwa sababu kati ya wenyeviti 26 wa mikoa, ni wawili tu waliohama kumfuata mgombea waliyemtaka. Kwa aina ya siasa tulizo nazo, CCM niseme kuwa imeendelea kushinda.

RAI: Unafikiri kwa nini operesheni ya vua gamba ilishindwa kutimiza malengo yaliyotakikana katika kipindi chako?

DK.

MUKAMA:

Tatizo lililojitokeza katika operesheni ile, ni la kutazama vitu kijuujuu. Mwenyekiti alipotoa mfano katika hotuba aliyoitoa kule Dodoma, Februari 5, mwaka 2011 katika maadhimisho ya miaka 34 ya CCM, alisema chama kina umri wa miaka 34, kwa hali ya nchi si umri mkubwa, ila kibinadamu anakaribia utu uzima. Hivyo hata nyoka ana tabia fulani ya kujivua gamba— inaitwa metamorphosis. Tabia hiyo inamwezesha kujivua gamba. Sasa chama cha siasa kinatakiwa kujivua gamba kwa maana kuwa kuwa kujire ‘brand’ na ‘repositioning’ na ‘repackaging’.

Ila rebranding ni zaidi ya vyote, pia repositioning, ni lazima kuoneshe ulipo na unapoelekea. Alisema ni wakati wa kujitazama.

Sasa ni bahati mbaya sana, katika kujirebrand ikawa imemezwa katika majina ya watu, sasa huko si kujirebrand, watu walitafsiri kama kutoa watu wakati lengo ni kutengeneza Chama upya. Ilikuwa lazima kuangali mazingira yaliyopotumekosea wapi, ndipo ikaja kujivua gamba, hii dhana ilipuuzwa, ikatumika visivyo— kwamba kwa kuwatoa watu fulani ndio kujivua magamba, na sisi wengine bahati mbaya ukifanya uchambuzi ndio hivyo tena.

Kwa hiyo, Mwenyekiti alikuwa na nia nzuri tu, na sasa chama kimejireposition. Anachokifanya Magufuli tulidhamiria kukifanya, ila watu wakatutafsiri viabaya na kuvuruga mpango huo.

Magufuli anapunguza gharama katika masuala yote ya uchaguzi, kwamba kila mkoa uwe na mjumbe mmoja, na tawi liende mpaka watu 300.

RAI: Unauzungumziaje Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana?

DK. MUKAMA:

Ukiangalia kitakwimu, vyama vya upinzani vimekua kwa sababu vilikuwa na mgombea mmoja, hata huko nyuma havikuwahi kuvuka asilimia 40 katika kura za urais. Kwa mfano 1995 na 2005, 2000 na 2005, walishuka sana. Kwa hiyo vyama vya upinzani kwa ujumla wamegangamala, ila kitakwimu bado sana.

RAI: Kingunge NgombaleMwiru ni mmoja wa makada wa CCM waliojiengua ndani ya CCM na kumuunga mkono Edward Lowassa, kwa kuwa alikuwa kiongozi wako kwa muda mrefu, katika utumishi serikalini na ndani ya Chama unazungumziaje maamuzi yake?

DK. MUKAMA:

Ngombale kwa umri aliokwisha fikia, alikuwa ni mzee wa Chama, hakuwa na nafasi ‘active’, hakuwa mjumbe wa vikao. Alikuwa mzee tu, sasa uzee una mipaka yake, ndio maana hakuna mtu aliyemsema. Yule ni mzee wangu alinichukua Kivukoni mwaka 1983 mpaka 1991, nilifanya naye kazi kwa karibu sana. Kwa heshima kama mzee na yeye mwenyewe alisema hatojiunga na chama ingawa alimsaidia mgombea wa Chadema, ila hakuwa na madhara makubwa sana, kwani watu walikuwa wanashangaa zaidi kuliko kutikiswa na kuondoka kwake.

kitakwimu, vyama vya upinzani vimekua kwa sababu vilikuwa na mgombea mmoja, hata huko nyuma havikuwahi kuvuka asilimia 40 katika kura za urais. Kwa mfano 1995 na 2005, 2000 na 2005, walishuka sana. Kwa hiyo vyama vya upinzani kwa ujumla wamegangamala, ila kitakwimu bado sana.

RAI: Unazungumziaje uamuzi wa Rais Magufuli kupiga marufuku mikutano ya vyama ambayo pia imekiathiri CCM?

DK. MUKAMA:

Suala la kuendelea na mikutano ya vyama baada ya uchaguzi ni Tanzania tu linafanyika, nchi zilizoendelea kidemokrasia kama Uingereza, Marekani, suala hili halipo na huwa linafanyika katika kipindi cha uchaguzi tu ambacho wagombea hutumia kufanya kampeni. Ni sahihi kwa sababu unatakiwa kuachia chama kilichoshinda kiunde serikali kuendesha nchi. Magufuli hajaanzisha kitu ambacho hakifanyiki kwingine.

RAI: Unafikiri kwa mwenendo huo Rais Magufuli ataweza kurudi katika Uchaguzi Mkuu wa 2020?

DK. MUKAMA:

Naamini atarudi kwa kishindo, kwa sababu kwa hali ilivyo, Rais Magufuli anaungwa mkono sana… kwanza kwa maamuzi yake, kauli na vitendo vyake vinaoana.

Dk. Wilson Mukama

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.