Si kila simu ya China ni feki - Huawei

Rai - - MAKALA -

Tna simu za kisasa lengo likiwa ni katika kusalia kuwa kinara. Tayari kampuni hiyo kuelekea msimu huu wa sikukuu imeweka sokoni bidhaa zake mbalimbali zikiwamo, Huawei Y6ii, P9lite, Y5ii na Y3ii ambapo pia imeanzisha utaratibu wa kutoa zawadi mbali mbali ikiwamo kubwa ya kushinda gari aina ya Renault KWID kwa wateja wake.

Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania, anasema watanzania licha ya kuwa simu feki zimetoweka kwa sasa lakini hawana budi kuwa makini kwa kununua bidhaa za kampuni hiyo.

“Kuna upotoshaji ulioshika kasi nchini kuwa simu yoyote iliyo na kioo cha kugusa “touch screen” ni smartphone. Na hii ndio iliyopelekea kuongezeka kwa idadi ya simu feki katika soko la Tanzania kipindi cha nyuma.

“Kifupi, smartphone inamuwezesha mtumiaji kupiga simu, ina sifa kama za kompyuta au laptop, uwezo wa kupata huduma za intaneti na kadhalika,” anasema Jacko.

Jacko, anasema kuwa siyo busara kwa watanzania kuendelea kuamini kuwa simu zote zinazotoka nchini China ni feki.

“Pia tofauti na mawazo ya wengi kuwa bidhaa zote kutoka China ni feki au ni za kiwango cha chini katika ubora, Huawei kama bidhaa ya kimataifa tumeendelea kuthibitisha msimamo wake kutengeneza bidhaa zilizo bora kwa wateja wetu katika masoko yetu yote,” anasema Jacko.

Kuhusu ubora wa vifaa vya kampuni hiyo, Jacko anasema kuwa, “Huawei tunaamini kuwa ubora ndio fahari yetu, zawadi ya ubora China ni alama ya msimamo endelevu wa Huawei katika ushindi. Kwa takribani miaka ishirini Huawei kama kampuni iliyojikita kutimiza mahitaji ya wateja, imeweka mkazo katika uvumbuzi na ubora wa bidhaa.

“Huawei itaendelea kufanya juhudi katika ubora na kutengeneza bidhaa zilizobora kwa wateja wetu duniani na Tanzania. Mahitaji ya wateja yamekua kiangalizo kikubwa katika shughuli za zetu toka mwaka 1987,” anasema.

Katika safari ya ubora, mwaka 2014 kampuni hiyo ilishika nafasi ya 94 kwenye Interbrand Top 100 ya Kampuni zinazothaminiwa duniani, ikiwa Kampuni ya kwanza kutoka China kuingingia katika orodha hiyo.

Mwaka mmoja baadae, Huawei imepata mafanikio zaidi na kushika nafasi ya 88. Kiujumla, katika ripoti za hivi karibuni imeshika nafsi ya 47 na ikiwa na thamani ya dola bilioni 19.7. Hii imefanya Huawei kuwa kampuni ya kwanza ya kichina kuingia katika 50 bora.

“Kampuni

yetu

pia imetambuliwa na shirika la Kimarekani ‘US-based Reputation Institute’ kama kampuni pekee ya kichina kuwa katika kumi bora ya Kampuni zinazoheshimika China.

“Tunashukuru kwa ushirikiano tunaoupata TCRA na wadau wetu kwa ujumla, hivyo tunawahaidi Watanzania wote kupata na kufurahia simu zilizohalisi na kwa bei nafuu, kwani tayari tumetoa ahadi ya kuongeza ubora kwa asilimia 30 kila mwaka,”anasema.

Huawei ipo nafasi ya 3 katika usambazaji wa simu duniani kwa mwaka 2015 ilikiwa imesambaza zaidi ya simu milioni 110 ulimwenguni.

Kampuni hii inamiaka siyo zaidi ya sita kwenye biashara hii ya utengenezaji simu lakini tayari imezipiku kampuni kubwa kama, Sony, HTC na hata LG ambazo zilikuwa ni kampuni kubwa kwenye biashara hiyo kipindi cha nyuma.

Hivyo kunauwezekano mkubwa wa kampuni hii kuiondoa Apple kwenye nafasi ya pili kwani inaonekana kuw ana watendaji wanaofanyakazi kwa nguvu zote ikichangiwa kuwa imefanikiwa kujipenyeza kwenye masoko ya Ulaya na Marekani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei nchini, Bruce Zhang

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.