‘Wapiga dili’ ni akina nani, mbona hawatajwi?

Rai - - MAKALA -

Tmaanani, kama nilivyotaja hapo juu, muda mrefu wa kutupiana mpira miongoni mwa wakubwa wakiwemo mawaziri ambao katika hali ya kawaida ya utawala bora, hawakutakiwa kuona sakata linafika hadi kwa rais.

Na kama miongoni mwa ‘wapiga dili’ hao ni vigogo katika utawala, basi hakuna haja ya kuwakawiza katika kuwatumbua, kama vile anavyofanya kwa wale wa ngazi za chini. Watu wanaweza kuanza kusema kwamba Rais sasa anachagua yaani anafanya ‘ubaguzi’ – (discriminates) katika utumbuaji wake. Hii haipaswi kuwa hivyo kwa rais huyu aliyedhamiria kusafisha kabisa ufisadi wote na chembechembe zake katika jamii.

Sakata hili ni katika muendelezo tu wa migogoro mingine ambayo imekuwapo na imekuwa ikiendelea miaka nenda miaka rudi bila ya kupatiwa ufumbuzi kwa sababu tu kiini cha migogoro yenyewe ni wakubwa katika utawala. Mfano wa hili ninalolisema ni mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo. Ni mgogoro ulioanza mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati wa utawala wa Awamu ya Pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Wiki iliyopita Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alimuagiza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa takribani miaka 20 katika pori Tengefu la Loliondo wilayani Ngororongoro mkoani Arusha.

Waziri alitoa maagizo hayo katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika kata ya Ololosokwan ikiwa ni sehemu ya ziara yake wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Kilichonishangaza ni kwa nini Waziri Mkuu aone kwamba mgogoro huu unaweza kutatuliwa na Mkuu wa Mkoa, kwa nini asitatue yeye mwenyewe? Nina sababu zangu za kusema hivi.

Kwanza mgogoro wenyewe si wa juzi au jana, ni wa miaka 20 na tangu wakati huo kumekuwepo Wakuu wa Mikoa zaidi ya kumi, na idadi ya wakuu wa wilaya wa Ngororongoro ndiyo usiseme. Na hiyo achilia mbali idadi ya Wabunge waliokuwapo eneo hilo. Wote hawa ni makada wa chama tawala – CCM na wote walishindwa kutatua huo mgogoro kwa miaka 20. Iwezeje leo hii Mkuu wa Mkoa wa sasa atatue mgogoro huo ndani ya mwezi mmoja?

Na hawa wote walishindwa kwa sababu gani? Kwa sababu haukuwa katika kiwango (level) yao ya kiutawala kuutatua. Level ya mgogoro huu ni kitaifa vinginevyo ni kuzunguka zunguka tu pale pale kama ilivyozoeleka.

Kama tunavyofahamu mgogoro ulianzia mapema miaka ya 90 pale mwekezaji mmoja kutoka nchi za Ghuba – kampuni ya uwindaji ya Ortello Business Corporation (OBC) alipopewa eneo la uwindaji na hivyo kuwalazimu jamii za ufugaji na kilimo zikiwemo mle kuhamishwa. Kuna waekezaji wengine pia kutoka nje na ndani ya nchi nao wamepewa maeneo sehemu hiyo.

Mengi yameandikwa kuhusu mwekezaji huyu kuhusu kuwanyanyasa wakazi wa eneo hilo ingawa inawezekana mengine yalikuwa ya kutia chumvi. Hata hivyo kuna tuhuma kwamba wanaochochea mgogoro huo ni mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayodaiwa kujikita eneo hilo kuzitetea jamii za ufugaji dhidi ya wanachokiita ‘uvamizi’ wa wawekezaji wa maeneo yao (ikiwemo kampuni ya OBC).

Na kama ni hivyo basi mgogoro hauwezi kutatuliwa kwa njia anayotumia Waziri Mkuu ya kumsukumizia Mkuu wa Mkoa. Mkuu wa Mkoa hawezi kutoa maamuzi mazito kuhusu wawekezaji walioko eneo hilo kwa miaka 20 – hili ni suala la wizara husika ya Maliasili na Utalii – watoa vibali vya maeneo ya kuwindia.

Siamini iwapo wakati, kwa mfano, OBC wanapewa liseni, mamlaka za mkoa, wilaya au hata tarafa zilishirikishwa katika maamuzi hayo.

Kiwanda cha saruji cha Dangote

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.