Uhalifu uliotikisa mwaka 2016

Rai - - MAKALA -

wanyonya damu.

“Watu watatu walikutwa wamefariki dunia huku miili yao ikiwa imeungua vibaya baada ya kukatwakatwa na mapanga na kuchomwa moto na wakazi wa kijiji hicho.

“Waliouawa walikuwa kwenye gari namba STJ 9570 ya Toyota Hilux, mali ya Kituo cha Utafiti cha Udongo na Maendeleo cha Selian mkoani Arusha.

“Katika hili walikuwamo watafiti wawili na dereva wao na mmoja kati yao alikuwa ni mwanamke,”alisema.

Chanzo cha mauaji hayo ni mwanamke mmoja aliyepiga yowe kuwaita wananchi wenzake akiwaeleza jinsi alivyoona wanyonya damu.

“Taarifa hizi zilipofika kijijini, Mchungaji wa Dhehebu la Christian Family, Patrick Mgonela (46) ambaye ni mkazi wa kijiji hicho, alitangaza kupitia kipaza sauti cha kanisa kuwa wamevamiwa na wanyonya damu.

Mauaji ya Tanga

gari

Mauaji ya watu saba wa familia moja

Tukio lingine lililotia simanzi kwa mwaka huu lilitokea katika Kijiji cha Sima, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, baada ya watu saba wa familia moja kuuawa kinyama kwa kukatwakatwa mapanga Mei 11 mwaka huu.

Familia hiyo ilivamiwa na watu ambao idadi yao haikutamnbulika usiku wa manane wakiwa wamelala katika nyumba tofauti.

Taarifa zilizopatikana wilayani Sengerema na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, zilidai kuwa mauaji hayo huenda yalifanywa na watu wawili au mmoja na chanzo chake hakijajulikana.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ambaye ni mmoja wa wanafamilia, Patrick John akielezea tukio hilo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama, alisema wavamizi hao baada ya kuingia ndani wakiwa na mapanga waliwaua wanafamilia hao kikatili.

Alisema wauaji wakiendelea kufanya unyama huo, ndugu yao Bestina Nasoro (10) alisalimika baada ya kujificha uvunguni na kujifunika nguo.

Mwaka huu pia huenda usisahaulike kwa wakazi wa mkoa wa Tanga ambao kwa namna moja ama nyingine wamekumbwa na dhoruba hii ya mauajia kwa nyakati tofauti.

Itakumbukwa Mei 30 mwaka huu watu 8 waliuawa kwa kuchinjwa na miili yao kutenganishwa na vichwa akiwamo mjumbe wa serikali ya mtaa kufuatia vikundi vya uhalifu kuvamia nyumba za wakazi wa mtaa Kibatini uliopo kata ya Mzizima jijini Tanga hatua ambayo imeleta hofu kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.

Wakizungumza katika eneo la tukio baadhi ya waathirika ambao ndugu jamaa na zao wamechinjwa majira ya saa saba usiku walidai kundi la watuhumiwa wanaokadiriwa kuwa walikuwa watu nane na kuvalia nguo nyeusi walipofika katika nyumba zao waliwaamuru akina baba watoke nje kisha kuwapeleka hadi katika vichaka kisha kuwachinja.

Siku chache baadaye watu wanne waliuawa katika mapambano na polisi yaliyotokea kwenye mapango ya Amboni mjini Tanga, eneo ambalo polisi mmoja aliuawa Februari mwaka jana katika tukio lililohusishwa na ugaidi.

Tukio hilo lilikuwa ni polisi wakiendesha operesheni ya kusaka majambazi waliofanya mauaji katika duka la Central Bakery.

Majambazi hao walivamia duka maarufu la Central Bakery mwezi uliopita na kuwaua watu wanne, kujeruhi wawili na kupora Sh 2.7 milioni baada ya kufanikiwa kuvunja kasiki.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Leonard Paulo aliwataja waliouawa katika mashambulizi ya risasi yaliyotokea katika mapango ya Amboni kuwa ni Nasibu Bakari, Abuu Katada, Abuu Mussa na raia wa kigeni aliyetambulika kwa jina la Idrisa Berato.

Kuuawa kwa Askari wanne

Tukio lingine ambalo liliogopesha wengi mwaka huu ni lile la Agosti 23, mwaka huu ambalo lilihusisha kuuawa kwa askari polisi wanne kufuatia tukio la uporaji lililotokea katika benki ya CRDB tawi la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Waliopoteza maisha kwenye tukio hilo ni pamoja na E5761 CPL Yahaya, F4660 CPL Hatibu na G9544 PC Tito, huku jila la askari mwingine likishindwa kutambulika.

Ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati askari wakibadilishana lindo na kwamba mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva.

Mauaji ya msikitini Mwanza

Mei 18 mwaka huu jijini Mwanza katika msikiti wa Masjid Rahman uliopo Ibanda Relini mtaa wa Utemini maarufu kama mapankini kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana,kulitokea mauaji yaliyofanywa na wasiozidi 15.

Watu hao walikuwa wamevalia mavazi ya kuficha uso wakiwa na mapanga, shoka na bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia ghafla kwenye msikiti huo.

Wakati waumini wa msikiti huo wakiwa wanaswali na kuzima taa na kutoa sauti wakisema “kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi?” na hapo hapo wakaanza kuwakata kwa mapanga baadhi ya waumini katika sehemu mbalimbali za miili yao.

Waliouawa kwenye tukio hilo ni, Feruz Ismail Elias(27)ambaye ni Muha Imamu wa msikiti huo na mkazi wa Ibanda reline, mwingine ni, Mbwana Rajab(40) ambaye ni Mbondei na mfanyabiashara na Khamisi mponda(28) dereva wa kiwanda cha samaki (TFP) ambao wote walijeruhiwa sehemu za kichwani, shingoni na mikononi.

Mwingine aliyejeruhiwa ni, Ismail Abeid Ghati (13), mwanafunzi wa madrasa katika shule ya Jabar hila iliyoko Nyasaka.

Kutokana na hali hiyo, waumini wengine walifanikiwa kukimbia huku wakipiga mayowe yaliyopelekea wahalifu hao kukimbia na kurusha ndani ya msikiti chupa mbili za konyagi zilizokuwa na petroli na tambi za moto, chupa moja ililipuka lakini haikuleta madhara makubwa.

Mauaji ya dada wa bilionea Msuya

Hili ni tukio lingine ambalo lilimhusisha aliyekuwa Dada wa marehemu Erasto Msuya aliyetambulika kwa jina la Anathe Msuya ambaye alikuwa ni Mtumishi wa Wizara ya Fedha, aliyeuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam.

Anathe aliuawa nyumbani kwake eneo la Kibada block 16, Kigamboni, ambako ilibainika kuwa wauaji hao hawakuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.

Anathe alikuwa ni dada wa marehemu Erasto Msuya ambaye alikuwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliyeuawa kwa kufyatuliwa risasi.

Hayo ni baadhi ya matukio makubwa ambayo yameweza kutokea mwaka huu na kuacha simanzi kubwa kwa ndugu jamaa na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo kwasasa hali ya kiusalama imeonekana kuimarika zaidi nchini licha ya kuwapo kwa changamoto za hapa na pale kutoka kwa baadhi ya watu wasiopenda kuona amani ikitawala.

Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na lile la kukutwa kwa miili ikiwa imefungwa ndani ya viroba na kutupwa mtoni kwenye mkoa wa Pwani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.