Mambo muhimu kwa JPM kupambana na rushwa CCM

Rai - - MAKALA - NA NASHON KENNEDY

MWENYEKITI wa CCM Taifa, Rais John Magufuli ametangaza vita ndani ya chama hicho kikongwe cha siasa ambacho ni miongoni mwa vyama vikongwe Kusini mwa jangwa la Sahara vilivyoendesha harakati za ukombozi kwa baadhi ya nchi za Bara la Afrika.

JPM alitangaza vita hiyo hivi karibuni mara baada ya kuendesha vikao vyake vya kwanza vilivyofanyika jijini Dar es Salaam tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho mapema mwaka huu.

Pamoja na kufanya mabadiliko ya uongozi huku akimteua Humprey Polepole kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi ndani ya chama, mambo mengine aliyosisitiza Dk. Magufuli ni pamoja na kupambana na rushwa ndani ya CCM bila suluhu.

Juhudi za Rais Magufuli za kupambana na rushwa hazikuanza leo, alianza wakati akiwa Naibu Waziri na Waziri Kamili wakati wa awamu ya tatu na ya nne ya uongozi wa Marais wastaafu wa awamu hizo, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

Moja ya mambo aliyokerwa nayo kwa wakati huo, ni pamoja na watu waliovunja sheria kwa kujenga kwa makusudi ndani ya hifadhi ya barabara na wale waliokuwa wakijihusisha na uvuvi haramu, ambapo baadhi ya vigogo nao wamekuwa ni wahusika wakubwa wa biashara ya uvuvi haramu ambapo hutumia makokoro ambayo hayaruhusiwi kwa mujibu wa sheria.

Tuliziona juhudi za Dk. Magufuli za kupambana na yote hayo kwa juhudi na maarifa licha ya kukumbana na changamoto za hapa na pale za kiutendaji, ambazo wakati mwingine ziliweza kumkwaza kwenye utendaji wake.

Suala la rushwa ni tete kwani hata vitabu vya maandiko matakatifu vinaonyesha ni jinsi gani rushwa iliweza kumshawishi mmoja wa wanafunzi na kipenzi chake Yuda ambaye alimuuza kwa rushwa.

Athari ya rushwa hata kwa mataifa makubwa duniani bado ni changamoto, lakini pia rushwa kwa nchi yenye watu maskini kama Tanzania madhara yake ni makubwa zaidi.

Lakini ifahamike kuwa madhara ya rushwa katika uchaguzi ni kuondoa uhuru wa mpiga kura, wagombea wenye vipaji na wenye uwezo wa kuongozahushindwakugombea kwenye uchaguzi kwa kukosa fedha, na hii huharibu dhana nzima ya uwakilishi kwa kuwa watakaokuwa wamechaguliwa hawana ridhaa kamili ya wapiga kura wao ( wananchi).

Rushwa pia ina madhara ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kiasi cha kuifanya jamii ya watu wanaoishi pamoja kuwa na kiu ya kusubiri kupewa na kufanya maamuzi ya mkato kwa kumpa haki mtu ambaye hastahili na kumchagua ambaye hastahili kwa ushawishi wa rushwa.

Matukio yote ya rushwa huonekana kwenye chaguzi mbalimbali za chama na serikali ambazo zimekuwa zikiendeshwa kuanzia ngazi za vitongoji, mitaa, vijiji, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa.

Uchaguzi ni hatua muhimu ya wananchi kuonyesha ukomavu wao wa kidemokrasia na kupitia taasisi zao za vyama wanalo jukumu la kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa uchaguzi kwa kuwachagua viongozi bora na sio bora viongozi kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.

Wanatakiwa kufanya maamuzi yao bila vitisho wala kushurutishwa kwa rushwa au namna yoyote ile maana uchaguzi ni jambo linalohusu maisha yao. Mwananchi akimchagua diwani au Mbunge makini maana yake ni kuwa atakutana na fedha zake za kodi kwenye barabara, huduma bora ya afya na ujenzi wa miundombinu imara itakayomwezesha kusafirisha mazao yake kwenda kwenye soko na huduma zingine muhimu.

Mwananchi anapokubali kupokea hongo ya fedha, rushwa, t-shirt na kofia za vyama vya siasa, maana yake anauza uhai wake, wa watoto wake na wajukuu wake kwa kipindi ambacho uongozi uliochaguliwa utakoma kuwepo madarakani.

Kwa miongo kadhaa sasa, chaguzi nyingi zinazofanyika ndani ya CCM zimekuwa zikigubikwa na rushwa ambayo imekuwa ikifanyika kisayansi zaidi. Zipo rushwa ambazo hutolewa kama mikopo ya kwenda kwenye Saccos na zingine hutolewa kama zawadi au misaada ya ujenzi wa majengo ya taasisi za umma na baadhi ya wagombea ambao sio waaminifu.

Kwa kifupi rushwa ndani ya CCM ina sura za kutisha, hubadilika mithili ya rangi ya kinyonga, na watoaji wa rushwa hiyo ni watu wenye mbinu nyingi kulingana na mazingira ya mahali, nyakati na sehemu na kwa nani anayetarajiwa kukabidhiwa rushwa hiyo.

Na ndio maana ilifika mahali rushwa ndani ya chaguzi za chama ilipata baraka kutoka kwa vigogo huku ikipewa majina laini likiwemo jina la takrima, ambalo kwa miaka kadhaa tulijuhudia mijadala mikali ya ndani ya chama hata bungeni ya kutoa baraka kwa jina hilo.

Katika uchaguzi Mkuu wa Chama uliopita, mimi nilikuwa miongoni mwa wagombea wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia Wilaya ya Ilemela. Kwenye kinyang’anyiro hicho sikuweza kubahatika kuchaguliwa katika nafasi hiyo, na badala yake Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ilemela ulimchagua Israel Mtambarike kuwa MNEC wa Wilaya ya Ilemela, na viongozi wengine wa Chama Mkoa na wilaya zingine walichaguliwa.

Safari yangu haikuishia hapo, katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka jana, niligombea nafasi ya udiwani kupitia CCM katika Kata ya Kisaka, wilaya ya Serengeti, ambapo nilishiriki kikamilifu kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya chama, ingawa vilevile kura hazikutosha na hivyo niliishia kwenye kura za maoni.

Kuna mambo kadhaa ambayo niliyagundua ambayo hasa yamekuwa yakiendeshwa na chama katika kuwapata wagombea wake huku yakiwa na changamoto kubwa ya tatizo la rushwa. Kiuhalisia rushwa ndani ya CCM ni mbegu iliyoota kuanzia kwa wana CCM wenyewe, viongozi na hata marafiki na wapenzi wa CCM.

Ni kitu cha kawaida sana pale wana CCM wanapomjua mtu anayetaka kutia nia ya kugombea ikiwa hata kwa tetesi, wao humuendea na kumwambia anawaachaje. Ushawishi wa rushwa ndani ya CCM huanza kujengwa kisaikolojia kwa wagombea kabla hata ya kuitishwa kwa vikao muhimu vya chama.

Ningeshauri kwa wanachama wanaonekana kuwa na ushawishi mkubwa wa rushwa ndani ya chama, na wao wadhibitiwe kwa kufutiwa uanachama wao.

Uchambuzi na kigezo muhimu kwa mgombea ndani ya CCM sio sifa za uongozi na uwezo wa kuongoza bali ni uwezo wa

Rais John Magufuli

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.