Demokrasia ya ndani ya Chadema iko wapi?

Rai - - MAKALA -

Baada ya kupitia machapisho kadhaa, juu ya uchaguzi wa viongozi Chadema kwa iitwayo Kanda ya Nyasa, umenichangamsha kutafakari kidogo. Rafiki yangu Dady Igogo mwanachama na kiongozi wa Chadema Iringa, ameeleza kwa masikitiko kilichotokea baada ya (MwenyekitiTaifa - Chadema) kuja na jina mfukoni la mgombea ambaye ni Peter Msigwa. Dady akaishia kwa kumuasa Msigwa nakutoa ushauri kwa chama chake.

Vilevile rafiki yangu Pascal Mwanjabala aliyejitambulisha wazi kutokua mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini ametoa rai juu ya ubabe uliofanywa na Mwenyekiti kwa kufukuza baadhi ya wanachama waliostaajabishwa na taratibu za uchaguzi kwa kutokubaliana kwao na mwenyekiti. Waliostaajabishwa kufukuzwa nje na hivyo kuishia kutopiga kura. Lakini namba hazikudanganya Msigwa hakuwa chaguo la walio wengi.

Niwazi asipounganisha makundi hayo hatoweza kuwaongoza atabaki kuwa mwakilishi wa Mwenyekiti Nyasa, Lakini tafakuri yangu inajikita kwa chama kinachohubiri ukiritimba wa vyama vingine vya siasa hasa msemo wao uliomaarufu sana kwa sasa wa Udikteta’ na kubinywa kwa demokrasia!

Mtizamo wangu ni kwamba Mwenyekiti si mjinga kufanya yaliyofanywa bali ni azma iliyowazi ya kupanga mtandao ‘ ndani ya chama hicho na kujichimbia Uenyekiti wa kudumu! Na wapiga kura ni hawa wanaoteuliwa/chaguliwa sasa.

Kama mtaniruhusu kulinganisha! Hiki kifanywacho na viongozi wa Chadema Taifa hakina tofauti na kile kilichoitwa uhaini wa Prof. Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe na Samson Mwigamba, na kupelekea kufutwa kwao chamani kwa kilichoelezwa kuanza mikakati ya uchaguzi mapema, japo chama kilikuta mpango ule kama jaribio la mapinduzi!

Hata hivyo, Tunaomba mahubiri ya demokrasia kama lilivyo jina la chama yaanzie chamani kwanza, Chama kinachohubiri nia ya kushika dola ni muhimu kijiandae kwanza kwa kuimarisha chama-Taasisi, ule ujanja ujanja wakupachikana utaendelea hata mkikabidhiwa dola, jambo ambalo halikubaliki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.