Tuna safari ndefu kuujenga upinzani wa dhati

Rai - - MAKALA - Com/raphael.lukindo” aphael Joseph Lukindo

HII tabia ya kuangushiana vitu vyenye ncha kali katika chaguzi za ndani za vyama vya upinzani ni kawaida sana ndani ya vyama hivyo si nzuri. Na hii ni kwa sababu viongozi wengi wa vyama vya upinzani hawataki kuwa na vijana ambao ni vijana wale wa kizazi cha kuhoji, wanataka watu ambao watakuwa karibu yao wale wa ndio mzee na sio wale wa kusema kwanini? Off course wanapenda sana kufanya kazi na watu watakaowasaidia kufanikisha mambo yao.

Mfano mmoja tu ndani ya chama fulani Mr. Kadawi Limbu alipigwa na kitu chenye ncha kali akaitwa mamluki kutoka Chadema kisa tu huyu mtu alikuwa ana hoja za msingi sana na alikuwa sio mtu wa ndio mzee, ndani ya chama hicho hicho katika jimbo la Muhambwe ndugu yangu kijana mwenzangu ambaye alitumia muda wake na rasilimali nyingi sana kujenga chama na kuandaa chama ndani ya jimbo la Muhambwe huko Kibondo Kigoma lakini mwisho wa siku alipigwa na kitu chenye ncha kali tena utosini hadi ikabidi akauze nyumba ya urithi. Ndani ya chama hicho hicho tu kuna katibu mmoja wa kwanza wa mkoa na yeye alipigwa na hicho kitu cha ncha kali. Hata mimi nimeshapigwa na kitu hicho aisee inatia huzuni sana. Hata kada mtiifu wa ACT kaka yangu Bwandu Ndaje na yeye alipigwa na hicho kitu tena utosini kabisa maana kwenye kura za maoni aligombania na kivuli na kivuli kikashinda.

Ukiangalia aina ya watu ambao wanapigwa na vitu hivyo kichwani utajua kwanini hawatakiwi na ukiangalia wale wanaopewa nafasi utajua kwanini wanatakiwa. Tuna safari ndefu sana katika kuujenga upinzani wa dhati na wa kweli hapa Tanzania.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.