2016 talaka zimemwagwa kama njugu Z’bar

Rai - - MAKALA - NA MUHAMMED KHAMI

NDOA ni makubali makubaliano ya baina ya pande mbili kati ya mume na mke kwa lengo la kujenga familia moja. Kwenye maisha ya ndoa kuna mazuri na mabaya ambayo huwakabili wanandoa hao.

wake pamoja na kumtaka aondoke na watoto wote kwenye nyumba hio huku akishindwa kuelewa ni vipi ataweza kuwahudumia watoto hao wadogo waliohitaji mahitaji mbali mbali kama watoto wengine.

Anasema hakua na budi na kukubaliana na hali hiyo na akaamua kurudi nyumbani kwao kuishi na wazazi wake ingawa ilimuia vigumu kutokana na hali ya maisha kuwa duni kwenye familia yake.

Anasema awali aliishi kwenye ndoa hio kwa amani na upendo lakini hafla aliekua mume wake alibadilika na kuanza tabia za kumpiga na kumfukuza kila mara kabla ya maamuzi ya kumuacha.

Nae Mwanshamba Said Haroud wa Mitondooni Mjini Magharib Unguja anasema pia aliishi kwenye ndoa kwa miezi sita tu tokea kuolewa kwake na badae kuachika huku aliekua mume wake akieleza sababu kadhaa za kumuacha ikiwa ni pamoja na alichokidai ugumu wa maisha.

Anaeleza kwamba kabla kuolewa kwake mwanaume huyo alimshawishi sana na kuamini kuwa angeweza kuishi maisha mazuri ya ndoa jambo ambalo lilitokea kuwa kama ndoto kutokana na hali alioikuta kweye ndoa.

‘’Wanaume wengine wana maneno mazuri wanapokuja kukuchumbia unaamini haraka sana kuhisi huyu ni mwanaume lakini ah wapi leo najutia kwanini nilikubali kuolewa na mwanamke asiekua na dira’’alieleza kwa mamasikitiko Mwanshamba.

RAI likiwa katika ofisi ya kadhi Vuga Mjini hapa lilishuhudia makundi ya kina Mama na wanaume kadhaa waliofika hapo wengi wao wakiwa na kesi za ndoa kama ilivo kawaida.

Baadhi ya wanandoa walikua wakigombana nje ya Mahakama hiyo huku kila mmoja akieleza hisia zake kwa mwenzake baada ya kufika kuskilizwa kwa kesi zao.

Baadhi ya kina Mama hao kwa nyakati tofauti walisikika wakisema Mahakama hio imekua na tabia ya kulimbikiza kesi bila ya kuzitolea hukumu kwa maamuzi huku wanandoa wakiendelea kuteseka kwenye ndoa zao kwa kusubiria maamuzi ya Mahakama hio maalumu inayohusika na wanandoa.

Juma Haroub Saidi kijana anaeishi kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa anaeleza kuwa ndoa ni maisha mazuri kwa wanandoa wenyewe iwapo watakuwa tayari kuishi kwa utulivu na amani bila ya kulazimishana vitu wasivyokua na uwezo navyo.

Anabainisha kutokana na hali halisi ya baadhi ya wanandoa wengi miongoni mwa familia kujaribu kuiga kutoka kwa mashoga zao au marafiki zao ni sababu kubwa zinazopelekea kuongezeka kwa wingi talaka kwa wanandoa.

Mwanafunzi wa darasala tisa skuli mjini hapa aliekataa kutajwa jina lake kwenye makala hii alisema kutengana kwa wazazi wake kunamkosesha amani pia kupunguza ari ya kusoma kila anapofikiria ugumu wa maisha unaomfanya Mama yake kuhangaika peke yake bila ya msaada wa yoyote ule.

‘’Nakumbuka niliamshwa kutoka usingizini na Mama yangu huku akilia sikuweza kujua kwa haraka analilia nini kwa vile nilikua natoka usingizini aliniambia niamke tuondoke Baba ametufukuza’’alieleza mtoto huyo huku machozi yakimtoka.

Ni mwaka wa pili sasa tokea Babake kuachana na Mama yake hajawahi kupata msaada wowote hule kutoka kwa baba yake mzazi jambo ambalo linamsikitisha sana na kukosa mapenzi na mzazi wake huyo.

Kwa upande wake Kaadhi mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis amekiri uwepo wa ongezo wa takala kwa wanadoa visiwani hapa huku akisema miongoni mwa sababu hizo ni ukosefu wa uvumilivu katika ndoa nyingi.

Alibainisha kuwa maisha ya zamani na sasa ni tofauti sana kwa wanandoa kwa vile zamaani wanandoa wengi waliheshimu taratibu za ndoa na kukubali kuwa wavumilivu katika maisha.

Lakini pia hakusita hapo alieleza zipo baadhi ya familia za wanandoa nazo pia huchangia kwa kiasi kikubwa kuvunjika kwa ndoa kutokana na kuwalazimisha watoto wao kuolewa na waume wasiopenda.

Akizungumzia kuhusu ukosefu wa maadili kwa wanandoa alisema nalo ni miongoni mwa sababu ambazo hupelekea ukosefu wa uwelewa wa kina kwa wanandoa wenyewe pia aligusia suala la utandawazi ni miongoni mwa changamoto za ndoa nyingi hivi sasa.

‘’Utaona wanandoa wegi sasa wanaiga tamaduni za nje na kutaka mambo yalio chini ya uwezo wa waume zao jambo ambalo limekua changamoto kwa ndoa nyingi visiwani hapa’’alieleza Kaadhi huyo.

Aidha, kaadhi huyo akitolea ufafanuzi kuhusu mrundikano wa keshi kwenye Mahakama yake alisema wanachokifanya wao kama Mahakama ni taratibu za kuskiliza kesi kisheria hawawezi kutolea majibu kwenye kesi za ndoa kama watu wanavofikiria .

‘’Unajua mwandishi watu wanadhani kesi hizi ni rahisi unaweza kuja leo na kesho kesi ikaamuliwa ,hatuwezi kufanya hivyo kesi za ndoa zinahitaji kuskilizwa pande zote mbili bila ya kuacha upande wowote hule na kisha kutolea maamuzi’’ anafafanua zaidi.

Anaendelea kwa kutoa wito kwa wanandoa na wale wote wanatoka kuingia kwenye ndoa kujidhatiti kabla ya kufanya maamuzi hayo wakijua kuwa ndoa inahitaji uvumilivu mkubwa.

Katika kuhakikisha suala la haki za wanawake linapatiwa ufumbuzi kwenye maeneo mbali mbali visiwani hapa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA)tawi la Zanzibar halikukaa kimya linaedelea kutoa elimu za haki za msingi kwa kina Mama ili kuweza kupambana na vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kupewa talaka na kukosesha watoto haki zao za msingi ikiwemo elimu bora.

Sasa imefika wakati jamii jamii kupaza sauti zetu kutambua kuwa mwananmke ni sehemu ya maisha yetu na Mama wa Taifa letu tuna kila sababu ya kumtunza mwanamke kwa maisha bora ya leo na kesho.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.