TUHUMA

Rai - - HOJA MCHANGANYIKO -

wanachunguza ukubwa wa tuhuma dhidi ya Rais Park hasa kuhusu ‘njama’ baina yake na Choi katika kuyapa misukosuko makampuni makubwa nchini humo kutoa michango kwa taasisi mbili ambazo alikuwa anazimiliki.

Baada ya kuvuliwa madaraka na Bunge, Park kabakia na urais wa jina tu, akisubiri Mahakama ya Katiba kuthibitisha au azimio la Bunge lililotaka ashitakiwe mahakamani.

Kim Ki-Choon amekuwa na mahusiano ya karibu sana na familia ya Rais Park, ambaye pia alifanya kazi chini ya rais Park Chung-hee, baba yake Rais Park Geun-hye.

Mahusiano haya ndiyo yalipelekea tuhuma kwamba lazima atakuwa anafahamu vyema ushawishi mkubwa aliokuwa nao Choi dhidi ya Rais Park hata kuvifanya vyombo vya habari nchini hum kumpachika jina la “Mganga wa Kike.’ Moja ya mashitaka dhidi ya mwanandani huyo wa rais park ni kuingilia masuala ya kitaifa wakati hana wadhifa wowote katika utawala.

Choi pia andaiwa kutoa ushawishi mkubwa kwa Rais Park katika uteuzi wake wa watendaji katika nyadhifa kuu za kitaifa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.