Mabadiliko makubwa soka la Tanzania mwaka 2017

Rai - - MICHEZO KIMATAIFA -

YALIYOPITA si ndwele tugange yajayo. Ndiyo tunavyoweza kusema hivi sasa tukiwa tunauaga mwaka 2016 na kuukaribisha 2017 huku kukiwa na matarajio makubwa ya kimageuzi katika soka la Tanzania.

Kauli hiyo ni faraja kubwa kwa watanzania ambao hawajawahi kabisa kuona wala kusikia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ikishiriki fainali za Kombe la Dunia, pia ikiwa ni miongo kadhaa sasa wakishindwa kushuhudia ikicheza fainali za Afcon.

Tanzazania ilishiriki fainali za AFCON kwa mara ya kwanza na mwisho mwaka 1980 katika Michuano iliyofanyika jijini Lagos, Nigeria na kutolewa katika hatua za awali kabisa baada ya kushindwa kufurukuta na kuishia katika hatua ya makundi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.