Fabio Capello ‘ambeba’Conte

Rai - - MICHEZO KIMATAIFA - MWANDISHI WETU NA MTANDAO

KILA mtu hivi sasa anazungumzia shughuli nzito wanayoionesha Chelsea kwa

kutembeza vichapo kila kukicha ambapo pia mapema wiki hii walifanikiwa kuandikisha ushindi wao wa 12 mfululizo ndani ya EPL baada ya kuinyuka Bournemouth mabao 3-0.

Yote hayo yanatokana na ujio wa Kocha Antonio Conte ambaye amebadilisha mfumo kutoka 4-2-3-1 hadi 3-4-3 baada ya kuanza vibaya msimu huu kwa kupokea vichapo vya aibu

kutoka kwa Liverpool na Arsenal. kutoka 4-2-3-1 hadi 3-4-3 baada ya kuanza vibaya msimu huu kwa kupokea vichapo vya aibu kutoka kwa Liverpool na Arsenal. Lakini bado kuliibuka maswali miongoni mwa wadau walioshindwa kuamini kama ni mfumo pekee uliomfanya Conte afanye vizuri kiasi hicho au kuna lingine nyuma ya pazia?

Ni maswali hayo yaliyomfanya Conte atoboe siri kwamba mtu aliyemsaidia pia ni kocha wa zamani wa England, Fabio Capello, ambaye alimpasha kuhusu ugumu wa soka la England.

Katika mahojino na gazeti la Daily Mirror, kocha huyo alifunguka namna Capello alivyomfungua akili kwa kumwelewesha jinsi ligi hiyo ilivyo ngumu mno kutokana na desturi yao ya kutokuwa na mapumziko ya majira ya baridi yanayoharibu mipango ya makocha wengi nchini humo.

Ushauri huo ulimfanya Conte ahakikishe kikosi chake kinazidisha umakini kwenye kila mchezo na hadi kufikia sasa,timu hiyo inatesa kwenye msimamo wa ligi ikiongoza baada ya kufikisha pointi 46.

“Ni changamoto niliyokutana nayo kweli, na nimeshasikia mengi kutoka kwa makocha mbalimbali wakisema kuwa mapumziko wakati wa majira ya baridi ni kitu cha muhimu hasa kutokana na historia ya athari zinazotokea kwenye timu za taifa kwa wachezaji wao kuumia kutokana na kukosa mapumziko,” anasema Conte.

Anasema, Capello mara zote alikuwa akimweleza kukosekana kwa mapumziko ya majira ya baridi kunaziathiri timu za taifa jambo ambalo linampa ugumu kukubali kwamba kweli inamuathiri kwani anaonekana kufurahishwa mno na changamoto hiyo.

“Ni vigumu kwangu kujibu kama ni kweli au hapana kama kucheza wakati wa kipindi cha Krismasi ni tatizo. Lakini kwangu mimi hii ni mara ya kwanza kukutana na jambo hili ila nafarijika kupata changamoto kama hii,” anasema Conte.

Conte anasema kufanya kazi katika sikukuu kama hii pia itakuwa ni changamoto ya kwanza kwa familia yake ambayo ilikuwa imezoea kupumzika wakati akizifundisha timu za Italia na Juventus.

“Mke wangu na binti yangu waliwasili hapa kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi nyumbani kwangu pamoja na kaka yangu na familia yangu, nadhani ni kitu kizuri,” anasema Conte.

Anasema itakuwa mara yao ya kwanza kukutana na hali kama hiyo lakini itakuwa ni vizuri kwa yeye na timu yake kujipanga.

“Katika kipindi kama hiki tulikuwa tukikitumia kwa mapumziko. Wakati mwingine tulikuwa tukienda mjini Lecce ama Torino (Italia) na mara moja tulikwenda Dubai. Ni muhimu kwao kuwa na furaha sikukuu ya Krismasi,” anasema.

Anasema kusherehekea sikukuu ya Krismasi na familia si jambo la muhimu bali ni kufikiria kuhusu mikakati ya kuisaidia timu yake ifanye vizuri katika ligi kuu hasa katika kipindi hiki ambacho timu yake inaongoza msimamo baada ya sikukuu, na atamaliza mwaka akiwa kileleni.

Historia ya Chelsea inaonesha katika misimu ambayo waliongoza ligi hadi kufikia kipindi cha Krismasi, walinyakua ubingwa wa ligi kuu kwa kishindo. Dalili njema kwao zimeshaonekana.

Timu ya Soka ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’

Antonio Conte

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.