Hatima ya Lowassa mikononi mwa Polisi

POLISI wanayo haki ya kunihoji kama wana wasiwasi na matamshi yangu na kwamba huo ni wajibu wao kwa sababu wapo kutekeleza sheria, ila wasiitumie kauli yangu kuminya demokrasia.

Rai - - MBELE - NA GABRIEL MUSHI

HATIMA ya Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, juu ya tuhuma za uchochezi anaodaiwa kuufanya Juni 24, mwaka huu, itajulikana leo. RAI linaripoti.

Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema), alianza kuhojiwa na polisi juzi baada ya kupokea wito wa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI).

Katika mahojiano hayo yaliyofanyika kwa sasa nne katika ofisi za DCI Makao Makuu ya Polisi, jijini Dar es Salaam, Lowassa alituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi wakati wa futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema).

Mwanasheria wa Lowassa, Peter Kibatala ndiye aliyewaambia waandishi wa habari kuwa mteja wake alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi kuhusiana na matamshi aliyoyatoa wakati wa futari hiyo.

Kibatala alisema Lowassa alipokea wito kutoka ofisi ya DCI kwamba aripoti polisi na alifanya hivyo bila kukaidi, ambapo mahojiano ya awali yalijikita katika kile alichodai kuwa ni kauli za uchochezi.

Alisema amechukuliwa maelezo yake ya onyo na alijidhamini mwenyewe na kutakiwa kurudi tena leo.

Duru za habari zimeliambia RAI kuwa mahojiano ya leo yanabeba hatima ya Lowassa ambayo ni aidha, kuachiwa tena ama kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma hizo.

Imeelezwa kuwa kauli hizo za Lowassa na uamuzi wa jeshi la polisi wa kumuita kwa ajili ya mahojiano zinaweza kuamsha joto jipya la kisiasa nchini.

Wanaobeba hoja hiyo wanaeleza kuwa Lowassa bado ni mwanasiasa mwenye uungwaji mkono mkubwa wa wananchi wa kada na rika mbalimbali, hivyo kauli yake huwa inapokelewa kwa uzito mkubwa tofauti na ilivyo kwa wanasiasa wengine.

Mbali ya kauli zake kupokelewa kwa uzito mkubwa, lakini pia wafuatiliaji wa mambo wanabainisha kuwa hata Serikali inapaswa kushughulika na mwanasiasa huyu kwa umakini mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa anaouungwaji mkono wa watu wengi, lakini pia alishawahi kuhudumu kama Waziri Mkuu wa nchi.

Hadi sasa kumekuwa na hisia na mitazamo tofauti juu ya sakata hili la Lowassa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini, wanasiasa na wasomi.

Wapo wanaoamini kuwa ni sahihi kwa jeshi la Polisi kumwita na kumuhoji mwanasiasa huyo na ikibidi kumpandisha kizimbani, lakini pia wapo wanaopingana na hilo kwa madai kuwa alichokisema ni maoni yake ambayo yanapaswa kuheshimiwa.

Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba, ni baadhi ya viongozi wa dini wanaoamini kuwa hakuna kosa lililofanywa na Lowassa.

Sheikh Katimba alionesha kushtushwa na hatua ya Lowassa kuitwa kuhojiwa polisi kwa sababu alichozungumza mbele ya Masheikh hakikuwa na nia ovu.

“Alizungumza kwa nia njema na wala si uchochezi, ni ukweli kwamba masheikh wako ndani kwa muda mrefu sasa, tukumbuka kuwa mtuhumiwa haimaanishi umetenda kosa. Tunamuomba Rais Dk. John Magufuli aliangalie suala hili.

“Tunamuunga mkono Rais katika mambo mbalimbali anayoyafanya, lakini tunandelea kumuomba kama wale masheikh walioko ndani hawana hatia waachiwe,” alisema Sheikh Katimba.

Maoni ya kada wa chama cha NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza yanalandana na yale ya Sheikh Katimba.

Katika mazungumzo yake na RAI, Ruhuza alisema anashangaa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.