Bayern walivyotumia miezi 12 kumpoteza Renato

Rai - - MBELE - MWANDISHI WETU NA MITANDAO

Ni mwaka mmoja pekee umepita tangu kinda Renato Sanches alipokuwa aking’ara na timu ya Taifa ya Ureno katika fainali za mwaka jana za Mataifa ya Ulaya (Euro 2016). Mbaya zaidi, hivi sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 19, ametemwa kwenye kikosi hicho kinachoshiriki Kombe la Mabara

Ni mwaka mmoja pekee umepita tangu kinda Renato Sanches alipokuwa aking’ara na timu ya Taifa ya Ureno katika fainali za mwaka jana za Mataifa ya Ulaya (Euro 2016).

Mbaya zaidi, hivi sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 19, ametemwa kwenye kikosi hicho kinachoshiriki Kombe la Mabara nchini Urusi.

Baada ya kushindwa kufanya vizuri katika msimu wake wa kwanza Bayern Munich, Sanches ameikosa nafasi hiyo ingawa ameitwa kwenye kikosi cha vijana wenye umri wa chini ya miaka 21 wanaocheza Euro mwaka huu.

Hata hivyo, alijikuta akianzia benchi katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Serbia ingawa alitoa ‘asisti’ ya bao la dakika za majeruhi katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata makinda wa Ureno.

Mwaka jana, kipindi kama hiki, Sanches alikuwa moto wa kuotea mbali nchini Ufaransa zilikofanyika fainali hizo za Euro 2016.

Kiwango chake klizuri kilimuwezesha kuwa nyota wa mchezo katika mchezo wa hatua ya mtoano dhidi ya Croatia.

Lakini pia, alifunga bao muhimu dhidi ya Poland na kuiwezesha timu yake ya Ureno kutinga nusu fainali.

Zaidi ya hapo, Sanches aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kucheza fainali wakati Ureno ilipocheza na wenyeji Ufaransa.

Akiwa na medali shingano mwake na tuzo aliyokuwa ameibeba ya mchezaji mwenye umri mdogo, alikuwa tumaini jipya kwa soka la Ureno.

“Renato atakuwa bonge la mchezaji,” alisema kocha wa Ureno, Fernando Santos.

Mkongwe Thierry Henry aliwahi kumwagia sifa chipukizi huyo ambaye amekuwa akitajwa kuwa na umri mkubwa kuliko vyeti vyake vinayvoonyesha, madai ambayo pia yamewahi kutolewa na rais wa zamani wa Benfica, Bruno de Carvalho, na aliyekuwa kocha wa Ufaransa, Guy Roux.

Klabu kadhaa za Ulaya zilianza kumfukuzia lakini ni wababe wa Bundesliga, Bayern Munich, ndio walioinasa saini yake.

Manchester City, Manchester United zilimtaka Mreno huyo lakini mwishowe alitua Bayern walimchukua kwa Pauni milioni 27.5.

Kiungo huyo alikuwa ameshachezea mechi 30 akiwa na klabu yake ya utotoni ya Benfica na Bayern walivutiwa zaidi na uwezo aliounyesha pindi timu zilipokutana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Sanches aliyeibuliwa na ‘academy’ ya Benfica, aliweza kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Bayern, ambapo alianza katika mechi nne kati ya sita za mwanzo wa ligi.

Baada ya hapo, upepo ulibadilika na kumshuhudia Sanches akihaha kurejea kwenye ‘first eleven’ ya kocha Carlo Ancelotti.

Ancelotti alisisitiza kuwa kinda huyo angepata nafasi lakini mpaka kumalizika kwa msimu, alikuwa ameanza mara tisa pekee katika michuano mbalimbali.

Tangu Desemba mwaka jana, Sanches anayetajwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 30 kwa sasa, ameingia mara mbili pekee kwenye kikosi cha kwanza cha Bavarians.

Kwa takwimu hizo, haikushangaza sana kuona akiachwa kwenye kikosi cha Ureno kilichokwenda Urusi kucheza Kombe la Mabara.

“Nafikiri sababu ya yeye kuhaha ni ukweli kwamba bado ni kijana,” alisema Torben Hoffman, beki wa zamani wa Bayer Leverkusen na 1860 Munich.

“Alikuwa na tatizo la lugha na ilikuwa ngumu kuelewana na timu. Pia kuna ushindani mkubwa wa namba Bayern.”

Pale Bayern, alitakiwa kupigania nafasi mbele ya Xabi Alonso, Arturo Vidal na Thiago Alcantara ambao tayari walishaweka mizizi Allianz Arena.

“Hakupata naafsi kubwa kikosini mwaka jana na sitazamii akiipata msimu ujao.

“Xabi Alonso ameshastaafu lakini msimu uliopita Ancelotti hakuonekana kuwapa nafasi kubwa wachezaji chipukizi.

Pia, Hoffman alitilia shaka uwezekano wa Sanches kupata nafasi kikosini hasa baada ya ujio wa mastaa Corentin Tolisso na Sebastian Rudy.

“Ni huzuni kubwa kwa mashabiki wa soka Ureno kusikia Bayern wametumia Euro milioni 40 kumchukua Tolisso,” alisema nyota huyo wa zamani wa Ujerumani.

“Walifikiri (Sanches) angepata nafasi zaidi, lakini itakuwa ngumu tena. Labda kama atapata nafasi akiwa na U-21, anaweza kurejesha hali ya kujiamini na kuishwishi klabu kama Man United kumfuata tena.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.