TUHITIMISHE

MJADALA WA MIMBA KWA TAHADHARI KUBWA

Rai - - MBELE - NA THADEI OLE MUSHI

Najua sote tunajua nguvu ya kauli ya Rais, popote duniani Rais ndiye msemaji wa mwisho kwenye kila jambo, Rais ndiye msimamo wetu kwenye mambo yanayohusu diplomasia yetu ya nje yaani Rais ndiye kila kitu. Ndio maana kuna kitu kinaitwa kwenye Sheria Decree, hii ni kauli ya mtu mwenye mamlaka akishaitamka waliopo chini yake wanaitekeleza kama sheria. Kwa maana rahisi kabisa Decree ni sheria ambayo inatokana na tamko la kiongozi, kwa maana hiyo msimamo wa rais kuhusu wajawazito mashuleni tayari ni sheria .... hata kama ilikuwa imelegezwa sasa itakazwa kweli kweli.

KWA SASA TUNAWEZA KUFANYA NINI?

Mbinu tunayotumia kumuomba nayo Rais alegeze msimamo wake sidhani kama anaweza kuikubali kwa asilimia 100. Nakubaliana na wanaotoa hoja na baadhi ya tafiti kuwa mazingira, umbali toka shule, ubakaji, na tamaduni zetu zinachangia wanafunzi wa kike kupata mimba. Nakubaliana nao kabisa kuwa si wote wanazipata kwa kupenda na nakubalina pia na kauli ya Rais wa awamu ya nne na hata hii ya Rais wa awamu ya Tano kuwa wengine wanazipata kwa uzembe.

Rais anataka kuzikomesha mimba hizi, anataka wanafunzi wajitambue wajue wanachokifanya, kuna ambao wanataka kuwatetea wale ambao wameshaingia mtegoni lakini njia wanazozitumia watafanya ‘uncle Magu’ akaze zaidi. Ni vizuri wakatulia wakajipanga ndipo wakatafuta mbinu ya kumuomba alegeze masharti. Yeye ni binadamu tena mcha Mungu kweli kweli hawezi kuacha kuwasikiliza lakini nasisitiza njia mtakayopitia ndio itakayoamuka kukubali kwake au kukataa maombi yenu.

ELIMU NI MUHIMU KWA WOTE

Kwa maana rahisi kabisa elimu ni nyenzo ya kumfanya mtu yeyote yule kupambana na mazingira yake katika kujipatia kipato na kujikimu.

Tanzania imeingia mikataba mingi ya kimataifa ambayo inazungumzia haki ya kila raia kuapata elimu na umuhimu wa elimu hiyo. Hapa nitatoa mifano michache:Mkataba wa kimataifa kuhusu Haki za binadamu (Human Rights), 10/12/1948 nchi 58 zilisaini kuhusu tamko la haki za binadamu. Tanzania nayo ni miongoni mwa nchi zilizosaini tamko hili baadaye. Kwenye tamko hili lenye vipengele 30 kipengele cha ya 26 inazungumzia kuhusu elimu kama haki ya msingi ambayo kila nchi mwanachama anapaswa kuipata.

Kwenye kipengele hicho ambacho kimegawanywa kwenye sehemu tatu kinazungumzia kuwa elimu ya msingi inapaswa kutolewa bure na ile ya vyuo vya elimu ya juu iwe Accessible yaani kila mtu mwenye kuihitaji aipate kwa vigezo vinavyotakiwa. Haya yanazungumzwa kwenye sehemu ya kwanza ila sehemu ya pili inazungumzia malengo ya elimu yenyewe. Ambapo tamko lile linataka elimu itakayotolewa iwe ni elimu inayoweza kumjenga mtu aweze kuhifadhi na kutunza haki za binadamu wengine, imjenge utu wake awe raia mwema, imjenge mtu awe mvumilivu, mwelewa na aweze kushirikiana na watu wengine ambao wapo tofauti kidini na hata kirangi. Sehemu ya mwisho inampa uhuru mzazi kuchagua aina ya elimu ambayo mwanawe ataipata.

Ukisoma tamko hili utaona kuwa Tanzania kama nchi ilisoma na kuona manufaa makubwayaRaiawakekupata elimu. Ukimnyima mtu elimu umemnyima kitu kikubwa sana... ni sawa na kumtoa kwenye ulimwengu huu na kumfungia mahali kwenye giza. Naamini viongozi wetu hawakushinikizwa kusaini tamko hili walilisaini baada ya kujiridhisha kuwa lina manufaa kwa raia wake.

Hawa mabinti inatupasa tuwadhibiti kwa hali na mali kuhakikisha wanaifaidi haki yao hii ya msingi na kuwafungulia njia. Elimu ni kama tochi kwao penye giza waitumie kumulika na kusonga mbele.

Tamko la pili ambalo nalo tumelisaini ni lile la International Covenant on economic, social and cultural Rights.Tamko hili lilisainiwa tarehe 16/12/1966. Tamko hili likitolewa kupima utekelezaji wa tamko lililotangulia la UN. Tamko hili lilianza kutumika tarehe 31/1/1979 kwenye tamko lile lilikuwa na vipengele 30 ila kipengele cha 14 na 13 ilihusu elimu. Tanzania nayo imesaini tamko hili.

Kwenye tamko hili hakuna kilichobadilishwa toka tamko la mwanzo la UN. Malengo, na manufaa ya elimu yalikuwa yake yale. Na kwa utashi wa viongozi wetu walilisoma na kukubaliana na tamko hilo ndio maana walilisaini kwa niaba ya watanzania.

Je, hakuna haja ya kutafuta vipimo vya kuwahukumu mabinti hawa? Kuna wengine si kwa kupenda kwao naamini kama wanaharakati watapitia njia iliyosahihi naamini Rais atawasikiliza. Nasema watawasikiliza kwa kuwa viongozi wetu wanajua umuhimu wa haya matamko na umuhimu wa elimu kwa ujumla.

Tamko la tatu ambalo Tanzania imeingia ni lile la UNESCO Convention against Discrimination in Education. Tamko hili lilitolewa tarehe 14/12/1960 likaanza kutumika 1962.

Kwenye tamko lile linasema kwenye elimu kusiwepo na ubaguzi wa aina yoyote ile iwe ni kwa rangi, jinsia, lugha, itikadi za siasa, utofauti wa kiuchumi, nk. Yaani elimu iwe ni kwa watu wote bila kujali makandokando yao.

Kwa hawa watakaopata mimba tukiwafukuza moja kwa moja hatuoni kuwa tutakuwa tunakiuka tamko hili tulilosaini wenyewe? Nadhani kama njia sahihi zitafutwa bado kutakuwa na uwanja wa majadiliano namna bora ya kulimaliza tatizo hili. Kuchukua ilan ya CCM na kumtumia Rais haitoshi kumshawishi kulegeza mtizamo wake. TumesainI pia hili kwa kuwa tunaamini kuwa Elimu ni mwanga kwa kila Raia.

Tamko la nne ambalo nalo tumelisaini kama taifa ni lile la Convetion on the elimination

all forms of descrimination ainst women. Hili ni tamko mwaka 1979 ambalo lilianza tumika 1981. Kwenye article

kumi kwenye tamko lile na kipengele kinachohusu mu. Kwenye kipengele cho yamewekwa masharti wa kwa jinsi mwanamume avyochukuliwa katika pata elimu basi na kwa asichana pia kufanyike hivyo vyo. Mvulana anayempa sichana mimba na huyo vulana ni mwanafunzi huwa namfanya nin? Sijui ila tamko li pia tumelisaini kwa kuwa tuliamini kuwa mwanamke anapitia mazingira mengi katika kupata elimu yake. Ndio maana nasisitiza umuhimu wa kutafuta njia sahihi ya kumkuta Uncle.

Tamko la Tano ambalo tumesaini ni lile la UN kuhusu haki za watoto 1989. Ambalo linamtambua mtu ambaye yupo chini ya miaka 18 kama mtoto.

Kipengele cha 28 na 29 kwenye Tamko lile linahusu elimu. Linazungumzia kuwa elimu ya msingi iwe ya lazima na itolewe bure. Wameelezea sana umuhimu wa elimu kwa mtoto. Na viongozi wetu walisoma na kukubalina na tamko hilo wakasaini badala yetu.

Kinachonikasirisha ni njia inayotumika katika kupanua huu mjadala. Elimu haina Itikadi mnapotaka kuijadili kwa kutumia itikadi mtaiona nguvu aliyonayo Uncle...

Tamko la sita ni lile la world conference on Education la mwaka 1990. Hili nalo tumesain ni tamko lilihusu kuondoa ujinga kwa watu wazima.

Mule ndani yamezungumzwa mengi na viongozi wetu walisain badala yetu kwa kuwa waliona umuhimu wa Elimu.

Tamko la saba ni lile la Dakar Declaration la mwaka 2000. Tamko hili tumekisaini na lilikuwa na lengo la kuufikia 2015 watoto wote wake kwa waume wawe na uwezo wa kumaliza elimu ya msingi.

Tumesaini lakini hapa kwetu tunataka wale wa kiume tu wawe ndio wanaomaliza wote. Tunaweza kupendekeza sheria kwa wanaowapa mimba hawa watoto ili tukalitekeleza tamko hili kwa vitendo.

Tamko la nane ni lile la Jakarta declaration hili lilikuwa la mwaka 2005. Kwenye tamko hili walitaka nchi zote zilizorudhia na kusaini kutamka kwenye kwenye katiba zao kuwa elimu ni haki ya msingi kwa kila raia.

Tanzania ilisaini na ikaingizwa kwenye katiba yetu. Changamoto tuliyonayo sasa ni hili kundi tunalotaka kuliacha njiani.

Tamko la tisa ni lile la African Charter lililofanyika Nairobi Kenya 1986. Kwenye ibara ya 17 ya tamko lile lilisema kila Raia ana haki ya kupatiwa elimu. Viongozi wetu wakalisoma na posho za kuhudhuria wakachukua na wakaona ni sahihi wakasaini.

Je, tumeweka mazingira gani kuhakikisha wananchi wetu wote wanapata elimu?? Ni mchakato wa majadiliano na sio itikadi hapa kutumika.

Hapa nimetoa mifano michache tu ya kimataifa humu ndani tuna matamko pia yanayoonyesha umuhimu wa elimu.

Hatuoni kuwa Rais katupa fursa ya kujadili suala hili na kutoa suluhu ya kudumu? Tukumbuke tunapozungumzia elimu tunazungumzia uhai wa watu na uhai wa Taifa.

MKATABA wa kimataifa kuhusu Haki za binadamu (Human Rights), 10/12/1948 nchi 58 zilisaini kuhusu tamko la haki za binadamu. Tanzania nayo ni miongoni mwa nchi zilizosaini tamko hili baadaye. Kwenye tamko hili lenye vipengele 30 kipengele cha ya 26 inazungumzia kuhusu elimu kama haki ya msingi ambayo kila nchi mwanachama anapaswa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.