Hili la Diamond, Kiba zaidi ya Messi, Ronaldo

Rai - - MBELE - NA AYOUB HINJO

‘HAWAAMINI kwenye kuunda Diamond au Kiba wawili, wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili’. Hiyo ni baadhi ya mistari aliyoimba Fareed Kubanda ‘Fid Q’ katika wimbo wake uitwao ‘Sumu’. Ni mistari ambayo ina maana kubwa sana kwa wadau wa muziki hapa nchini.

HAWAAMINI kwenye kuunda Diamond au Kiba wawili, wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili’. Hiyo ni baadhi ya

mistari aliyoimba Fareed Kubanda ‘Fid Q’ katika wimbo wake uitwao ‘Sumu’.

Ni mistari ambayo ina maana kubwa sana kwa wadau wa muziki hapa nchini. Maana kubwa ya mistari hiyo ni kuwa wadau wengi wapo nyuma ya Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba lakini kila mmoja amekuwa akimuunga mkono msanii wake miongoni mwa hao wawili.

Fid Q alielezea hilo kwa upana zaidi, aliendelea kusema wakati yeye na msanii mwenzake Witness wameteuliwa kwenye Tuzo za Afrika, walishangaa kuona wasanii wa kutoka Nigeria wakifurahi pamoja tofauti na Watanzania ambao walionekana kukaa kwa makundi.

Ushindani huu ambao upo kwenye tasnia ya muziki hasa ile ya kizazi kipya au Bongo fleva upo pia hata katika soka. Messi mshindi wa Ballon d’Or mara tano dhidi ya Ronaldo aliyeinyakua mara nne. Upinzani wao upo katika kila sehemu ambayo wachezaji hao wapo.

Ukitazama katika kikosi cha Barcelona, Messi hutazamwa kama nyota wa timu hata katika kikosi cha Real Madrid, Ronaldo naye hutazamwa kama shujaa wa timu hiyo vilevile.

Ushindani wao umevuka mipaka hadi katika matangazo yao ya kibiashara. Kila mchezaji ana matangazo yake ya biashara na kila mchezaji ana mvuto wake katika matangazo na biashara zake.

Tofauti na wengi wanavyowatafsiri, wao wenyewe wanasema hawana uadui kabisa lakini mashabiki wao wamekuwa wakiwapambanisha kutokana na ubora ambao wachezaji hao wako nao.

“Napenda kumuangalia Messi akiwa uwanjani. Anavutia kumtazama, hasa ule mguu wake wa kushoto akiwa na mpira. Ni mchezaji hatari sana. Kila napokuwa naye huwa tuna mahusiano mazuri, sio adui yangu”. alikaririwa Ronaldo akimzungumzia Messi. “Ni mchezaji bora, amekwisha thibitisha hilo. Sina kingine cha kueleza juu ya ubora wake alionao. Ronaldo ni mtu mzuri nje ya uwanja mara kadhaa tumekuwa tukizungumza tunapokutana”. Alisema Messi akimzungumzia Ronaldo.

Tofauti ipo kubwa sana kati ya mastaa hao na wasanii wetu wawili ambao wameugawa muziki wa Bongo fleva hapa nchini na kuwa katika pande mbili tofauti.

Chuki zimetawala, visasi vimetawala na ubaya wa mambo mengi yametawala zaidi. Hakuna anayemzungumzia mwenzake kwa uzuri, kila mmoja anajiona bora zaidi.

Majigambo ni kitu cha kawaida sehemu yoyote ambayo kuna ushindani. Lakini heshima ni kitu kikubwa sana kinachoweza kukupa thamani mbele ya mpinzani wako.

Hakuna jinsi, Diamond na Kiba hawajiheshimu, angalia walivyoacha chuki kati mioyo ya mashabiki wao.

Ushindani ni kitu kizuri sana, mahali popote ushindani lazima uwepo. Heshima lazima itawale ili thamani yako ikue zaidi na zaidi.

Wiki chache zilizopita, Fid Q alimshirikisha Diamond kwenye wimbo wake wa ‘Fresh’ ambao aliufanyia marejeo tena baada ya kutoa ‘ Fresh’ halisi.

Mistari aliyoimba Diamond, haikuonyesha heshima kwa Kiba na hata mashabiki Diamond walibaki wakishangaa, ya nini yote hayo? Kwa nini asingeimba muziki wake ambao ungemuweka katika kilele cha juu zaidi?

Hakuna jinsi ila wasanii hao wawili wamewakosea sana Watanzania, licha ya mafanikio yao kuwa makubwa katika muziki bado hawajautendea haki wakiwemo mashabiki wa muziki hapa nchini.

Diamond anaonekana kuwa na mafanikio zaidi ya Kiba kwa sababu ni msanii anayeweza kutumia fursa pindi anapoipata. Hivi karibuni amezindua karanga zake, pamoja na ‘perfume’. Vyovyote vile iwe ni zake au za mtu lakini likatumika jina lake bado ni sehemu ya mafanikio tu kwake.

Hayo ndio maendeleo ambayo watu wanataka kuyaona, acha mafanikio yake kimuziki ambayo yamemfanya ajulikane karibu kila kona ya Afrika na sasa anavuka bara hilo.

Kiba hana mafanikio sana kimuziki lakini ni msanii anayependwa tu. Alitangulia kimuziki kabla ya Diamond. Tungo zake katika nyimbo zake zimekuwa na mafundisho kwa jamii.

Pia ni moja ya msanii ambaye alifanikiwa kufanya kolabo na mwanamuziki nguli duniani kutoka Marekani, Robert Kelly ‘R Kelly’. Kwa wakati ule alikuwa staa lakini alishindwa kutumia fursa ile kupenya kimataifa zaidi na badala yake akazimika kabla ya kuzinduka na sasa anapambana ili kutambulika zaidi kimataifa.

Wote wawili wanapaswa kuheshimiana, angalia jinsi nchi ilivyopasuka katikati Wote tunapenda maendeleo lakini si haya ya malumbano ambayo yanaendelea hata Messi na Ronaldo lakini wanaheshimiana.

Diamond Kiba

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.