Tusifanye dhihaka kuhusu ‘bomu’ la ajira

Rai - - MAONI/KATUNI -

Jean-Jacques Rousseau, Mfaransa mtunzi vitabu vya riwaya wa Karne ya 17, vitabu ambavyo vilikuja kusukuma ‘Mapinduzi ya Ufaransa” (French Revolution) aliandika: “Mara tu baada ya shughuli za utumishi wa umma zitaacha kuwa shughuli kuu za raia, basi utawala hauko mbali

Jean-Jacques Rousseau, Mfaransa mtunzi vitabu vya riwaya wa Karne ya 17, vitabu ambavyo vilikuja kusukuma ‘Mapinduzi ya Ufaransa” (French Revolution) aliandika: “Mara tu baada ya shughuli za utumishi wa umma zitaacha kuwa shughuli kuu za raia, basi utawala hauko mbali kuyumba.”

Lakini mtazamo huo ni wa medani nyingine kabisa ya kisiasa na kijamii, uliotokea katika Bara jingine na karne tatu zilizopita. Aidha sisemi sasa hivi hapa Tanzania tupo kwenye hali hiyo au hata kama ni suala la kufirika.

Msamiati huu “ukweli” katika hali ya kawaida – polepole umekuwa ukijitoa katika jukumu lake la kiuchumi na kijamii kwa wananchi na kuachana kuwa kama mdau muhimu katika maendeleo yao. Wadadisi wa mambo wanaona hali hii ni hasi kwa amani na utulivu tuliokuwa nao kwa muda mrefu.

Na ni muhimu kwa Rais John Magufuli kulitambua hili. Bila shaka anatambua kwamba katika uchaguzi uliopita uliomuingiza madarakani, miongoni mwa mamilioni ya wapigakura waliokuwa wanamuunga mkono mgombea wa upinzani walikuwa ni vijana – wengi wao wakiwa wale wasiokuwa na ajira za kuaminika. Hivyo Magufuli alikuwa akionekana katika jitihada ngumu ya kuwavuta upande wake.

Sasa baada ya kuingia madarakani ingefaa awafikirie vijana hawa – pamoja na kuazima ukurasa kutoka kwa baba wa Taifa Mawlimu Julius Nyerere. Kuanzisha kwa dhati kwa ajira ni moja ya majukumu ya kila awamu za utawala zilizopita walizokuwa wakijaribu kukwepa – ukiacha ule utawala wa Nyerere, bila kujali ile ilani ya siku zote kwamba ukosefu wa jira ni bomu linalosubiriwa kulipuka.

Hebu fikiria: Watawala walikuwa wanadiriki hata kubadilisha tafsiri ya masuala fulani ili kufunika kushindwa kwao – au sahihi zaidi kujaribu kuendana na zile ‘sukuma twende’ zao. Tanzania huenda ni nchi pekee duniani ambako ‘shughuli za wamachinga’ – shughuli zinazofanywa na malaki ya watu ambao hawakujaliwa kupata elimu bora kutokana makosa yasiyo yao – ni sera ya serikali.

Siyatungi haya. Mwaka 2008, aliyekuwa waziri wa kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana, Prof Juma Kapuya alisimama Bungeni, Dodoma na kutangaza kwamba serikali ilikuwa imepitiliza lengo lake la kutengeneza ajira kwa zaidi ya asilimia 27 – ilikuwa imetengeneza ajira milioni moja. Alisema serikali ilitengeneza ajira 1,271,923 hadi kufikia Desemba 2007, miaka miwili kabla ya muda uliojiwekea wa mwaka 2010.

Akifafanua ‘upikaji’ huu Prof Kapuya alisema ajira 1,185,387 zilitengenezwa katika sekta binafsi wakati serikali ilitengeneza ajira rasmi 85,571 na ajira 965 katika sekta ya umma.

Kwa kuangalia haraka haraka takwimu hizi zilizotolewa kwa tarakimu kamilifu kwa ajili ya kuaminika kwa wananchi, mtu angeweza kusema zilikuwa zinaonyeshajinsiserikaliilivyokuwa inawajibika kwa wapigakura hasa katika changamoto nzima ya utengenezaji wa ajira.

Lakini takwimu zina kawaida za kudanganya hasa zikiangaliwa kwa mbali. Kwa karibu ni kwamba ajira hizo milioni moja ‘zilizotengenezwa’ katikia sekta binafsi ni “biashara za ‘wamachinga” wakiwa na liseni zao za “nguvukazi.”

Wachache wengine wanaojumuishwa hapa ni vibarua katika sehemu za ujenzi na vibarua wengine wanaopata ujira siku kwa siku katika maeneo ya sokoni, sekta ya usafiri na sehemu nyingine ndogo ndogo za kiuchumi ambazo hazina kinga za kazi au bima.

Kujigamba kwa Prof Kapuya kulimuinua Dr wilibrod Slaa, Mbunge wa zamani wa Chadema na katibu Mkuu wa chama hicho kumtaka athibitishe takwimu zake kwa kuonyesha mikataba ya kazi, jinzi ajira hizo zilivyotangazwa na kadhalika.

Hii yote ilionyesha jinsi watendaji wa serikali walipofikia – katika namna ya kuelezea changamoto halisi zinazoikabili jamii. Iwapo mjukuu wangu atakosa nafasi katika kidato cha Tano na akaanza kuuza mandazi, basi hiyo ni ajira iliyotengenezwa na serikali na waziri atakuwa tayari kujigamba nayo Bungeni.

Naamini kabisa tafsiri yetu ya “ajira” katika mantiki ya ki-uchumi iko sawasawa na ile ya Marekani au nchi nyingine, au jinsi ilivyokuwa hapa hapa Tanzania miongo kadha iliopita.

Lakini sasa hivi ni kazi kubwa hata kwa utawala wa Trump kutengeneza ajira 200,000, inakuwaje Tanzania kutengeneza ajira milioni moja kwa urahisi tu?

Hii ina maana kwamba kiuhalisia hakuna ongezeko la ajira, labda ni mfano wake tu. Pia inamaananisha kwamba hakuna tafsiri halisi ya misamiati ya ajira, vijana, wazururaji, kazi na wawekezaji.

Kwani hua tunaona watu wa nguvu na heshima zao wakiuza maji ya chupa barabarani au kwenye vituo vya mabasi, wauza karanga na wauzaji wa vitu vya plastiki – kazi ambazo zote hizi tunasema ni ajira.

Na kuna hili jipya ambalo kwa hakika huwafanya vijana wetu kuwa kama machizi vile – kukusanya chupa tupu za plastiki barabarani na kwenye majalala. Hakika Mwalimu Nyerere atajigeuza kaburini!

Kweli anaweza au atalazimka kufanya hivyo. Sera ya serikali yake kuhusu ajira kwa vijana haikuwa kama hii – serikali kujiondoa kabisa katika jukumu hilo na kuwaachia vijana watafute namna yao ya kujikimu kimaisha na hapo hapo serikali hiyo kujigamba kwa sauti kubwa kwamba imewatengenezea ajira.

Akitilia maanani suala la ukosefu wa ajira, Nyerere, kwa hatua za kimakusudi aliunda mashirika na viwanda vya umma ambavyo vilitoa ajira kwa maelfu ya vijana waliokuwa wakimaliza shule kila mwaka.

Mashirika ya umma aliyoyaunda ni pamoja na kiwanda cha kutengeneza viatu (Tanzania Shoe Company -Bora Shoes), kiwanda cha zana za kilimo (UFI), kiwanda cha magurudumu ya magari (General Tyre), (viwanda vya nguo (kama vile Urafiki, Mbeyatex, Mwatex, Mutex, Kiltex nk), KAMATA, Tanganyika Packers, kampuni za biashara za Mikoa (RTCs) na nyingine nyingi sana.

Baada ya uongozi wa Nyerere mameneja wa viwanda na mashirika hayo walishindwa kuyaendesha, kutokana na uzembe, ufujaji na wizi wa fedha na mali zake. Awamu zilizofuatia ziliamua kuyauza mashirika hayo kwa bei ya chee kabisa na hivyo mara moja kuwafanya maelfu ya vijana kuingia mitaani bila ya ajira. Walioyanunua walishindwa kuviendeleza na eti sasa serikali inataka maelezo kwa nini.

Kitu kizuri pekee kilichotokana na kufa kwa mashirika hayo ya umma ni ‘kuendelezwa’ kwa eneo la kifahari la Mikocheni jijini Dar es salaam. Hakuna haja ya kuwaza fedha hizo zilitoka wapi.

Kiwanda cha magurudumu ya magari General Tyre kilikuwa kinatoa ajira nyingi kwa vijana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.