Mikataba kuwa ya siri ni stahiki, ukomavu

Rai - - MAKALA - NA SHERMARX NGAHEMERA

Siri ni faragha, umahiri, aminifu, vumilivu, yenye kaba na heshimika na iko ulimwenguni kote, na kwa watu wote wazima; kwani ni mtoto tu ambaye hana siri na haaminiki ila kwa masuala yake mwenyewe ndio ushahidi wake unaweza kuchukuliwa.

Maisha bila siri ni maisha ya kitoto kwa hiyo ni mnafiki yule ambaye anataka mambo yote hadharani kwani ni kuingilia ubiniadamu wa mtu na utunzaji wa siri zake.

Ni kuingilia haki zake za kibinadamu kwa kutaka na kudai kumchujua mtu na siri zake.

Kimsingi hakuna maisha bila siri kwani siri ni nguvu ya matendo yetu kwani inapokosekana siri maisha huwa magumu na ya kukatisha tamaa.

Hivyo basi siri ziko za aina mbili za asili na za kupanga. Siri ya asili ni kuwa hatuna uwezo wa kujua yatakayotokea kesho ila kwa kusubiri kesho ifike na tuone matukio yake na sio kabla yake. Mungu tu ndiye ajuaye na hiyo ndio siri kubwa ya maisha.

Lakini tunaweza kupanga mambo ya kesho lakini uhakika wake utatokana na kesho yenyewe na hiyo ndio inayofanya watu wapange maisha yao ya baadaye bila shida lakini anayejua kwa sisi tunaoamini ni Mungu pekee. Kwa msingi huo siri ya asili hutupa nguvu ya matendo yetu yote. Tukiikosa huwa tunanyong’onyea na kukwama.

Ni Mungu anayejua mambo ya usoni na kutokana na hali hiyo ya asili inafanya maisha yaende mbele kwani kama watu wangejua nini kitatokea kesho wasingefanya kazi au kutafuta riziki kwani wangejua matokeo ya juhudi zao hizi kabla na kukata tamaa.

Swali kubwa ni kuwa Siri ni nini? Kwa nini watu siku hizi wanataka sana uwazi kwa watu wengine wakati wenyewe wakijikita kwenye siri?

Siri ni nguvu na umahiri wa kila kitu kwani ndani yake iko faida ya hali na mali. Bila siri hakuna biashara ya maana wala taaluma tarajali kwani ni siri ndio zinaendesha maisha ya mtu binafsi, kikundi, jamii na nchi kwa ujumla bila hivyo ni vurugu tupu zinazotokana na kuoneana wivu na maya. Kwani inasemekana huwezi kuwajibika kikamilifu kama mambo yote yako wazi na hivyo kunahitajika siri ili mambo yaende kwa umurua na hivyo siri ni kitu muhali na ghali.

Katika maisha ili mambo yaende lazima kuwa na watu wanaojua na wengine wasijue kama kwa asili au kwa kitaaluma na kikazi. Ukijua mlolongo mzima wa bei huwezi ukanunua kwa mtu wa kati kwani yeye ni ghali.

Wafanyabiashra watapigana kulinda nafasi ya kujua bei ya chini ya wanakochukua mali na kuwauzia wengine kwa beijuu na hiyo ndio faida yenyewe. Bei kwao ni siri kubwa ili kulinda faida yake. Vivyo iko kwa wataaluma na wagenzi ili kuweza kupata siri hiyo inabidi ulipie yaani ununue.

Ukiumwa unaenda kumwona daktari au mganga ambaye yeye atatumia taaluma yake kutegua ugonjwa kwa kutumia vipimo vya maabara au uzoefu na ukishafanya malipo uaambiwa nini kilikuwa kinakusumbua yaani siri hutoka baada ya kuanza kupata faida kwa pande zote zinazohusika vinginevyo ugonjwa utaendelea kuwepo.

Duniani miundo yake imetengenezwa ili kutengeneza na kutunza siri kwani bila hivyo hakutakuweko nchi tajiri na masikini wala watu masikini na matajiri. Inasemekana utajiri au umasikini wa mtu unatokana na kwa kiasi kikubwa kiwango chake cha kutunza siri. Kama huna utunzaji siri usitegemee unaweza kuendelea kwenye fani yoyote ila ya umbeya na ghilba.

Kutokana na hali hiyo yote uyaonayo sio ndivyo yalivyo kwa wote ila yametengenezwa kuwaweka sawa watu wa aina fulani tu na wengine wanaona tofauti na hao ndio wanaofaidika na mtindo huo.

Mifano iko mingi yaani kama siri sirini, mpenda chongo huona kengeza na mtaka cha uvunguni sharti uiname au uinue kitanda, yaani lazima uvunje siri zilizofichika chini ya kitanda.

Orodha ni ndefu ila cha kukumbuka ni kuwa ili kuwepo na amani lazima kuweko na siri kwani bila hivyo maisha hayakaliki na hayakubaliki. Ni siri pekee ndio huwa azima ya matendo na mwenendo wetu.

Tuna familia kwa sababu tuna mambo mengi ya wenzi wetu hatuyafahamu kwani tukiyafahamu yote hakuna salam ya mapenzi wala heshima inabakia katika mahusiano hayo.

Sio kwamba ni kuficha maovu kwa msemo kuwa ukimchunguza sana kuku au bata huwezi kumla au unapomchunguza mkeo uwe na ujasiri wa kumpa talaka vinginevyo ni kero tupu. Acha!

Siri sirini Hivi basi hata katika mahusiano yetu ya karibu sana ya mume na mke bado tunaendelea kuwa na siri zetu kama siri za ukoo. Huwezi kama una binti kikojozi ukaanza kumtangaza kwa majirani kuwa ana matatizo hayo kwani atakosa mume na hivyo kuifanya siri hiyo kuwa ya familia husika na vivyo kama unaukichaa kwenye familia yenu huwa haitangazwi kwani hiyo ni changamoto ya familia pekee.

Mambo mengi hufanyika na kufahamika kwa wahusika tu na sio kwa kila mtu kwani hayo ndio maisha yenyewe yamejengeka na kukuzwa katika usiri.

Familia au kabila na sasa nchi. Kila sekta ina siri zake na hata katika jeshi moja watu kikosi cha ndege wana siri ambazo watu wa majini au nchi kavu hawajui. Ndio. Kwani nchi isiyo na siri ni ya wendawazimu kwani hata kuvaa nguo ni kuficha siri ya maungo yetu ambayo huwa hayapendezi mbele ya umma ila kwa wahusika wawili tena wakiwa chumbani wakati milango na madirisha yamefungwa au kusindikwa.

Kutokana na hayo inakuja dhana kuwa waume huweza kudanganya wake zao lakini sio vimada vyao. Kimsingi kila mtu umwonaye ana kitu angalau kimoja kuwa ndio siri yake na haelezwi mtu kwani kinaweza kumwangusha katika maisha; yaani ana kamfupa kadogo anakokafungia kwenye kabati (Everyone has at least one skeleton they wanted to keep safely locked up in the cupboard).

Mafanikio yaliyopitiliza huleta ukorofi na majivuno ambayo kimsingi hayaendani na usiri na hapo ndipo watu wanaanguka katika mambo yao kwa kufichua siri zao kama yalivyotokea kwenye Biblia kwa Samson na Deliilah. Alipofichua siri na kusema kuwa nguvu zake ziko kwenye nywele zake na hapo ndipo nguvu zikamwishia na kupotea. Ni muhimu kujua kuwa nguvu yako hutokana na maadui zako kutokujua ulivyo kwani wakijua wameshashinda kwa nusu bila hata ya kuanza kupigana.

Inatuashiria kuwa siri ni kitu muhimu wakati wote yaaani wakati wa kuweka mikakati, utekelezaji wake na wakati wa kuhitimisha kwani lolote linaweza kutokea na kubadilisha hali. Wakati mwingine kile cha mwisho kwa kutokea ndio chanzo cha masuala yote kama ugonjwa kwani huja mwisho baada ya mwili kushindwa kumudu mashamabulizi ya viini vya magonjwa na hivyo huwezi

na mila na desturi za binadamu

hao wanaounda Serikali na ina hisia zao katika masuala ya usalama na mwenendo wake na hapo ndipo suala la mahusiano na maelewano kati ya idara mbalimbali zinazofanya Serikali.

Madaraja mbalimbali ya utumishi huundwa katika mfumo ambao kiini chake ni usiri ili kuweza kudhibiti taarifa na habari ili mambo yaende katika mkondo na mwenendo unaokubalika na wengi au wote wanaofanya muundo wa Serikali.

Hivi basi Serikali huendeshwa kwa siri na siri hizo huvunjwa na wenyewe kadiri mtu anavyopanda cheo au kupata madaraka fulani ambayo yanamwezesha kujua au kustahili kupata taarifa husika, lakini huko akitahadharishwa juu ya unyeti wake kwa kugongewa mihuri kuwa ni ya siri au kwa macho yake tu. Kuna ngazi saba za siri ikiishia na ile kwa macho yako tu ambapo mhusika haruhusiwi kuwa na nakala yake bali husoma na kuondoka.

Kwani hilo liko wazi kuwa Serikali ni siri na siri ni Serikali. Ukitaka kujua kuwa uko katika ngazi gani serikalini, pale ambapo utakapoanza kuruhusiwa kusoma mambo yaliyoandikwa SIRI kuachia barua yako ya ajira.

Watu wakishinda kura hupewa madaraka na kabla ya kukabidhiwa mikoba ya kutawala, hula kiapo cha kutunza siri za Serikali au Baraza la Mawaziri na hivyo kuwemo katika kundi lile la wachache, wateule katika nchi wanaojua kinachoendelea katika Serikali na hata jamii kwa kina.

Chama tawala kina siri zake za kutawala na kushinda chaguzi wakati wale waliopo kwenye upinzani wana siri zao za kutaka kuangusha utawala uliopo madarakani kidemokrasia, ni kwa kutumia kura za uchaguzi au makosa ya watawala na hivyo kufanya nchi na tawala zetu zifanye kazi ya ziada ili kuendelea kuwepo kwa mafanikio katika nafasi zao.

Kadiri tunavyojijali tunashangaa makosa ya wengine, lakini inabidi tufikirie kwanza makosa na dhambi zetu na hivyo tutakuwa na huruma na uelewa wa makosa ya wengine.

Kadiri mtu anapojishusha hupanda na Mungu kwani mahusiano ya mtu na Mungu ni kitu cha siri kubwa.

Kadiri tunavyokuwa na mahitaji machache ndio tunakaribia utukufu wa Mungu.

Siri za mikataba

Mikataba ni mapatano ya kufanya mambo fulani yanayoingiwa na watu, kampuni, taasisi, vyama au mashirika ili kufanya shughuli zao za kiuchumi na kitamaduni zenye faida kwao. Mikataba hiyo inalenga kulinda masilahi yao na kudhibiti mwenendo wa kila mhusika kwa kuainisha mambo mbalimbali yanayohusika na hivyo kimantiki na kimuundo huchukuliwa kuwa ni siri kubwa ili washindani au watu wenye shughuli kama zao wasijue na kuja kutibua mambo yao ikiwa ni msingi wa ushindani kibiashara.

Hivi basi maneno hulia na machozi husema. Na katika maneno ya kuonesha huzuni kwa ulimi au kwa kalamu ni kuwa: KAMA NINGEJUA…

Kwani siri nyingi huvuja kwa maneno na hivyo kufanikiwa kwako kuweka siri kunatokana na wewe mwenyewe kuwa na uwezo wa kusema mengi, lakini si kitu chochote (speaking much without saying anything) yaani kubwabwaja.

Mikataba ni siri ya kupanga ili kuwashinda wapinzani na hulinda masilahi ya kila mtu kama ilivyoelezwa mwanzo. Hakuna ubaya Serikali kuingia mikataba ya siri kwani mtekelezaji ni yenyewe na si kila mtu ni kikoa kwa Serikali husika.

Ni watu maalumu kwa shughuli maalumu. Ni kusema kweli kuwa jambo lisilokuhusu hutakiwi kulijua hata kama ni la serikali ya kidemokrasia kwani kila kitu kina wenyewe. Tusijidanganye vinginevyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.