Odinga: Uhuru Kenyatta amelewa

Rai - - MBELE - NAIROBI, KENYA

Mgombea Urais wa muungano wa vyama vya upinzani NASA nchini Kenya Raila Odinga amedai kuwa Rais Uhuru Kenyatta alipowatukana Majaji wa Mahakama ya Juu alikuwa amelewa. Akihutubia mkutano juzi katika uwanja wa Nyamaiya, County ya Nyamira, kiongozi huyo wa upinzani alisema Uhuru

Mgombea Urais wa muungano wa vyama vya upinzani NASA nchini Kenya Raila Odinga amedai kuwa Rais Uhuru Kenyatta alipowatukana Majaji wa Mahakama ya Juu alikuwa amelewa.

Akihutubia mkutano juzi katika uwanja wa Nyamaiya, County ya Nyamira, kiongozi huyo wa upinzani alisema Uhuru alikuwa amekunywa pombe kabla ya kufanya ziara katika maeneo kadhaa ya jiji la Nairobi.

Kauli za Uhuru zilifananishwa na makabiliano yake makali na Majaji hao ambao aliwaita “wakora’ – yaani wahuni tu.

Raila ametoa shutuma kali dhidi ya mshindani wake katika kinyanganyiro cha kuwania urais kufuatia kauli zake za kuwatusi Majaji hao ambao Ijumaa iliyopita walitoa hukumu ya kubatilisha ushindi wa Uhuru Kenyatta uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 8, mwaka huu.

Raila aliwaacha wahudhuriaji wakipigwa na mashangao mkubwa baada ya kusema rais Uhuru hakuwa sawasawa wakati akiishambulia Mahakama ya Juu.

Alisema baada tu ya uamuzi wa Mahakama hiyo alikwenda kunywa pombe na kuibuka akiwa na macho mekundu na kuanza kuushambulia Mhimili wa dola.

Katika mkutano huo wa juzi, huku akishangiliwa na wananchi Raila alisema: “Uhuru tunakuonya, acha kabisa kuitukana Mahakama ya Juu.”

Aliendelea kusisitiza msimamo wa NASA kwamba IEBC ya sasa haina uhalali wa kuendesha uchaguzi mpya.

Na katika hatua nyingine akizungumza katika mkutano huo huo Raila Odinga amepinga Oktoba 17 kuwa tarehe ya kufanyika uchaguzi wa marudio na umetaka tarehe isogezwe nyuma hadi mwishoni mwa Oktoba 2017. Aidha Raila amedai kwamba tarehe hiyo imepangwa bila ya kuhusishwa chama chake.

Chama hicho cha upinzani pia kimetishia kutoshiriki uchaguzi huo iwapo IEBC itakuwa bado na Makamishna wale wale walioendesha uchaguzi wa Agosti 8.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.