Mkakati wa SADC kudhibiti ugaidi unahitaji mbinu mpya

Rai - - MAKALA -

yatakayotokea katika nchi hizo.

Mafunzo hayo yaliyodumu kwa takribani mwezi mmoja, yalijulikana kwa jina la Operesheni Matumbawe ambayo iliweza kufanyika katika maeneo ya nchi kavu na majini katika Ukanda wa Bahari ya Hindi.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, anasema mazoezi ya ugaidi na uharamia yaliyofanywa na vikosi vya SADC yatasaidia kuibua mbinu mpya ya upambanaji wa matishio ya uvunjifu wa amani na usalama kwa nchi washirika.

Kutokana na wahusika wa matukio ya ugaidi na uharamia kubadili mbinu za matukio hayo mara kwa mara, hivyo hali hiyo imechangia kutolewa kwa mafunzo hayo ili kuwapa uwezo wanajeshi wa nchi za SADC kupambana na uhalifu huo.

Anasema matukio ya uharamia ama ugaidi hayana mipaka na hivyo ni lazima yakapigwa vita kwa pamoja kwa kushirikiana baina ya nchi washirika wa umoja huo.

Anasema kwa sasa nchi za SADC ni kama bara moja ambalo linashirikiana katika kutunza amani pamoja na kudhibiti na kuzuia vitendo vyovyote vitokanavyo na kuvuruga amani.

“Mazoezi hayo ni sehemu ya uthibitisho wa ushirikiano uliokuwepo baina ya nchi washirika katika kupambana na matishio ya ugaidi na uharamia katika nchi za SADC pale ambapo yanatokea,” anasema Waziri Mwinyi.

Vilevile Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, anasema operesheni hiyo ilikuwa imelenga katika malengo makuu matatu ambayo ni kujenga uzoefu baina ya majeshi na kuweka ushirikiano wa kindugu na ukaribu, kutengeneza mkakati wa kulinda amani kwa pamoja hasa katika kukabiliana na matishio ya ugaidi, uharamia na biashara za madawa ya kulevya na binadamu.

“Operesheni hiyo ililenga katika kuandaa vikosi hivyo kuweza kushiriki katika jeshi la pamoja la Afrika, kwani nchi za SADC majeshi yake huwa yanashiriki katika kanda tano za Afrika.

Aidha, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, anasema kama wanajeshi wameweza kupiga hatua moja mbele kwani vitisho vinavyotokea sasa havina mipaka, hivyo tunahitaji ushirikiano.

Huku akikumbushia namna ambavyo mwaka 2012 matukio ya uharamia yalivyoweza kuleta athari kwa nchi ya Tanzania yalihusisha utekaji wa meli za mizigo ambayo ilikuwa imebeba bidhaa za wafanyabiashara kwa ajili ya kuleta katika soko la Tanzania.

Hivyo hali hiyo iliweza kusababisha matishio ya hali ya uchumi wa nchi, kwani wafanyabiashara walilazimika kutishia kusitisha kuleta bidhaa kutokana na watekaji hao kudai fidia kubwa ili kuachia mizigo hiyo. Na kusababisha majeshi ya kimataifa kuingilia katika kukabiliana na matishio hayo yaliyokuwa yakiukabili ukanda huyo, ambapo kutokana na matukio hayo ndipo majeshi ya nchi za SADC yaliweza kujiimarisha.

“Kama mnakumbuka matishio yaliyoweza katika maeneo ya

Amboni jijini Tanga na Kibiti namna ambavyo yalivyoweza kuleta athari kwa wananchi na mali zao,” anasema Mabeyo.

Matukio ya Amboni majeshi yetu yaliweza kupambana na ugaidi vizuri, hivyo tukaona tuwalete wenzetu nao waweze kushuhudia kama mapango hayo yanaweza kuingilika.

Hivyo ameongeza kuwa kuja kwa Operesheni hiyo ni kuongezeana nguvu ili kukabiliana na matishio ya aina hiyo pamoja na kubadilishana uzoefu wa kimiundombinu pamoja na vifaa vya utaalamu katika kukabiliana na matukio hayo. Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni hiyo, Meja Jenerali Harison Masebo, anasema licha ya vikosi hivyo kufanya kazi iliyokusudiwa pia vimeweza kushiriki katika shughuli za maendeleo zilizoko jirani na eneo hilo la Mlingano.

vizuri kutokea

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.