Mkombozi wa mazingira kapatikana

Rai - - MAKALA - NA VICTOR MAKINDA

UKATAJI miti ovyo ni moja ya chanzo kikuu cha ukame na mabadiliko ya tabia nchi.

Zipo sababu zinazosukuma watu kukata miti, mathalani upasuaji wa mbao, ujenzi na matumizi ya nishati za kupikia.

Katika miaka ya hivi karibuni maeneo mengi nchini yanakabiliwa na ukame, hali hii imesababishwa na ukataji wa miti.

Aidha kilimo cha kuhama hama nacho kinatajwa kama sababu za uharibifu wa mazingira, kwa sababu wakulima hulazimika kuanzisha mashamba mapya kila msimu, hali inayosababisha kukatwa kwa miti.

Wakulima wengi ambao hawajapata mafunzo ya kilimo cha kisasa na matumizi bora ya ardhi wamekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira.

Kwa miaka mingi Tanzania haikuwa na sera ya mkaa badala yake Serikali ilikuwa ikipiga marufuku marufuku na kuweka sheria ngumu kwa wachomaji na wauzaji wa mkaa.

Hata hivyo Serikali haijatoa mbadala wa nini wananchi wafanye ili kuweza kupata nishati mbadala ya kupikia.

Katika kuzingatia hayo ndipo Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu ya Asili Tanzania (TaTEDO) sambamba na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania ( TTCS) walipokuja na wazo la la Sera ya Mkaa Endelevu.

Lengo kubwa likiwa ni kutoa mafunzo kwa jamii ya ya jinsi ya kutumia misitu vizuri ili iwapatie mkaa pasipo kuiharibu.

Mradi huo umejikita kwenye wilaya za Kilosa, Morogoro Vijijini na Mvomero mkoani Morogoro. Mradi huu unaota mafuzo maalumu kwa wananchi ya jinsi ya kuvuna mkaa katika misitu yao ya asili huku wakitoa nafasi kwa miti kumea katika kipindi kifupi cha miaka kadhaa.

’’Kwa mfano msitu wenye Heka 20, hapa tunawaelekeza wananchi kuvuna mkaa katika heka moja kila mwaka na kuacha eneo lilivunwa ili miti iliyokatwa iweze kuchipua sambamba na kuotesha miti mingine. Katika kipindi cha mzunguko wa miaka kumi eneo la hekali iliyotangulia kuvunwa itakuwa tayari imeotesha miti yenye ukubwa wa kuweza kuvunwa kwa ajili ya kuchoma mkaa’’. Anaeleza Mohamed Nyamangalo Afisa Kilimo katika mradi wa Kuleta Mageuzi Sekta ya Mkaa, eneo la Morogoro.

Aidha mradi huo meendelea kuhamasisha kuyatunza mazingira.” Ni vigumu sana wananchi kutokata miti hii ni kutokana na umuhimu wa nishati ya kuni na mkaa katika kupikia. Tulioana hakuna maana ya kuwazuia wananchi kutochoma mkaa na kukata mazao ya misitu kwa ajili ya kuni pasipo kuwaa na njia mbadala ya kupata nishati ya kupikia “Mradi huu wa mkaa endelevu unaweza kuwa na tija kubwa kwa wananchi kwani wataelewa namna nzuri ya kupata nishati muhimu ya mkaa pasipo kuharibu mazingira.”

Hata hivyo Serikali inapaswa kushirikiana na taasisi hizo ili kufanikisha utunzaji wa mazingira.

Uafiti wa kina uliofaywa na ilibainika kuwa kilimo cha kuhamahama ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa misitu.

Kwa kuzikatia matokeo na sababu zinazowafanya wananchi kuharibu misitu, Mradi wa Mkaa Endelevu umekuja na mkakati, Kilimo Hifadhi katika maeneo ya Wilaya ya Mvomero, Kilosa na Morogoro Vijijini mkoai Morogoro.

Mradi wa kilimo Endelevu umejikita katika kutoa eneo katika vikundi vya wakulima ili kuweza kuzijua na kuzitumia kanuni bora za kilimo.

Katika mradi huu wa Kilimo Hifadhi wananchi huelimishwa umuhimu wa kulima kwenye shamba moja kwa muda mrefu.

Wanapewa mbinu za kuandaa shamba bila kutumia motokwa sababu moto hupunguza rutuba na hutoa mwanya kwa magugu kuota kirahisi.

Aidha wakulima wanatakiwa kuacha masalia ya mazao na mimea pasipo kuyachoma moto li yaweze kuoza yenyewe na kuwa chanzo cha mbolea.

Wanaelimishwa juu ya kupanda mbegu mapema pamoja na kutumia mbolea ya samadi pamoja na mbolea rafiki wa mazingira.

‘”Mradi huu wa Kilimo Endelevu umesaidia kukifanya kilimo kuwa na tija kubwa kwa wakulima na kuepuka uharibifu wa mazingira. Wengi wao wameondokana na tabia ya kulima kilimo cha kuhama hama,’’ Anaeleza Maria Leshalu, Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, Wilaya ya Morogoro vijijini.

Mwenyekiti wa kikundi cha Jitegee, Maulid Luango anasema kilimo Endelevu ni mkombozi wa maisha yake kijijini na wakulima wengine wa kijiji cha Diguzi, Tarafa ya Ngerengere.

Dhamira kubwa ya mradi huu wa Kilimo Endelevu ni kuhakikisha kuwa misitu inalindwa na kubaki salama pasipo kuharibiwa.. Anamaliza kusema Nyamangalo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.