Nani kacheka, nani kalia usajili England

Rai - - MAKALA JAMSEIPITEMBA - MWANDISHI WETU NA

DIRISHA la usajili barani Ulaya limefungwa rasmi Agosti 31, 2017. Ilikuwa ni siku ya pilika pilika kwa kila timu iliyohitaji kupata saini za wachezaji katika siku hiyo ya mwisho.

Kimsingi usajili huo umekuwa ukifuatiliwa sana na wachambuzi wa soka barani ulaya hasa kwa timu zinazoaminika ndizo zenye ushindani wa kuwania taji la Lig Kuu ya England pamoja na nafasi nne za ushiriki wa Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Waliosajiliwa: Alexandre Lacazette (Lyon, Pauni Mil 52), Sead Kolasinac (Schalke, bure).

Walioondoka: Alex OxladeChamberlain (Liverpool, Pauni Mil 35), Wojciech Szczesny (Juventus, Pauni Mil 14), Gabriel Paulista (Valencia, Pauni Mil 10), Kieran Gibbs (West Brom, Pauni Mil 7), Yaya Sanogo (ameachwa), Carl Jenkinson (Birmingham, mkopo).

Arsenal hawajafanya usajili wa kutosha katika dirisha hili. Wamesajili mshambuliaji na beki mmoja. Kwa aina ya kikosi chao walihitaji kuwa na nguvu kubwa ya mabeki kwani hawana safu imara ya ulinzi. Bila shaka mechi dhidi ya Liverpool ilijidhihirisha hilo.

Pia hata katika safu ya kiungo hawako vizuri, tangu kuanza kwa msimu imeonekana hawana nguvu ya kupambana kwa dakika zote 90. Kweli walihitaji mshambuliaji na wamesajili mwenye uwezo wa kuiongoza safu yao.

CHELSEA

Waliosajiliwa: Danny Drinkwater (Leicester, Pauni Mil 35), Alvaro Morata (Real Madrid, Pauni Mil 70), Willy Caballero (Manchester City, bure), Antonio Rudiger (Roma, Pauni Mil 34), Tiemoue Bakayoko (Monaco, Pauni Mil 40), Davide Zappacosta (Torino, Pauni Mil 23)

Walioondoka: Nemanja Matic (Man Utd, Pauni Mil 40), Kurt Zouma (Stoke, mkopo), Nathaniel Chalobah (Watford, ada haijulikani), Ruben LoftusCheek (Crystal Palace, mkopo), Juan Cuadrado (Juventus, Pauni Mil 17.3), Christian Atsu (Newcastle, Pauni Mil 6.2), Asmir Begovic (Bournemouth, ada haijulikani), Dominic Solanke (Liverpool, makubaliano), John Terry (Aston Villa, bure), Nathan Ake (Bournemouth, Pauni Mil 20), Tammy Abraham (Swansea, mkopo).

Inaonekana Diego Costa hatocheza tena Chelsea, licha ya jina lake kuwepo katika orodha ya wachezaji 25 wa timu hiyo. Wamefanikiwa kumsajili Alvaro Morata kutoka Real Madrid, ni mshambuliaji mzuri lakini ataweza kufunga idadi ya magoli aliyokuwa anafunga Mhispania mwenzake?

Wamemuuza Matic, lakini wamefanya usajili wa viungo wawili wakabaji, Bakayoko na Drinkwater. Ni usajili mzuri kwao, pia wamefanya usajili wa Rudiger ambaye ataziba nafasi ya John Terry. Wanaweza kutetea ubingwa wao kama watakuwa vizuri zaidi ya msimu uliopita.

LIVERPOOL

Waliosajiliwa: Dominic Solanke (Chelsea, maelewano), Mohamed Salah (Roma, Pauni Mil 34.3), Andy Robertson (Hull, Pauni Mil 10), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal, Pauni Mil 35).

Walioondoka: Divock Origi (Wolfsburg, mkopo), Andre Wisdom (Derby, ada haijulikani), Kevin Stewart (Hull, ada haijulikani), Sheyi Ojo (Fulham, mkopo), Lucas Leiva (Lazio, Pauni Mil 5), Mamadou Sakho (Crystal Palace, ada haijulikani)

Hawajafanya usajili wa kutisha. Sawa, wamempata Chamberlain, lakini unajiuliza ataenda kucheza nafasi ipi? Ikiwa yeye mwenyewe anahitaji kucheza kiungo cha kati ambako kuna Emre Can, Gini Wijnaldum na Jordan Henderson.

Kwa upande wa Salah ni sawa sababu walihitaji nguvu kubwa katika eneo la ushambuliaji, pia Jurgen Klopp alihitaji machaguo mengi ya ushambuliaji kwa sababu ana mashindano mengi msimu huu.

Solanke ni mchezaji chipukizi, ana kipaji kikubwa sana ana uwezo wa kucheza nafasi kadhaa kama vile kiungo cha kati, pembeni na mshambuliaji.

Sehemu ambayo hawajaitendea haki ni safu yao ya ulinzi. Hawako imara sana, walihitaji beki wa kati mmoja ambaye ataituliza safu hiyo, kumkosa Virgil van Dijk ni pigo kwao. Usajili wa beki huyo ulikuwa muhimu zaidi kwao.

MAN CITY

Waliosajiliwa: Benjamin Mendy (Monaco, Pauni Mil 49.2), Danilo (Real Madrid, Pauni Mil 26.9), Bernardo Silva (Monaco, Pauni Mil 43), Ederson (Benfica, Pauni Mil 34.7), Kyle Walker (Tottenham, Pauni Mil 50).

Walioondoka: Wilfried Bony (Swansea, Pauni Mil 12), Fernando (Galatasaray, ada haijulikani), Kelechi Iheanacho (Leicester, Pauni Mil 25), Pablo Zabaleta (West Ham, bure), Gael Clichy (Istanbul Basaksehir, bure), Jesus Navas (Sevilla, bure), Willy Cabellero (Chelsea, bure), Bacary Sagna (ameachwa), Nolito (Sevilla, ada haijulikani), Joe Hart (West Ham, mkopo), Samir Nasri (Antalyaspor, ada haijulikani), Aleksandar Kolarov (Roma, Pauni Mil 4.5).

Pep Guardiola lazima apewe hongera kwa usajili alioufanya. Amesajili aliowahitaji na kuwaondoa asiowahitaji waliyoifanya timu hiyo ikimaliza nafasi ya tatu msimu uliopita.

Licha ya kufanya usajili huo, bado walihitaji beki mmoja wa kati, laity wangempata Johnny Evans, hakika angekuwa sahihi kwa falsafa ya Guardiola anayependa mpira wa pasi kuanzia nyuma.

Katika nafasi zingine wamesajili vizuri. Wana aina ya wachezaji wanaoweza kuwapa matokeo muda wowote kama ilivyokuwa kwenye michezo miwili iliyopita dhidi ya Everton na Burnley.

MAN UNTD

Waliosajiliwa: Victor Lindelof (Benfica, Pauni Mil 30.7), Romelu Lukaku (Everton, Pauni Mil 90), Nemanja Matic (Chelsea, Pauni Mil 40), Zlatan Ibrahimovic (bure).

Waliondoka: Wayne Rooney (Everton, ada haijulikani), Adnan Januzaj (Real Sociedad, ada haijulikani), Cameron Borthwick-Jackson (Leeds, mkopo), Timothy Fosu-Mensah (Crystal Palace, mkopo), Sam Johnstone (Aston Villa, mkopo), Andreas Pereira (Valencia, mkopo).

Jose Mourinho amefanya usajili mzuri sana kwa kikosi chake. Ingizo la Lukaku na Matic wameleta kitu kilichokosekana msimu uliopita.

Matic ana uwezo wa kutuliza mashambulizi ya wapinzani kisha kuanzisha mashambulizi kwa kupiga pasi zenye madhara kwa wapinzani. Lukaku ni mfungaji mzuri wa mabao, msimu uliopita alifunga mabao 25.

Licha ya Mourinho kushindwa kupata saini ya kiungo wa pembeni mmoja, bado ana wachezaji wanaoweza kufanya kazi hiyo bila wasiwasi kama vile Anthony Martial, Juan Mata na Marcus Rashford.

Kitu muhimu zaidi kwake alihitaji mlinzi wa kushoto asaidiane na Daley Blind huku Luke Shaw akiwa bado majeruhi.

Mourinho

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.