WAZIRI LUKUVI: Wadau jitokezeni kutatua kero ya maji

Rai - - MAONI/KATUNI - NA FRANCIS GODWIN, IRINGA

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia serikali kutatua kero ya maji katika vijiji mbalimbali nchini.

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia serikali kutatua kero ya maji katika vijiji mbalimbali nchini.

Lukuvi alitoa kauli juzi katika kijiji cha Mapogolo kata ya Idodi mkoani Iringa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa visima viwili vinavyotarajiwa kuwanufaisha wanakijiji zaidi ya 6000 wa vijiji vya Mapogolo na Ikorongo mkoani Iringa.

Visima hivyo vinavyotumia umeme wa jua vimefadhiliwa na madhehebu ya Ismailia pamoja na taasisi yao kutoka kusini iliyoshirikiana na taasisi ya Agakhan Development Network (ADKN).

Lukuvi alisema wafadhili hao wameona umuhimu wa upatikanaji wa maji hasa katika vijiji ambavyo vinakabiliwa na ukame.

“Agakhan Development (AKDN) ni taasisi iliyoundwa na mtukufu Agakhan kwa zaidi ya miaka 100 imeendelea kukuza na kuboresha maendeleo ya Tanzania kwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu, kilimo na kuboresha miundombinu ili kukuza uchumi na maisha bora kwa watanzania.

“Pamoja na jitihada zilizofanywa na AKDN kwa kusaidia wananchi kutatua kero ya maji bado serikali inayomalengo makubwa kutatua kero ya maji katika vijiji vyote nchini ifikapo mwaka 2020, hivyo kuchimbwa kwa visima hivyo kutasaidia kupunguza kero ya maji iliyopo wakati serikali inakuja na suluhisho la kudumu ya kumaliza kero ya maji katika vijiji,” alisema.

Alisema wakati serikali ya awamu ya tano inajiandaa kutatua kero hiyo ya maji ila bado maji hayo ya visima ni mazuri zaidi kwani yatakuwepo wakati wote tofauti na maji ya bomba ambayo pindi bomba zinapokatika huduma hiyo hukosekana .

Kwa upande wake Makamu Rais wa jumuiya ya Ismailia Tanzania, Kamal Khimji akizungumza kwa niaba ya Rais wa jumuiya hiyo Tanzania alisema kuwa miradi hiyo ya maji imedhaminiwa na madhehebu ya Shia imami Ismailia kupitia taasisi yao ya kusini kwa kushirikiana na Agakhan Development Network (AKDN) ambayo imeendelea kusaidia jamii katika mambo ya maendeleo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi ambaye ni Mbunge wa Ismani Iringa (kulia) akishirikiana na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Ismailia Tanzania, Kamal Khimji kuzindua mradi wa visima viwili vilivyofadhiliwa madhehebu ya Shia imami Ismailia kupitia taasisi yao ya kusini kwa kushirikiana na Agakhan Development Network (AKDN) juzi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.