Jamhuri ya Muungano ya ‘Watu Wasiojulikana’

Rai - - MAKALA - Zitto Kabwe

ABSALOM Kibanda aliteswa na kuumizwa na watu wasiojulikana. Mpaka leo hawajajulikana.

Ben Saanane amepotezwa na watu wasiojulikana.

Ofisi za Wakili Omar Said Shaaban Zanzibar zililipuliwa na watu wasiojulikana, mpaka Leo hawajajulikana.

Ofisi za Uwakili za IMMMA Advocates Dar Es Salaam zililipuliwa na watu wasiojulikana. Mpaka leo hawajajulikana

Mwanaharakati dhidi ya Ujangili Bwana Lotter aliuawa Dar Es Salaam na watu wasiojulikana. Mpaka leo hawajajulikana

Mbunge Tundu Lissu amepigwa risasi 32 mchana kweupe mjini Dodoma Bunge likiendelea. Waliompiga risasi ni watu wasiojulikana. Watu wasiojulikana wanasakwa na Polisi.

Huu si Utanzania. Tukatae kuwa Jamhuri ya Muungano wa Watu Wasiojulikana

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.