Stars itapatikana kwa vigezo si makubaliano

Rai - - MBELE - MWANDISHI WETU NA MITANDAO

ILIWAHI kutokea kwa wakati mmoja Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuwa nahodha wa Yanga na timu ya taifa, pia Agrey Morris, nahodha wa Azam huku Said Cholo, kuwa nahodha wa Simba. Hii iliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita na hata sasa bado wapo wengi wakinguuruma ndani ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Yote hayo watu waliona

KUFUKUZWA kwa Kocha mkongwe kwenye mchezo wa soka, Carlo Ancelotti, na waliokuwa waajiri wake, klabu ya Bayern Munich, kulitegemewa na wadau wengi walioona jinsi kikosi chake kilivyokuwa kikicheza katika siku za

hivi karibuni.

Ilitambulika mapema na wazi kuwa kocha huyo alikuwa akisumbuliwa na changamoto nyingi katika timu hiyo, changamoto kuu ikiwa ni wachezaji wake kadhaa ambao alikuwa akitofautiana nao, na wengine

waliohusishwa na kutoelewana naye walistaafu miezi michache iliyopita.

Tatizo hilo alilikiri rais wa klabu ya Bayern, Uli Hoeness, ambaye alisema kuwa kulikuwa na nyota watano ambao walikuwa hawamkubali kocha huyo wa Kiitaliano .

Baada ya rais huyo kunukuliwa mapema siku chache zilizopita, wengi walijiuliza ni akina nani hao ambao walikuwa wameunda umoja wao wa kupingana na Ancelotti?

Vyombo vya habari vya Ujerumani, hasa vile vya michezo viliibuka na taarifa huku vikiwataja wachezaji hao kuhusika kwa asilimia kubwa na sekeseke hilo.

Wa kwanza kabisa ni winga Arjen Robben. Huyu baadhi ya wadau wa soka watakuwa wakielewa jinsi alivyokuwa hamuelewi Ancelotti.

Katika muda wote ambao walikuwa wakifanya kazi pamoja, nyota huyo na kocha wake hawakuwa katika maelewano mazuri, ambapo majibu yake kwa mwandishi wa habari hivi karibuni wakati Bayern ikikutana na kichapo kikali cha mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kutoka kwa PSG yalidhihirisha kila kitu.

Robben, aliulizwa swali moja tu na mwandishi huyo wa habari kama wachezaji wako pamoja na kocha wao katika nyakati hizi ngumu, swali ambalo winga huyo aligoma kulijibu kwa kusema: “Sitalijibu hilo swali.”

Katika kudhihirisha kuwa Robben alihusika kwa kiasi kikubwa na kuondoka kwa Anceloti sambamba na kocha huyo kutopata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mastaa wake na hata waajiri wake kwa ujumla, vigogo wa klabu walimheshimu zaidi Robben kuliko Ancelotti. Na ni kitu kinachoingia akilini kusema kwamba kocha huyo ‘alipewa machaguo’ aidha atimuliwe au ajiuzulu mwenyewe!

Franck Ribery naye anachukua nafasi hapa. Winga huyo ambaye amecheza pamoja na Robben kwa muda mrefu sasa, alikuwa akikerwa mno na sera ya Ancelotti ya kufanya mabadiliko ya kikosi kila baada ya mechi, huku Ribery akiwa mmoja wa wahanga wa sera hiyo.

Uhusiano baina yake na Ancelotti ukavunjikia hapo na haikuwezekana tena kuurudisha kwenye mstari. Kwani Muitaliano huyo alikuwa akimtumia Ribery kutokea benchi au kumfanyia mabadiliko ndani ya mechi huku dakika zikiwa bado za kutosha.

Mmoja wa wachezaji wanaoheshimika Bayern, na wengi wao humuona kama mtu mpole, Thomas Muller, naye ana mkono wake hapa.

Ule umaarufu wa Muller kama mmoja wa mastraika wa kiwango cha hali ya juu barani Ulaya uliathirika kutokana na uwepo wa Ancelotti pale Bayern.

Wengiwenumtamkumbuka Muller alivyokuwa chini ya makocha kama Louis van Gaal na Pep Guardiola, lakini kwa huyu Ancelotti, Muller alirudi nyuma badala ya kwenda mbele zaidi.

Kiungo mshambuliaji huyo alikuwa akiathirika kutokana na kukosa muda wa kutosha wa kucheza, na ni kitu ambacho alikuwa haoni soo kukisema hadharani.

“Sielewi kwa kweli ni kipi ambacho (Ancelotti) anakitaka (kutoka kwake),” maneno aliyowahi kunukuliwa Muller akimzungumzia Ancelotti.

Katika mtanange dhidi ya PSG, Bayern ilionekana kutokuwa na uelewano na pia ilikosa kiongozi ambaye mara nyingi amekuwa ni beki Jerome Boateng.

Kwenye hiyo mechi, Boateng hakuanzishwa. Hata kwenye benchi hakukaa. Hata Ancelotti hakuonesha kujutia uamuzi wake wa kutomtumia Boateng.

Kwa hatua hiyo ya Ancelotti, chombo cha habari maalum cha klabu ya Bayern, ‘Bavarian Football Works’ kilimjumuisha beki Jerome katika orodha ya maadui wa Ancelotti.

Mats Hummels? Robert Lewandowski? Au Kingsley Coman? Bado haijajulikana adui wake wa tano ingawa inaonekana kama anatoka katika hayo majina matatu hapo.

Kwa yeyote atakayekuwa wa tano, ilionekana wazi Bayern Munich iliwaamini zaidi wachezaji wao kuliko kocha.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.