.... asisubiri kiporo cha Katib

Rai - - MAKALA - NA MANENO SELANYIKA

H ATIMA ya mchakato wa kupata Katiba Mpya nchini bado ni ndoto kwani imeonekana kupigwa danadana, hivyo Watanzania kushindwa kuelewa hatima ya jambo hilo muhimu katika maendeleo ya Taifa.

Serikali iliyopo madarakani wakati walipokuwa katika harakati za kuwania nyadhifa mbalimbali katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 moja, kati ya ahadi walizoahidi ni kuhakikisha wanaendeleza mchakato wa kupata Katiba Mpya.

Hata hivyo, baada ya kuingia madarakani takribani miaka miwili sasa hakuna kiongozi yeyote anayetaka kuzungumzia suala hilo, hivyo Watanzania kuzidi kuachwa njia panda.

Wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu wameendelea kupaza sauti zao na kuhoji kila uchwao kuhusu ni lini sasa Serikali itaanza mkakati, lengo lao kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata stahiki zao endapo tu baadhi ya vipengele katika Katiba vitaboreshwa ama kurekebishwa.

Miongoni mwa taasisi zinazofuatilia kwa makini ahadi za viongozi wa Serikali kuhusu suala la mabadiliko ya Katiba Mpya ni Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), ambao kila wakati wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaikumbusha Serikali mchakato huo.

Akitoa taarifa kuhusu hatima ya mchakato wa Katiba hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukata, Hebron Mwakagenda, anasema baada ya kufuatilia kwa makini Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mfululizo wa mwaka wa fedha 2016/17 na 2017/ 18, kuna mapungufu mengi mojawapo ni kutotengewa fedha kwa ajili ya mchakato huo.

Anasema mbali na kutotengewa kwa fungu hilo pia hakuna maelezo yoyote ya kina juu ya hatima ya mchakato huo ambao ni muhimu kwa masilahi ya mwananchi wa kawaida.

“Waziri wa Katiba na Sheria, Professa Kabudi, anasema atafufua lakini maneno na maandiko ya Serikali yanakataa kabisa yaani mwaka huu ukiisha ukweli ni kwamba Watanzania wasahau mchakato wa kupata Katiba mpya kwa kuwa patakuwapo na maandalizi ya chaguzi mbalimbali kama wa kupatikana kwa viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na ule Uchaguzi Mkuu 2020.

“Ushauri wetu kwa Rais Magufuli apeleke bungeni bajeti ya dharura kinyume na hapo ikishidhikana itakuwa ngumu kwa sababu bajeti ya mwakani itakuwa na masuala mengi,” anasema Mwakagenda.

Anasema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, hapo katikati patakuwa na maandalizi ya uandikishwaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura hivyo ni vugumu sana kufanya mchakato wa Katiba Mpya kwa sababu patakuwa hakuna utulivu.

Anasema awali matumaini ya Watanzania walio wengi walitambua kwamba mchakato wa kupata Katiba mpya ungeweza kukamilishwa katika msimu wa kwanza wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano, lakini hadi sasa matumaini yamekuwa hafifu.

Mwakagenda anasema endapo mchakato huo hautakamilishwa kabla ya mwaka 2020, basi suala hili liangaliwe na kwamba baadhi ya vipengele vya sheria vilivyopo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na ile ya Zanzibar ya mwaka 1984 vifanyiwe marekebisho ya msingi (Minimum Reforms), ili kupunguza kasoro mbalimbali zinazolalamikiwa hasa kwanye Uchaguzi wa Tanzania.

Aidha, Mkurug anataja baadhi ya vip vilivyopo katika Kati vinavyolalamikiwa ku na kuwa na uhuru ka Taifa ya Uchaguzi na il Zanzibar.

Kasoro nyingine n ya mgombea huru hapa nchini, uwepo w kuhoji matokeo ya uc ya urais mahakam vyama vya siasa ku na kisheria kwa lengo mgombea mmoja.

Sababu nyingine n Katiba na kwenye sh uwakilishi sawia kati na mwanamume vya maamuzi kama ya madiwani, Bunge Wawakilishi.

“Tutambue tu kwa uhalifu na ukiukwaji yanayoendelea amba Polisi kukamata kama wa vyama hasa pinz udhaifu kwa Katiba iliy

“Kutungwa kwa s mpya zinawaban washindwe kujieleza, za utafiti na makos kutishwa kwa wab na mau Jeshi la na ma

www.rai.co.tz

ya wakuu wa wilaya; hayo yote yanatokana na udhaifu wa Katiba,” anasema.

Mwakagenda anasema huu ndio wakati Serikali ambayo ni sikivu itasikiliza na kuyatenda kwa vitendo ili kupata Katiba itokanayo na maoni ya wananchi na kwamba si kubaguana, akitolea mfano Chama Cha Mapinduzi (CCM), chenyewe kinaendelea na mikutano bila kuingiliwa na Polisi wakati kile cha Wananchi CUF kikivurugwa na kukosa mwelekeo.

UCHAGUZI WA KENYA

Mkurugenzi huyo anasema katika uchaguzi wa Kenya ambayo ni nchi ya kwanza Afrika na ya tatu duniani kwa kutengua matokeo ya uchaguzi, anasema si vibaya Tanzania wakaiga uamuzi wa Kenya kwa kubadili Katiba.

Anasema nchi nyingi za Afrika, majaji bado hawana uhuru hasa wa kutoa maamuzi kwa kuwa jaji mkuu mara nyingi ndio anakaimu nafasi hizo, ambapo hushindwa kusimamia zoezi zima kwa kuwa sheria bado inamlinda.

Anasema kwa sasa Kenya kuna kesi mahakamani zaidi ya 100 za wabunge na madiwani zimefunguliwa kupinga matokeo na kwamba pindi utakaporudiwa watakaochaguliwa watakuwa wamepita kwa amani na uhalali.

“Kule Kenya hawa majaji hawateuliwi na rais tofauti na ilivyo hapa kwetu ndio maana wanapata wakati mgumu kuchukua maamuzi.

“Tumeona kabisa jinsi Tume ya Taifa ya Kenya ilivyoshindwa kuleta fomu kadhaa kwa ajili ya kuthibitisha kabla ya Mahakama ya Juu kule Kenya kuchukua uamuzi,” anasema Mwakagenda.

Kuhusu suala la mgombea binafsi, anasema lina umuhimu wake kuwekwa katika Katiba yetu kwa sababu baadhi ya vyama vya siasa havitendi haki kwani humteua mgombea wasiyemtaka.

“Nchini Kenya wagombea binafsi ngazi za ugavana, ubunge wengi wameshinda ambao ni wa jinsia zote,” anasema Mwakagenda.

Anasema katika nchi zinazofuata mfumo wa demokrasia, viongozi huchaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi baada kunadi sera na mikakati watakayotumia kuwaletea wananchi maendeleo endapo watapewa nafasi hizo.

Kwa mantiki hiyo, Serikali inatakiwa kujipanga namna ya kutekeleza ahadi walizoziahidi kwa wananchi ikiwemo ukamilishwaji wa mchakato wa kupata Katiba Mpya.

Aidha, itakuwa ni heshima kubwa kwa Serikali ya Awamu ya Tano endapo itaweza kukamilisha kabla ya uchaguzi mkuu ujao, vinginevyo itabaki kwenye historia kwamba Serikali ya awamu hii imezima ndoto za Watanzania katika mchakato wa kupata Katiba Mpya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.