Amani,utulivu bila upendo ni unafiki

Rai - - MAKALA - NA MWANDISHI WETU

AMANI…Amani na utulivu.Nikiandika maneno hayo najisikia kuwaza amani na utulivu huletwa na nini?

Jibu ninalolipata ni upendo, je nitawezaje kupata upendo? Ni lazima niwe karibu na wenzangu kwa kuleta ushirikiano.

Ni jambo lililonishtua niliposoma RAI ya Septemba 7 – 13,mwaka huu na kuona Magdalena Sakaya hana haja ya ushirikiano, yeye anafanya kazi na nani iwapo hana ushirikiano na wenzake?

Popote pale ulipo katika maisha yako ni lazima uwe na upendo na huwezi kuwa na upendo bila kuwa na mtu mnayeshirikiana.

Mama Sakaya serikali ni nani ni viti vilivyomo ama watu waliomo Bungeni ambao watakupa jibu la ulichohoji?

Pamoja na Spika kufuata kanuni, lakini atakayekujibu ni mwenzako, Spika ambaye hamna ushirikiano atakayejibu kwa kutokuwa na ushirikiano.

La ajabu Spika ananyamazia jambo hilo ambalo wabunge walionyesha kuwa ushirikiano ndio kitu kinacholeta upendo katika Bunge na kuwa Bunge ni la wote sio la CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi wala ACT Mzalendo.

Sijui Mama Sakaya ulipata kuishi vijijini, adhabu kubwa ya kuleta amani na utulivu ni ushirikiano, usipotoa ushirikiano kwa wenzako hutengwa na wanakijiji wenzako, huwezi kupewa ushirikiano kama wewe mwenyewe huna ushirikiano.

Nashangaa Spika anaweza kukaa bungeni na watu ambao hawana ushirikiano bila kutafuta jinsi ya kuwafanya washirikiane na hilo Spika unalijua.

Mara nyingi majirani hutafuta amani kwa kushirikiana, kuna vikundi mbalimbali vya Kiislamu na Kikristo hufanya mambo yao kwa pamoja ili kutafuta amani na ushirikiano.

Hili jambo sio dogo kulitenda na si dogo kulitizama na kusema acha hao wanajifurahisha sivyo Spika wangu.

MamaSakayausileteubabe kwa neno hilo ushirikiano, wewe mwenyewe ingawa ni Naibu Katibu wa CUF na Mbunge wa Kaliua, je una ushirikiano na Katibu Mkuu wako, mpaka sasa hujui ni nani na hujui kuna CUF ngapi. Kuna CUF Maalim Seif ama CUF Lipumba. Kwa ajili ya kukosa ushirikiano ndio maana majina hayo yanatokea na hata Msajili wa Vyama vya Siasa anashindwa kueleza umma kuwa kuna CUF ngapi ama vyama vya upinzani ni vingapi sio tungojee wakati wa uchaguzi ukikaribia. Kukosa ushirikiano kunaleta mengi ya kuzuia maendeleo.

Wakati Mwenyekiti wako Profesa Lipumba alipokimbia uchaguzi hakutegemea kuwa atakuja kufukuza wabunge waliochaguliwa na watu wenye nia ya chama. Leo pamoja na kwamba kesi bado haijahukumiwa anaanza kuleta kutoshirikiana na wenzake, serikali inaangalia. Ushirikiano ndio silaha kubwa ya amani. Mnaweza kuwa askari wengi kati ya maadui, lakini kama hamna ushirikiano mnasambaratishwa na maadui kidogo tu.

Naomba serikali ifikirie njia ya kuleta ushirikiano nchini, tusipite kelele bila kuelewa kinachotukosesha amani. Ni kama hivyo mtu mmoja anatamba tunamwangalia sio Spika wala Serikali. Haya yote ni kuachia makosa madogo madogo mwisho mazoea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.