KIMATAIFA:

UN NA CHANGAMOTO MPYA YA KOREA KASKAZINI

Rai - - MBELE - NA HILAL K SUED

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ni mtu aliyezingirwa na siku zake zinahesabiwa. Hata kwa wengi ambao siku zote hukana kuwepo kwa makundi ndani ya chama tawala cha Zanu PF, andiko hilo liko wazi sasa hivi. Mvutano uliokuwa ukitokota polepole sasa hivi umefikia hatua isiyioweza kusimamishwa.

Hakuna makonde yanayorushwa tena, kwani hakuna kitu cha kuficha. Kwamba makamu wa Rais wa nchi anaweza kuraruriwa waziwazi hadharani na si na mtu mwingine, bali mke wa rais, Grace Mugabe si kitu cha kuficha kwamba mtu huyo ni wa kuondoka tu wakati wowote.

Zimbabwe imekuwa na msururu wa makamo wa marais tangu ilipojipatia uhuru wake miaka 37 iliyopita. Ukiangalia kwa karibu historia ya viongozi hawa utagundua mwenendo mmoja wa ajabu, mwenendo ambao husema mengi kuhusu hali halisi ya kisiasa.

Hakuna makosa kuhusu Rais wa Zimbabwe, kwani nchi hiyo imemjua mtawala mkuu mmoja tu tangu Robert Mugabe awe Rais wa nchi hiyo.

Watu wazima nchini Zimbabwe wanakumbuka utawala wa juu katika miaka ya 90 ambao ulijumuisha Makamu wa Marais wawili – Joshua Nkomo na Simon Muzenda.

Wawili hao walikuwa na umri mkubwa kuliko Mugabe na walikufa wakiwa kwenye nyadhifa zao. Nkomo alipachikwa jina la “Baba wa Zimbabwe” na alikufa Julai 1, 1999 akiwa na umri wa miaka 82. Hakuna kilichokuwa kinatoka kinywani mwake zaidi ya kuhimiza umoja wa Zimbabwe.

Katika kipindi chake chote akiwa Makamu wa Rais hakuwahi hata siku moja kutuhumiwa kwa kutaka kupora madaraka ya juu. Kuzungumzia suala la kurithishiana madaraka lilikuwa halipo kabisa.

Na vivyo hivyo ilikuwa kwa Muzenda ambaye aliridhika kubakia Makamo wa Rais hadi siku alipofariki akiwa na umri mkubwa. Hata hivyo ilikuwa dhahiri kwamba kutokuwapo kuzungumzia suala la kurithishiana madaraka lilitokana na umri wao mkubwa.

Swali la kujiuliza: Je, ilikuwa ni bahati tu iliyotokea kwamba viongozi hawa wawili ambao katika vipindi vyao kulikuwapo hali kubwa ya utulivu wa kisiasa, ilitokana na umri wao mkubwa kuliko ule wa Rais?

Wazee hawa wawili walionekana kuwa siyo tishio kwa “kiti cha enzi.” Aidha hakuna hata mmoja kati yao alikuwa na mipango ya kuanzisha makundi ya kutaka kupora madaraka.

Baada ya kutoweka kwa makamu wa marais hawa wawili wenye umri mkubwa alikuja Joseph Msika. Naye pia, kipindi chake cha unaibu kwa Mugabe kilikuwa cha utulivu hasa katika suala la kurithishiana madaraka – hususan ndani ya chama tawala.

Hakuna aliyemtuhumu Msika, ambaye pia alikuwa wa umri mkubwa, kwa kutaka kuleta chokochoko kuhusu madaraka ya juu. Na ndivyo ilivyokuwa kwa makamu wa rais aliyekuja baada ya Msika – John Nkomo.

Katika kipindi kikubwa cha umakamu wa rais Nkomo alikuwa akisumbuliwa na afya yake, lakini pia hakuonekana kuwa na tamaa yoyote ya kutaka kumrithi Mugabe.

Hivyo kwa wote hao makamu wa rais wanne – Nkomo, Muzenda, Msika na John Nkomo, kulikuwa hakuna kilichosikika kuhusu kutaka kumpora Mugabe madaraka au hata kuanzisha makundi kwa azma hiyo.

Hawakufanya hivyo ama kutokana na umri wao mkubwa, au afya zao kuwa si nzuri. Na hii ilikuwa ‘sifa’ moja kuu kwao kuwa makamu wa rais wazuri. Sasa ni lini hasa pale suala

la lurithishiana madaraka lilipoanza nchini Zimbabwe? Katika miaka ya karibuni, medani nzima ya kisiasa nchini humo inatawaliwa na tuhuma nyingi dhidi ya makamu wa marais mbali mbali walioshika nyadhifa hizo kutaka kumpora Mugabe madaraka.

Suala la kurithishiana madaraka lilianza kukua kwa kasi huku tuhuma nyingi zikirushwa na kujibiwa.

Hali hii ilianza baada ya uteuzi wa Joice Mujuru, mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa Rais nchini Zimbabwe. Hata hivyo uteuzi wake uliibua mshangao – kwani awali ulichukuliwa kama wa wale wengine waliomtangulia – kwamba hakuwa na tamaa zozote za kutaka kumrithi Mugabe.

Lakini uteuzi wake ulikuwa na kasoro moja – ingechukuwa muda mrefu kwa Wazimbabwe kukubali hata lile wazo tu la kuwapo kwa makamu wa rais mwanamke.

Lakini kwa upande mwingine uteuzi wa Mujuru mwaka 2004 ulilenga kuendeleza katika kutuliza ile dhana ya kutokuwa na makamu wa rais mkorofi. Lakini badala yake, hapo hapo ndipo matatizo yote yalipoanzia.

Katika miaka ya mwisho mwisho ya umakamu wa urais wa Mujuru, minong’ono isiyozoeleka ikaanza kusikika. Mujuru alikuwa na umri mdogo na alikuwa kipenzi cha wananchi wengi hasa vijana pamoja na ndani ya chama.

Lakini hadi kufikia mwisho wa 2013 uhasama na tuhumua dhidi yake zilifikia kiwango cha juu. Miongoni mwa tuhuma dhidi yake ni kutaka kuuendesha serikali sambamba na ile ya Mugabe pamoja na kutaka kumuua bosi wake.

Hivyo anguklo lake halikushangaza sana. Na laiti Mujuru angekuwa ni waziri tu wa kawaida, bila shaka bado angekuwa katika wadhifa wake. Ni umakamu wa rais ndiyo uliomponza.

Na sasa Emmerson Mnangagwa. Uteuzi wake kuwa Makamu wa Rais nao ukaanza kuonekana kutishia “kiti cha enzi.” Kama vile ilivyokuwa kwa Mujuru, leo hii naye anakabiliwa na tuhuma kadha dhidi ya serikali na dhidi ya Mugabe mwenyewe.

Upanga uliomuondoa Mujuru sasa hivi unamkabili Mnangagwa. Grace Mugabe ambaye ndiye aliyeongoza mashambulizi dhidi ya Mujuru, anaoneka tena akifanya hivyo hivyo dhidi ya Mnangagwa.

Hii ina maana ya kwamba kiti cha umakamu wa rais nchini Zimbabwe ni cha moto kweli kweli na kina aina fulani ya laana ndani yake na hasa kinaposhikwa na watu wa umri mdogo wanaodhaniwa kuwa na tama ya madaraka.

Emmerson Mnangagwa

Joice Mujuru

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.