Wasanii, wanamichezo watakiwa kutumia vizuri fursa

Rai - - MICHEZO - NA OSCAR ASSENGA,TANGA

WASANII na wanamichezo kwa ujumla wamekumbushwa kutumia vizuri fursa wanazozipata kupitia fani zao ili kusaidia pia kukuza uchumi wa nchi.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella wakati akipokea msaada wa vifaa tiba mbalimbali kutoka kwa Umoja wa Wasanii Tanzania ikiwa ni malum kwa ajili ya hospitali za mkoa huo.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 29 ambavyo ni X-Ray, Ultra Sound, viti vya kutembea wagonjwa, Magongo ya walemavu pamoja na craches vimetolewa na wasanii hao ili kusaidia kuinua X-ray, ultra Sound kwa ajili ya kuinua sekta ya afya mkoani huko huku wakilenga zaidi kuokoa maisha ya wakina mama wajawazito na watoto.

Akizungumzia nafasi yao kwa jamii, alisema sekta hiyo ya michezo na sanaa inaweza kusaidia sana kuinua uchumi wa chini iwapo tu watatambua dhamana kubwa waliyonayo kwa taifa lao.

Alisema mchango wao ukiungana na jitihada za wazi za Serikali kuna uwezekano mkubwa maendeleo yakapatikana katika kipindi kifupi.

katika jitihada zake za kukuza

Mkuu huyo wa mkoa ameoneshwa pia kuridhishwa na jitihada za awali zinazoonyeshwa na wasanii kuanzia katika harakati za Uchaguzi mkuu kwa kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi na sasa wamekuwa wakiendelea kusaidia serikali yao kutokana na wanachoingiza kupitia fani yao.

“Ninatambua asilimia kubwa mlizunguka kwenye kampeni mkiwaomba watanzania wamchague Rais Dk. John Magufuli kutokana na dhamira yake nzuri ya kuleta

maendeleo lakini pia hivi sasa mnashirikiana naye kwenye sekta ya afya kwa kumuunga mkono kwa kutoa mchango wenu niwaambie huu ni uzalendo ambao ni msingi wa maendeleo ya Taifa “Alisema.

Imeelezwa hatua hiyo ni uzalendo mkubwa wan chi na taifa hivyo wadau wengine nao wametakiwa kuiga mfano huo.

Alisema wasanii kupitia shughuli zao wanaweza kusaidia juhudi zilizoanzishwa kwa ajili ya kusaidia kufungua fursa za kiuchumi na kuhamasisha jamii kuwajibika ipasavyo ili kuchochea kasi ya maendeleo.

Kujitolea kwa wasanii hao kunadhihirisha wazi kukubali kwao kuungana na Rais Magufuli ambaye muda mwingi amekuwa akiwahimiza juu ya utunzaji wa rasilimali za nchi hivyo kwao ni faraja na itachangia kasi zaidi.

Hata hivyo wasanii hao kwa kauli moja walisema uamuzi wao wa kusaidia sekta ya afya unatokana na ukweli kwamba taifa lenye matatizo ya afya na tiba kamwe haliwezi kuwa imara hivyo juhudi zao ni katika kuhakikisha taifa linakwua na

Wakawaasa pia watanzania wenzao hasa wafanyabiashara kulipa kodi inayostahili na kwa wakati ili kila mmoja anufaike na huduma zinazotolewa na serikali kutokana na kodi hizo.

Wasanii hao wametakiwa kutembelea wilaya za mkoa huo ili kuangalia fursa zilizopo na ikiwezekana kuzitumia katika kujiongezea kipato chao lakini pia serikali nayo ikinufaika.

Moja kati ya vitu walivyoshauriwa kuviangalia ni pamoja na sekta ya ardhi katika wilaya mbalimbali za mkoa huo ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza.

Wasanii wa filamu, Asha Boko (kushoto) na Tausi Mdegela wakitoa burudani muda mfupi kabla ya kumkabidhi vifaa tiba Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, kwa ajili ya hospital za Mkoa huo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.