Hii ni CCM mpya ya mabubu?

Rai - - WIK -

KWENYE Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Pili, neon “Bubu” lina maana mbili. Neno hilo tunaambiwa kuwa ni nomino yenye maana sawa na ‘bubwi” hivyo waweza kusema “Mabubu”, mtu asiyeweza kusema na pili ni mtu asiyependa kusema. Aghalabu kiafya ‘bubu’ ni kitu kinachotokana na tatizo fulani mwilini, lakini ipo maana ya mtu kuamua kunyamaza na kutojishughulisha na kauli au jambo fulani.

Rafiki yangu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole (pichani) namhurumia sana. Namhurumia kwasababu kipindi kirefu amekuwa kiongozi pasipo kutoa suati yoyote yenye kuashiria anashughulikia kwa ukamilifu kauli mbiu yake ya “CCM mpya”.

Ninakubaliana naye kuwa kauli mbiu hiyo inalenga kurudia chama kwa wananchi. Natambua kuwa kanuni zimebadilishwa. Katiba imefanyiwa marekebisho na miongozi mbalimbali ndani ya chama inaonyesha kuwa chama cha mapinduzi kimechagua mwelekeo mpya.

Pamoja na mwelekeo huo bado nakiona chama hicho hakiwezi tena kuwa cha wakulima na wafanyakazi. Dunia imebadilikia. CCM kimebadilika na hakiwezi kujigamba kwamba kinashikilia mzizi uleule wa ‘wakulima na wafanyakazi’ wakati kila mara tumesikia kauli ya ‘chama kijitegemee, ksitegemee fedha za matajiri’.

Hiyo ni kauli inayoeleweka mno kwa wanachama wa chama cha mapinduzi lakini haiwezi kuakisi chochote mbele ya siasa mambo leo. Siasa ambazo zinachagiza “Marafiki wa chama” kuwa na nafasi yao ya kutoa mchango wao kwa chama chochote. Marafiki wa chama wanatokana na ‘wadau’ ambao ni zao la wanachama wa chama wenye hadhi ya juu kuliko wanachama wa kawaida.

Ndiyo kusema “marafiki wa chama” ni watu wa daraja la juu ambalo mchango wao haugusiki. Tukitaka kuelewa hilo turudi kwenye aina ya wanachama wa CCM au chama chochote cha siasa. Kila chama cha siasa kuanzia NCCR Mageuzi, TLP, Chadema, CUF, ACT-wazalendo na kadhalika, vyote hivi vina kundi la “marafiki wa chama”.

Kwahiyo tunapozungumzia CCM mpya hatuwezi kujidanganya kusema kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi tena. Bali ni chama cha wadau marafiki wa chama ambao kwa namna moja au nyingine wanajitolea bila kutegemea faida yoyote, kwa mapenzi yao au kunuia mambo fulani ambayo0 yatapatikana kwa chama husika.

Sasa hii CCM mpya anayohubiri rafiki yangu Polepole ndiyo hasa inanitiza. Nafahamu ningeweza kumuuliza swali moja kwa moja yeye mwenyewe, lakini nimeona tushirikiane nawe msomaji tutafakari kwa pamoja. Ni CCM mpya ya aina gani anayozungumzia rafiki yangu Polepole?

Kuna mifano ambayo rafiki yangu Polepole na wenzake katika Idara yao ya Uenezi wanapaswa kujiuliza. Si hapo pekee pia hata Umoja wa Vijana wa CCM wanapaswa kujiuliza pia. Kwanini imekuwa hivyo au ni mwelekeo mpya wa kwenda wapi na kuwa mabubu?

Sifa ya kwanza ya chama cha siasa ni kujiuza. Chama cha mapinduzi ni kikongwe na kikubwa sana barani Afrika. Kinastahili sifa hiyo kwakuwa wananchi wamekipatia ridhaa. Sasa basi, chama kinapojiuza maana yake kimekuwa na mikakati, sera, mipango na kudumisha amani kwa wananchama wake pamoja na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wanaowatawala.

Rafiki zangu wa CCM siku hizi wanasnishangaza sana. Wao ni chama tawala lakini wamekuwa wakisahau jukumu lao la msingi kabisa “mapambano ya kisiasa”. Katika mapambano ya kisiasa kitu cha kwanza tunachofanya ni kuhakikisha tunamshinda mshindani wetu iwe kwenye vyombo vya habari na kila jukwaa tunalopata nafasi tunahakikisha hafurukuti. Kwamba chama kinakuwa maarufu zaidi kwa mambo mbalimbali. Tunakiweka chama midomoni mwa washabiki wake, wanachama wake, wanazuoni na watu wa kila kada.

Kwahiyo chama kinaseti ajenda ambayo inazungumzwa na kuwa mjadala zaidi huku kukiwa kinapanga kufanya mambo mengine yatakayokuwa ajenda. Lakini hayo yote siku hizi kwenye chama cha mapinduzi yamekauka. Siwezi kuhitimisha kuwa wameishiwa makali lakini hali hiyo imeshangaza.

Mathalani, tunapozungumzia CCM Mpya huku kikishindwa kujibu makombora ya wapinzani wake kisha kutegemea msemaji wa serikali yao atoe majibu tuna maanisha nini? Mtu yeyote asiniambie kuwa serikali ni ya chama tawala, kwasababu nafahamu yapo mambo ya kisiasa yanatolewa ufafanuzi na serikali bila hata sababu, wakati chama kipo na idara ya euenzi ipo. Hapo hapo nisiambiwe kuwa serikali inao wajibu wa kujibu, kwasababu sifa mojawapo ya Uenezi ni kuhakikisha unapangua hoja kinzani na kupanga hoja za kuwashinda wapinzani wako.

Nimewahi kuandika hapa, kuwa lilikuwa kosa la kiufundu kuziacha siku 18 trangu Agosti mosi mwaka huu kutozungumzia suala la ndege yetu aina ya Bombardier ambayo Mwenyekiti aliahidi kuwa itawasili mwezi Julai mwaka huu. Tuliona mwezi Julai ulikwisha hivi hivi, ikawa kimya. CCM mpya ya rafiki zangu wapendwa haikuwa taarifa yoyote. Hakukuwa na mpango wa kuitafisha toja ya kuchelewa kuwasili ndege. Hapa pia nisiambiwe kuwa Mwenyekiti alikataza, kwasababu alipaswa kuambiwa “Mzee tulia, siasa haiku hivyo”. Kama hakukuataza basi mimi ninashangaaa rafiki zangu kuliweka pengo hilo wazi likatumiwa na wapinzani wao.

Uchokozi mwingine unaofanywa na wapinzani wa CCM ume,kuwa ukilenga kukifanya kizungumze au kuonyesha namna kilivyokuwa ‘kizito’ kukabiliana na wapinzani wake. Hapa pia nisiambiwe kuwa kuna mabadiliko ya mbinu, ikiwemo kukaa kimya (mabubu?).

Siku hizi imekuwa kawaida kusikia msemaji wa serikali tu akiitetea serikali ya CCM. Kwa upande wao chama cha mapinduzi wenyewe wamekaa kimya. Sasa sijui rafiki zangu hawa wanataka kuendesdha siasa za aina gani? Amini nawaambieni hata kama chama kitaendeshwa na watendaji wote wenye “Phd” lakini suala lka kutokukisemea chama ni udhaifu. Kukiacha chama kijibiwe na msemaji wa serikali si aswa.

Kimsingi ni udhaifu au uzembe kwa chama cha mapinduzi kutegemea kusemewa na kutetewa na msemaji wa serikali (bila kujali kama chama cha mapinduzi ni tawala). Chama ni lazima kijisemee chenyewe kama ilivyokuwa ada.

Nikisikia CCM mpya huwa nashangaa sasna, kinashindwa hata kujibu ‘matamko ya kisiasa’ ya washindani wake. Hapa mtu asiniambie kuwa wamebanwa na majukumu ya kutekeleza ilani. Kwasababu ili itekelezwe ni lazima kuwe na mgawanyo wa majukumu ambayo chama chenyewe kinapaswa kuyafanya.

Leo naomba niwaulize rafiki zangu hivi mnaponiambia juu ya CCM mpya mna maanisha nini hasa au mnataka kuendelea kuwa mabubu hivi? Imekuwaje chama chenu kifikie hatua ya kudhani “kupuuzia” matamko ya kisiasa siyo siasa? Makabiliano ya kisiasa ni pamoja na kujibu mapigo ya kisiasa dhidi ya washindani wenu. Asinidanganye mtu kuwa eti “Hapa Kazi tu” kwasababu msingi wa siasa haupo hivyo. Huo mwongozo wa CCM mpya napenda kukumbusheni kuwa kumtegemea msemaji wa serikali wakati mambo mengine anayoyasemea ni yenu wenyewe ni uzembe au udhaifu katikati ya muongozo wa ‘CCM Mpya”. Labda niambieni kama mmekuwa ‘mabubu’.

Kwahiyo chama kinaseti ajenda ambayo inazungumzwa na kuwa mjadala zaidi huku kukiwa kinapanga kufanya mambo mengine yatakayokuwa ajenda. Lakini hayo yote siku hizi kwenye chama cha mapinduzi yamekauka. Siwezi kuhitimisha kuwa wameishiwa makali lakini hali hiyo imeshangaza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.