Hizi ni dalili kuwa Serie A imefufuka?

Rai - - MBELE - MWANDISHI WETU NA MITANDAO

wagumu1 NI misimu michache tu iliyopita Ligi Kuu Italia (Serie A) ilikuwa ikitajwa ni ya mabeki kupitika. Juventus-ikaja kutikisa sana, ikabeba sana mataji ya Serie A, lakini sasa hivi vita ni ya wote. Kipindi fulani ilionekana kama ni ‘tusi’ kusema Serie A ni ligi ya tatu kwa ubora wa soka barani Ulaya lakini ukweli ni kwamba ligi hiyo ni bora mno. Mara 12 imetoa timu zilizocheza fainali za michuano ya Ulaya kati ya 1983 na 1998

NI misimu michache tu iliyopita Ligi Kuu Italia (Serie A) ilikuwa ikitajwa ni ya mabeki wagumu kupitika. Juventus-ikaja kutikisa sana, ikabeba sana mataji ya Serie A, lakini sasa hivi vita ni ya wote.

Kipindi fulani ilionekana kama ni ‘tusi’ kusema Serie A ni ligi ya tatu kwa ubora wa soka barani Ulaya lakini ukweli ni kwamba ligi hiyo ni bora mno. Mara 12 imetoa timu zilizocheza fainali za michuano ya Ulaya kati ya 1983 na 1998 (timu zilizotikisa).

Ubora uliokuwa unazungumziwa hapa labda ni kwenye masuala ya kifedha. Kiuchumi. Hapa kweli Italia waliangushwa sana na kutokuwa na dili nzuri za mikataba ya TV na wamiliki mabilionea. Hilo lipo Ligi Kuu England kwa sasa. Timu za England zinalipa mishahara mikubwa ambayo hakuna mmiliki wa klabu yoyote ya Italia mwenye uwezo wa kujitutumua na kutoa.

Upande mwingine, Barcelona na Real Madrid nazo zikatumia vizuri sana michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kujijengea majina yao duniani huku zile timu za Serie A zilizokuwa zikijiweza kiuchumi, zikihangaika na ile skendo ya upangaji matokeo ya Calciopoli na kujikuta hata Bundesliga nao wakikwea juu yao katika ubora barani Ulaya.

Baada ya misimu sita ya Juve kutesa Serie A, sasa kiti chao cha ufalme huenda kikachukuliwa na Napoli ambao wameshinda mechi zote saba za awali na kuwa na wastani mzuri sana wa mabao (angalau bao tatu kila mechi).

Zamani wachezaji vijana walikuwa hawana hamu ya kwenda Serie A. Siku hizi kila kijana anajisikia furaha kusakata soka na kufunga mabao. Na kuweka rekodi.

Hivi majuzi, kinda Pietro Pellegri, aliyezaliwa 2001, aliandika rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kucheza mechi ya Serie A, na pia aliweka rekodi ya kufunga mabao mawili akiwa na umri mdogo zaidi dhidi ya Lazio.

Mwingine alikuwa ni Federico Chiesa mwenye umri wa miaka 19, ambaye anakumbushia ‘mavituz’ ya baba yake, Enrico, katika klabu ya Fiorentina, huku Milan, ambao baada ya kutumia zaidi ya euro milioni 200 kwenye usajili mwaka huu, wameanza mechi zao na mlinda mlango mdogo mno, Gianluigi Donnarumma, na straka kinda, Patrick Cutrone.

Licha ya kwamba mwanzo wa Milan umekuwa ni mgumu, lakini ile ari ya kufanya vizuri, wakiwa sambamba na majirani zao, Inter, imeamsha shauku ya mashabiki kwa mara nyingine.

Kwa kuzingatia neno ‘shauku’, katika mchezo wa kufuzu Ligi ya Europa miezi michache iliyopita, Milan walishuhudia mashabiki 65,673 wakiingia San Siro kuwatazama wakivaana na Craiova.

Wiki chache zilizofuata, mashabiki 51,752 walitinga dimbani kuwatazama Inter wakiitandika Fiorentina kwenye mechi ya Serie A,

idadi kubwa

ya mashabiki kuwahi kuingia kwenye uwanja huo katika mechi ya Oktoba tangu Nerazzurri hao watwae mataji matatu msimu wa 2009-10.

Wastani wa mashabiki wanaotazama mechi za Serie A uwanjani imeongezeka hadi zaidi ya mashabiki 1,500 kwa kila mechi kutoka msimu uliopita. Klabu za Milan zimechangia hilo, Napoli pia, na bila kusahau Atalanta, ambao wanaonesha tofauti kubwa siku hizi wakiwa na kikosi cha vijana hatari.

Ni wazi Serie A haijarudi kwenye ule ubora wa zamani wa ‘Sette Sorelle’ (wadada saba), kipindi kile Juventus, Milan, Inter, Fiorentina, Lazio, Roma na Parma walikuwa wakitajwa kama wanaowania taji.

Lakini utitiri wa mastaa unazidi kuongezeka Serie A, na kuzifanya timu nane au tisa kwa sasa ziwe na ushawishi wa kutajwa kwamba zinawania taji.

Upande wa wafungaji hatari. Dries Mertens ni kifaa kinachotikisa. Tangu kuanza kwa mwaka huu, Mertens ametupia mabao 24 na kutoa pasi 11 za mabao. Lakini klabu kama Lazio nayo ina Ciro Immobile ambaye mabao yake 13 msimu huu yamezidiwa na Lionel Messi pekee kati ya zile ligi tano kubwa za Ulaya.

Torino wana Andrea Belotti na Atalanta wana mashine ya mabao, Papu Gomez.

Serie A bado ina safari ndefu ya kuja kutambulika tena kama ni ligi bora duniani. Lakini kwa jinsi mabao yanavyofungwa sana. Rafu zikipungua kwa kasi siku hizi na wachezaji wenye vipaji safi wakizidi kuongezeka, ni dalili nzuri.

Wachezaji wa Napoli, ambao ni vinara wa Serie A, wakishangilia moja ya mabao yao msimu huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.