ANAYEKUFA» NI MTU FIKRA HAZIFI (3)

Rai - - MBELE -

Nimelazimika kuendelea na sehemu ya pili ya makala hii kutokana na maoni mengi niliyoyapokea kutoka kwa wasomaji wangu maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Nimeanza kuandika muda mrefu, nikili kuwa hakuna makala ambayo nimewahi kuandika na kupata mrejesho mkubwa kama makala niliyoandika katika toleo lililopita la gazeti hili.

Kazi ya fasihi inawahitaji watu wawili. Mtu wa kwanza ni mfasihi/ msanii na mtu wa pili ni hadhira au tunaweza sema ni mlengwa wa kazi ya fasihi husika. Namna nzuri ya kubaini kuwa kazi hiyo ya fasihi imewafikia walengwa kwa muktadha chanya ni mrejesho unaoupata kutoka kwa hadhira.

Siwezi kuwajibu na kuwanukuu wote walionipigia na kunitumia jumbe kunipongeza, kunikosoa na kutoa maoni yao. Wapo wengi na kufanya hivyo itachukua ukurasa mzima na pengine isitoshe. Itoshe tu kusema kuwa kama mwanafasihii lengo la kazi yangu ya fasihi kuwafikia hadhira limetimia.

Mmoja kati ya watoa maoni aliyenipigia simu na kuzungumza naye kirefu, alijitambulisha kuwa ni Padre wa kanisa katoliki katika kutoliki na ambaye aliomba nisilitaje jina lake. Maoni yake na maelezo aliyoyatoa wakati tukizungumza ndio sababu hasa iliyonifanya kuendelea na makala hii, Anayekufa ni mtu, fikra hazifi.

Msomaji huyo aliniachia swali. Swali lake lilikuwa ni kwa nini watu wenye fikra mbadala amabao wameonekana kuwa mwiba kwa watawala wamekuwa wakitweza au kuuwawa?

Binafsi swali hili limenifikirisha sana na nikaona ipo sababu ya mimi na wewe msomaji wangu tuufate ukweli na majibu mujarabu wa swali hili. Katika makala iliyopita nilitoa mifano michche ya watu na fikra zao ambazo kimsingi hazikufa ijapokuwa wao walikufa. Swali ni kwa nini fikra zao hazikufa na Kwa nini baadhi yao waliuwawa kwa kuwa tu walikuwa na fikra mbadala dhidi ya mifumo Fulani?.

Jibu ni kwamba viongozi wengi mahali pengi duniani hawataki kukosolewa. Wengi wao hujigeuza miungo watu na kamwe huwakubali mabadiliko na fikra za kimabadiliko. Huamini katika wao na vyama vyao. Wengi wao wanatoka katika vyama ambavyo kimsingi vimepoteza ushawishi kwa wanannchi na vimeshindwa kuleta mageuzi na ustawi wa maisha ya wananchi wao.

Ipo mifano mingi. Nchini Zimbambwe chini ya utawala wa Robert Mugambe nchi imebadilika. Zimbambwe inatajwa kuwa ni nchi yenye hali mbaya kiuchumia na maisha ya wananchi wake ni hoe hae kupindukia. Mtawawala wa nchi hiyo aliyeitawala tangu uhuru nchi hiyo ilipopata uhuru wake 1981 ameng’ang’ania madarakani licha ya kuchoka kiumri, kuchokwa kwa chama chake na wananchi kuchoka mfumo wake mzima wa utawala wa chama cha ZANU-PF.

Licha ya nchi hiyo kuwa na mfumo wa vyama vinggi vya siasa lakini vyama vya siasa havuifurukuti. Wanasiasa nguli wa upinzani nchini huo wamebanwa kisawasawa. Wale wote wanaotoa maoni na fikra mbadala ambazo hazimpendezi Mugabe wamekuwa wakikutana na mkono wa chuma na sheria kandamizi dhariri na zenye kutweza. Hii ni kwa upande wa Zimbambwe hali ambayo ipo hata sasa. Mugabe hataki kukubali kuwa nchi imemshinda na licha ya ukikongwe wake bado anatamani kuendelea kuwa mtawala wa nchi hiyo. Wananchi wa Zimbambwe wanamtazama Mugabe kama alama ya ufukara na ukamizaji wa kiutawala. Hawana la kufanya kwa kuwa wamebanwa na hawana njia ya kujinasua.

Nchini Unganda nako hali si shwari, Rais Yower Museven aliyeitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miongo mitatu angali amesalia madarakani. Katiba ya nchi hiyo ipo katika majaribio makubwa ya kubadilishwa ili impe haki ya kuendelea kuwania nafasi hiyo ya urais licha ya katiba iliyopo kutoa ukomo wa umri wa mika 75 kutogombea nafsi hiyo. Museven bado anaitaka Uganda. Museveni anaota kuendelea kuitawala Uganda pengine kwa mawazo yake mpaka kifo. Mbaya zaidi wakosoaji wake na wote wanaoonesha fikra mbadala kuinyume na utawala wake wanakiona cha mtema kuni. Nani asiyeyajua yanayowakuta viongozi wa vyama vya upinzani nchini humo hususani kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Kiiza Bisyege ambaye amekuwa akisukukwa sukwa na kutweza na vyombo vyo dola kwa kuwa tu amekuwa na fikra mbadala dhidi ya utawala wa Museveni na chama chake cha NRM?

Tunao mfano mwingine wa wazi uliomuhusu Mwandishi na mwanaharakati wa mazingira wa nchini Nigeria, marehemu Kenny Saro Wiwa. Utawala dhalimu wa diktekta Sana Abacha ulimuua Saro Wiwa kwa kuwa tu alikuwa na fikra mbadala na alitetea maslahi ya wanyonge wan chi hiyo waliokuwa wakikandamizwa kunyanyaswa kuonewa na kudhulumiwa na makampuni makubwa ya uchimbaji wa mafuta kutoka ulaya.

Jibu kwa nini wenye fikra mbadala hufa au kutweza linakwenda mbali zaidi. Zipo sababu nyingine nyingi za wanaharakati hao kutendewa ndivyo sababu hizo ni Uchu wa Madaraka na ubinafsi.

UCHU WA MADARAKA

Viongozi wengi barani Afrika wamejawa mno na uchu wa madaraka. Wao hutamani kutawala milele, Mifano ya Mugabe, Museven na wengine wengi ni michache katika mingi. Hawa kwa kuwa huwa na uchu wa kutawala kwa muda mrefu, hutumia nguvu nyingi kuwapunguza nguvu wapinzani wao wakihofu kuwa kama watawaacha huru fikra zao mbadala kuchanua huenda wakahatarisha nafasi zao za uongozi. Dhana ya demokrasia na kuruhusu maoni sambamba na kuachiana madaraka kwa njia ya amani imekuwa ni muhali kwa viongozi walio wengi.

UBINAFSI

Viongozi wengi wa ki-Afrika na mahali pengine wamekuwa ni wabinafsi kupindukia. Wao kwao uongozi ni njia ya kuchuma mali na kunyonya wanyonge. Hawa wapo tayari hata kuuza nchi zao au kuuza rasilimali za nchi kwa wageni ili tu waweze kujinufaisha wao na waatu wao wa karibu huku wakiacha jamii pana ikitaabika. Katika hali kama hiyo, hujiahidi kadri wawezavyo, kuhakikisha fikra za kimapinduzi dhidi ya tawala zao dhalimu hazipati nafasi. Hapa huwakandamiza wote wenye fikra mbadala.

Ubinafsi umekuwa ni chanzo kikuu si tu cha migogoro katika mataifa mbalimbali bali hata vyama vya siasa vinatumbukia katika shimo hilo. Tunaona hata hapa kwetu Tanzania vyama vya siasa vinasambaratika kila kukicha kwa sababu ya kutoruhusu fikra mbadala iwe ni za viongozi au wanachama ambazo zinaonekana kuhatarishi maslahi binafsi ya viongozi wakongwe.

Natoa shime kwa viongozi wa kiafrika na mahali pengine ulimwenguni, kuacha na kuruhusu ukosoaji juu ya namna wanavyotawala. Waruhusu na kuwaruhusu wenye maoni na fikra nzuri watoe maoni yao kwa uhuru ili kuweza kuifanyia dunia kuwa mahali salama pa kushi. Kuwatweza au kuwatendea kinyume walio na fikra mbadala ni kwenda kinyume na haki za biniadamu. Ikumbukwe kuwa ulimwengu huu tunapita tu. Kila kilichopo tutakiacha kama kilivyo. Yuko wapi Diktekta Mabutu Seseseko, Yuko wapi San Abacha na wengine?

Licha ya nchi hiyo kuwa na mfumo wa vyama vinggi vya siasa lakini vyama vya siasa havuifurukuti. Wanasiasa nguli wa upinzani nchini huo wamebanwa kisawasawa. Wale wote wanaotoa maoni na fikra mbadala ambazo hazimpendezi Mugabe wamekuwa wakikutana na mkono wa chuma na sheria kandamizi dhariri na zenye kutweza.

Kenny Saro Wiwa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.