Mubutu Seseseko alivyochangia DRC kuwa dampo la walanguzi wa kibepari (2)

Rai - - MAONI/KATUNI - NA MBWANA ALLYAMTU

Sehemu ya kwanza tuliangazia chimbuko la nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo pamoja na mambo mbalimbali tulidadavua kuhusu tamaduni na

Sehemu ya kwanza tuliangazia chimbuko la nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo pamoja na mambo mbalimbali tulidadavua kuhusu tamaduni na utawala wa nchini. Hata hivyo, mfululizo wa makala hizi umelenga kuchambua namna Rais wa pili wa nchi hiyo, Mobutu Seseseko, alivyochangia mauaji ya Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo, Patrice Lumumba. Pia jinsi alivyoigeuza Kongo kuwa jalala la mabepari. Endelea... MAISHA YA MOBUTU JESHINI

Mobutu alikutana na nidhamu katika maisha ya jeshini pamoja na mfano wa baba alivyokuwa Sagenti Joseph Bobozo kwake. Mobutu alifanya yote aliyotakiwa kufanya kwa nidhamu pia alianza kuazima magazeti kutoka kwa maofisa wa Kibelgiji na vitabu kila alikoweza na alipenda kusoma kila alipopata nafasi. Katika vitu alivyopenda kusoma ni mada za Rais wa Ufaransa wa wakati huo, Rais Charles de Gaulle, Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchil na mwana philosopha Muitaliano Niccolo Machiavelli.

Baada ya kumaliza na kufaulu masomo yake ya uhasibu, alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Bado alikuwa na hasira na mapadre wa shule waliompa adhabu ya kwenda jeshini, aliamua kuwa hataoa kanisani. Mchango wake katika harusi ulikua sanduku la bia, hii ndio mshahara wake ulichomudu.

Akiwa askari, Mobutu aliandika kwa kutumia jina bandia mambo yanayoendelea katika siasa katika gazeti jipya lililoanzishwa na wakoloni wa Kibelgiji Actulites Africaines. Mnamo mwaka 1965, aliacha jeshi na kuwa mwandishi wa habari, akiliandikia gazeti la Leopoldiville daily L’Avenier. Miaka miwili baadaye alikwenda Ubelgiji kuchukua habari juu ya 1958 World Exposition, alibakia huko kupata mafunzo ya uandishi wa habari. Muda huu Mobutu alishakutana na vijana wengi wa Kikongo wasomi ambao walipinga utawala wa kikoloni. Alianza urafiki na Patrice Lumumba na alijiunga na Chama cha Lumumba cha Movement National Congolais (MNC). Mobutu hatimaye alikuwa msaidizi maalumu wa Lumumba ingawa watu walishaanza minong’ono kuwa Mobutu anafanya kazi na Shirika la Ujasusi la Ubelgiji.

Kipindi cha mwaka 1960 mazungumzo mjini Brussels juu ya Uhuru wa Congo yaliendelea, ubalozi wa Marekani ulihodhi mazungumzo ambayo yaliazimia kupata picha kamili ya uwakilishi wa Congo. Wafanyakazi kila mmoja walikabidhiwa majina ya wageni wa kuwapokea na kuongea nao, balozi aligundua jina moja linajirudia, lakini hakuwa kwenye orodha kwakuwa hakua mmoja wa wageni, alikuwa katibu wa Lumumba. Lakini kila mtu alikubali kuwa mtu huyu alikuwa na akili sana, bado kijana lakini atafika mbali.

MVUTANO WA KONGO BAADA YA UHURU 1960

Kufuatia ahadi ya Uhuru hapo Juni 30, 1960, Serikali ya mseto iliundwa, iliongozwa na Waziri Mkuu, Patrice Lumumba na Rais Joseph KasaVubu. Taifa jipya haraka lilianza kuona matatizo wakati jeshi lilipoanza kukaidi maofisa wa jeshi wa Kibelgiji. Lumumba alimpa cheo Mobutu kama Katibu Mkuu Kiongozi wa Jeshi la Wananchi wa Congo na Victor Lundula alikuwa Mkuu wa Majeshi. Katika nafasi hiyo Mobutu alitembea nchi nzima kuhimiza wanajeshi warudi kambini. Jitihada zilifanywa na Serikali ya Ubelgiji kulinda mashimo ya madini ya Kusini mwa Congo walileta Jeshi la Umoja wa Mataifa.

Akiwa na wasiwasi kuhusu uwepo wa majeshi ya Umoja wa Mataifa si kwa kutuliza amani bali ni kwa lengo la kuligawa Taifa, Lumumba aliwaendea Umoja wa Soviet (USSR) kwa msaada, alipewa msaada mkubwa wa silaha na askari wa Kisoviet kama 1,000 kwa msaada wa kiufundi kwa wiki sita. Serikali ya Marekani iliona jitihada za Umoja wa Soviet ni njia ya kueneza ujamaa

Mobutu alimlaumu Lumumba kwa kutafuta huruma ya Umoja wa Soviet, sasa wamejenga mgongano na Wamarekani, Lumumba aliamua kwenda Staneyville ambako alipanga Serikali yake.

Afrika ya kati. KasaVubu alihamasishwa na Wamarekani na Wabelgiji kuanzisha mpango wa kuchukua madaraka kijeshi na kumuondoa Lumumba. Lumumba alipogundua hilo haraka alimtoa KasaVumba madarakani. Wote wawili Lumumba na KasaVubu walimpa maelekezo Mobutu ya kumweka ndani mwenzake. Akiwa Katibu Mkuu wa Majeshi, Mobutu alikuwa katikati ya msukumo kutoka sehemu mbalimbali. Balozi za Magharibi ambazo zililipa mishahara ya askari, pia Kasa-Vuba na wanajeshi wa chini hawakupenda uwepo wa majeshi ya Umoja wa Soviet.

Mobutu alimlaumu Lumumba kwa kutafuta huruma ya Umoja wa Soviet, sasa wamejenga mgongano na Wamarekani, Lumumba aliamua kwenda Staneyville ambako alipanga Serikali yake. Umoja wa Soviet tena walimpatia msaada wa silaha na aliweza kupigania nafasi yake. Baadaye mwaka 1960, Lumumba alikamatwa na kupelekwa Katanga. Mobutu bado alimuona Lumumba ni tishio kwahiyo aliamrisha akamatwe na apigwe hadharani hiyo ilikuwa Januari 17, 1961. Baada ya hapo alitoweka kwenye macho ya watu na hakusikika tena. Baadaye ilifahamika aliuawa siku ile ile na majeshi maalumu ya Moise Tshombe baada ya kuigeuka Serikali ya Mobutu na mabishano na Wabelgiji. Wamarekani walimuona Lumumba ni kiongozi hatari na masilahi yao yangekuwa hatarini kama angebaki madarakani.

Januari 23, 1961 KasaVubu alimpandisha cheo Mobutu kuwa Mkuu wa Majeshi, De Witte anasema hii ilikuwa ni kwa sababu za kisiasa zaidi kwa nia ya kulipa jeshi nguvu kubwa zaidi, alikuwa mtu ambaye rais alimwamini zaidi pia umuhimu wake katika jeshi. Mwaka 1964 Pierre Mulele aliongoza wafuasi wa vyama vingine katika mapinduzi. Kwa haraka walishikilia 2/3 ya eneo la Congo lakini Jeshi la Congo likiongozwa na Mobutu waliweza kuchukua eneo lililotekwa lote ilipofika 1965.

Mwandishi wa makala haya ni msomaji wa RAI na mchambuzi wa masuala ya kidiplomasia. Anapatikana kwa simu namba +255679555526 na DRC +243 977 860 824.

Mubutu Seseseko (kushoto) akiwa na Nelson Mandela

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.