George Weah; Mwafrika pekee mwenye Ballon d’Or anayeitaka Ikulu Liberia

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

Rai - - MAKALA JAMOIKITOBA -

MPACHIKAJI mabao wa zamani wa timu ya kinyang’anyiro cha kuwania Urais wa nchi hiyo, akifuatiwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa awamu iliyopita, Joseph Boakai.

Weah mwenye umri wa miaka 51 na Boakai (72) wamewaacha mbali wagombea wengine katika kukiwania kiti cha Rais anayemaliza muda wake, mwanamama Ellen Johnson Sirleaf.

Matokeo hayo ya awali yalionesha kuwa staa Weah anaongoza akiwa na asilimia 39.2 ya kura milioni 1.2, huku Boakai akiwa na asilimia 29.6.

Hata hivyo, matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa na tume ifikapo Oktoba 25.

Weah, aliyewahi kuzichezea kwa mafanikio klabu za Monaco, PSG, AC Milan, Chelsea na Manchester City, alikuwa mgombea aliyempa wakati mgumu Sirleaf katika uchaguzi uliopita, kabla ya mwananama huyo kuingia ikulu.

Nje ya siasa, moja kati ya kumbukumbu nzuri alizoziacha nyota huyo katika ulimwengu wa soka ni kuwa Mwafrika wa kwanza na pekee kufanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or, akifanya hivyo mwaka 1995 akiwa na AC Milan ya nchini Italia.

Makala haya yameichambua kwa ufupi safari ya mafanikio ya soka ya mshambuliaji huyo ambaye kama atashinda uchaguzi huo, basi ataweka rekodi nyingine, kwani atakuwa mchezaji wa kwanza kuwa rais wa nchi.

Baada ya kung’ara na timu za nyumbani kwao Liberia, jina la Weah lilitua Ulaya mwaka 1988, aliposajiliwa na Monaco ya Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’iliyokuwa ikinolewa na kocha wa sasa wa Arsenal, Arsene Wenger.

Akiwa na timu hiyo, Weah alifanya vizuri na hata kuinyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 1989, ikiwa ni tuzo yake ya kwanza kubwa tangu alipoanza kucheza kandanda.

Mchango wake wa mabao uliiwezesha Monaco kutwaa Kombe la Ligi na kufika nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1992, akipasia nyavu mara mbili katika mechi tisa za michuano hiyo, ambayo kwa kipindi hicho ilifahamika kwa jina la Kombe la Washindi.

Mafanikio hayo yalimfanya asajiliwe na PSG ambayo pia aliipa mafanikio makubwa yakiwamo mataji mawili ya Kombe la Ufaransa (1993 na 1995). Lakini pia, msimu wa 1994– 95 ulikuwa mzuri kwake kwani alitwaa kiatu cha mfungaji bora Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa amezipasia nyavu mara saba.

Makali yake hayo mbele ya walinda mlango yaliwavutia AC Milan waliomsajili mwaka 1995, klabu ambayo ilimuwezesha kutwaa Ballon d’Or na kuwa Mwafrika pekee kuwahi kuipata hadi leo hii.

Kuipata tuzo hiyo haikuwa rahisi kwani ilikuwa baada ya kushinda taji la Serie A mwaka 1996, kipindi ambacho Milan ilikuwa chini ya kocha Fabio Capello. Lakini pia, Weah aliibua kuwa mfungaji bora wa kikosi hicho kilichokuwa na mastaa wengi akiwamo Muitalia Roberto Baggio.

Mwaka 2000, Weah alikuwa Ligi Kuu England alikokuwa anaichezea Chelsea kwa mkopo akitokea Milan. Mashabiki wa Blues watamkumbuka kwa bao la ushindi dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo wake wa kwanza akiwa na timu hiyo.

Katika safari ya ubingwa wa Kombe la FA katika msimu wa 1999-2000, alifunga mabao mawili likiwamo moja dhidi ya Liverpool.

Baadaye, aliibukia Manchester City akiwa mchezaji huru na kusaini mkataba wa miaka miwili, akilipwa Pauni 30,000 kwa wiki.

Kabla ya kuondoka Man City kwa madai ya kukorofishana na kocha Joe Royle, Weah alikuwa ameichezea timu hiyo mechi 11 na kufunga mabao manne.

Staa huyo alirejea Ufaransa alikoanzia soka lake na safari hii alijiunga na Marseille aliyodumu nayo hadi mwaka 2001 kabla ya kutimkia Falme za Kiarabu kujiunga na klabu ya Al-Jazira.

Mwaka 2013, akiwa na umri wa miaka 37, baba huyo wa watoto watatu aliwatangazia waandishi wa habari kuwa amefikia uamuzi wa kuachana na mchezo wa kandanda.

Weah, ambaye alianza kugombea kiti cha Urais wa Liberia mwaka 2005, ambapo aliambulia asilimia 40.6 pekee ya kura huku mwanamama Sirleaf akishinda kwa asilimia 59.4, anaungana na wanasoka Roman Pavlyuchenko, Andrey Arshavin na Romario, ambao baada ya kustaafu soka waligeukia ulingo wa siasa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.