Shigela awaandalia vinono wageni

Rai - - MAKALA - SUSAN UHINGA,TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela ni miongoni mwa viongozi

hodari na shupavu ndani na nje ya Serikali.

Kiongozi huyu anayo historia ya kipekee, historia iliyojaa ushupavu na uhodari katika kuamua na kutenda. Wanaomjua wanamfananisha kiongozi huyu na jeshi la mtu mmoja.

Ukweli wa jambo hilo unadhihirishwa na jitihada zake kadha wa kadha anazozifanya katika kuimarisha usalama wa mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, lakini pia yuko mstari wa mbele kuhakikisha anahuiosha uchumi wa Tanga.

Kushughulika na mambo haya mawili si jambo dogo na ukweli ni kwamba haliwezi kufanywa na mtu dhaifu asiye na malenzo na mtazamo chanya katika majukumu yake.

Kwa ujumla ndani ya Tanga sasa hivi hali ya kiusalama iko imara na hilo ndilo limekuwa chachu ya kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda.

Shigela amejitahidi kuweka mambo sawa kwenye eneo la usalama hatua hiyo imemsukuma kuangalia ni namna gani atahakikisha ujio wa bomba la mafuta ghafi unakuwa na tija kwa jamii ya Tanga na Tanzania kwa ujumla.

Katika mazungumzo yake na RAI yaliyofanyika juzi jijini hapa, Shigela ameeleza namana ambavyo mkoa wake umejidhatiti katika kupokea wageni wote watakaokukuja kwa ajili ya shughuli mbalimbali zinazohusu mradi huo.

Kutokana na ukubwa wa mradi huo Shigela alisema mkoa unatarajia kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, hivyo wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wageni hao wanafurahia maisha ya Tanga na kufanya kazi zao kwa amani na utulivu wa hali ya juu.

MIUNDOMBINU

Shigela aliema katika suala la miundombinu ya barabara Mkoa unazo barabara nzuri zinazopitika kwa urahisi kwenye maeneo yote na katika kipindi chote cha mwaka .“Barabara zetu zinapitika na zinaunganisha wilaya zetu hivyo hata wakulima wetu wanaweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi pasipo bugudha yoyote.’’

HUDUMA ZA AFYA

Kwa upande wa Afya alisema Hospitali ya rufaa ya Bombo ipo imara kwa maana ya matabibu ya uhakika pamoja na vifaa tiba vya kutosha,huku miundombinu ya hospitali hiyo ikionekana kuboreswa siku hadi siku.

“Vituo vya afya pia vimeboreshwa ili kuweza kupunguza msongamano wa hospitali ya Rufaa Bombo, tuna matabibu pamoja vifaa tiba vya kutosha, hivyo wakazi wa Tanga pamoja na wageni kamwe wasiwe na wasiwasi kwa sababu tyunao uwezo wa kuwahudumia.”

NISHATI YA UMEME

Kuhusu upatikananji wa huduma ya nishati ya umeme, Shigela alisema tayari wameshafanya mazungumzo na uongozi wa wizara ya Nishati kuona ni namna Mkoa utajidhatiti katika suala hilo ili kuepukana na kutokuwa na umeme wa uhakika.

Alisema kwa kuzingatia ujio wa viwanda vikubwa pamoja na mradi mkubwa wa bomba la mafuta ambao kimsingi utahitaji umeme wa kutosha ili kuweza kukishi mahitaji, mkoa umejipanga ili kwenda na kasi ya mahitaji ya umeme.

“Tayari tumekwishafanya mazungumzo na viongozi mbalimbali hasa wa Tanesco, lengo likiwa ni kuona mkoa unakuwa na umeme wa uhakika kwani kama tunavyoona sasa Tanga inakaribisha wawekezaji wa viwanda.”

MAJI SAFI NA SALAMA

Kuhusu uhakika wa upatikanaji maji safi na salama alisema mkoa umeshaanzisha jitihada za kupata maji ya kutosha na salama na tayari jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda kwani mkoa unazalisha maji ya kutoshela mahitaji.

Alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni kuharibiwa kwa vyanzo vya maji jambo ambalo ameapa kuwashughulikia watu wote wanaojihusiha na uharibifu huo.

“Mkoa wetu unaendelea kufunguka hivyo fursa zilizopo lazima ziendane na huduma nzuri, sasa sitamvumilia atakaethubutu kufanya hujuma yoyote ya kukwamisha juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.”

BANDARI YA TANGA

Alisema tayari timu ya wataalamu imeshafika Tanga ili kuangalia namna ambavyo Bandari hiyo itaongezwa kina kwa ajili ya kuweza kupokea meli zitakazokuwa zinashusha shehena za mabomba ya kusafirisha mafuta.

“Na hili ni utekelezaji wa agizo la Rais, aliagiza wakati alipokuja katika ziara yake pamoja na uzinduzi wa mradi wa bomba la mafuta, aliagiza kuboreshwa kwa bandari ili iweze kuhudumia shehena zote zitakazotua kwenye bandari hiyo.”

Alibainisha kuwa agizo jingine ambalo limetolewa na Rais Mgufuli ni pamoja na ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Tanga.

Kuhusu huduma nyingine Shigela amewataka wamiliki wa nyumba za

kulala wa geni pamoja na watoa huduma mbalimbali kuhakikisha wanaboresha huduma hizo ili kuweza kuwavutia wageni wanaokuja. Pia amewataka wazazi kuwasomesha watoto na kuhakikisha wanasimamia vema maendeleo ya watoto wao kwa kushirikiana na walimu ili waweze kuandaliwa kupokea mabadiliko makubwa ya kiuchumi mkoani hapa.

--

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.