Rafiki yako kwenye siasa ndio adui yako kesho

Rai - - MAKALA - Comred Malipanga Daniel

SAMSON Mwigamba aliejivua uanachama ACT amejiunga rasmi na CCM.

My Take ikumbukwe Mwigamba ndiye yule alievuliwa uanachama kipindi kile na wakina Zitto wakati walikuwa wanatumiwa na CCM kukiharibu chama mafahari hawawezi kukaa zizi moja wasaliti wanasalitiana.

Dhambi ya unafiki inawatafuna hamna anaemuamini mwenzake Mwigamba, Zitto hawakutaka kuingia CCM moja kwa moja wakaamua kuanzisha ACT kama mwamvuli wa kuingia CCM baadae Kitila, Mghwira na mwigamba wameenda nakumuachia Zito ACT walioianzisha wao.

Sidhani kama Zitto anaweza kwenda CCM mbeleni ingekuwa CCM ya Jakaya naamini angekuwa amejiunga muda mrefu sababu ndio walio mrubuni. Sasa ni muda wa Zitto kuijenga ACT mpya aache wanafiki waende kwanza na abaki atengeneze chama chenye ushindani mkubwa wa siasa za Tanzania vile vile sitashangaa Zitto akihamia CCM 2020. Siasa hazina adui wala rafiki wa kudumu.

Zitto Kabwe akihutubia wananchi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.