Bobi Wine ‘amtikisa’ Yoweri Museveni

Rai - - MAKALA - NA BALINAGWE MWAMBUNGU/MITANDAO

Kwa zaidi ya wiki tatu hivi zilizopita, Afrika Mashariki na dunia nzima, ilizizima na kushuhudia vitendo vya kusikitisha, kama sio kutisha, na kuwabughudhi wanahabari wakiwa wanatimiza wajibu wao nchini Uganda.

Kipindi hicho dunia imeshuhudia wanahabari wakitishwa, kushambuliwa na kuumizwa katika kile kinachoonekama kuwa ni kampeni endelevu ya vyombo vya usalama nchini Uganda dhidi ya sauti huru, lengo lake likiwa ni kuwanyamazisha wapinzani na kufinya uhuru wa vyombo vya habari.

Kwa mara ya kwanza Wabunge vijana wa Kenya wamepaza sauti zao na kutishia kwenda Kampala, Uganda kuongoza maandamano ya kutaka Robert Kyagulanyi, aka Boi Wine, Mbunge wa Kyadondo Mashariki, achiwe huru.

Wakiongozwa na Jared Okelo, Mbunge wa Nyando, Babu Owino (Embakasi Mashariki, na Gideon Keter (Mteule) wa Chama cha Wabunge Vijana (Kenya Young Parliamentarians Association), walisema kwanza wataandamana kwenda Ubalozi wa Uganda nchini Kenya, kabla ya kuyakoleza nchini Uganda.

Pia wasanii maarfu wa kimataifa 100, akiwamo Angelique Kidjo na Chris Martini, wamelaani kitendo cha kikatili dhidi ya msanii yota wa Uganda Bobi Wine na kuitaka familia ya mataifa yenye heshima (decent nations), yasikae kimya wanahabari wanapofanyiwa vitendo kama hivyo.

Wameitaka serikali ya Uganda kuacha mara moja kuwashambulia na kuwabughudhi wanahabari na kuomba Umoja wa Afrika (AU), Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na marafiki wa demokrasia duniani, kutimiza wajibu wao kusisitiza umuhimu wa uhuru wa mawazo kwa wananchi wa Uganda.

Afrika Mashariki ilishitushwa na vitendo vya kutisha na matumizi ya nguvu kubwa ya kijeshi iliyotumika kuwadhibiti wananchi wa Uganda Kaskazini na baadaye kuwashambulia wanahabari mjini Kampala, wakiwa katika kutimiza wajibu wao.

Hii imeifungua macho jamii nzima ya wapenda haki na amani katika Jumuia ya Afrika Mashariki na kwingineko barani Afrika—kwamba viongozi walio madarakani, hawataki kukosolewa wala kunyoshewa kidole—hata pale wanapofanya vibaya.

Bobi Wine alikamatwa kama mhalifu—jambazi na kupewa kisago cha mbwa mwizi. Kama hilo halikutosha, akapelekwa kwenye kambi ya kijeshi— Makyinde Nilitary Barracks ambako wanaokumbuka enzi za utawala wa dikteta Jenerali Iddi Amin, jina la Makyinde likitajwa, damu yao ililikuwa inazizima kwa hofu—mtu akipelekwa Makindye ilikuwa sawa na kifo.

Kitendo cha hovyo na uonevu wa kidola usioelezeka— ambao haukuwahi kutokea hata wakati wa utawala katili wa Iddi Amin, unaitaka jumuia ya kimataifa sasa kuingilia kati masuala ya watawala wenye nia ovu ya kutaka kunyamazisha sauti huru kwa kuwatesa, kuwajeruhi na hata kuwaua, au kuwatupa gerezani wananchi wanao wakosoa.

Iddi Amin aliponyakua madaraka Uganda, Yoweri Kaguta Museveni alikuwa bado ni mwanaharakati wa kisiasa na alikuwa akiishi Tanzania. Baada ya kurejea Uganda, alishiriki katika serikali ya umoja na baadaye, yeye na kundi ambalo halikupenda kuona wananchi wa Uganda waendelee kuburuzwa, kukandamizwa na kudhulumiwa haki zao, akaingia mstuni. Baada ya vita na jeshi la Uganda, akatwaa madaraka kupitia jeshi la mstuni la NRA—National Resistance Army mwaka 1986.

Ili kujihalalisha kuendelea kutawala, NRA baadaye wakajivua magwanda ya kijeshi, na kuvaa suti za kiraia. Wakabadilisha jina na kujifanya chama cha siasa—National Resistance Movement (NRM)— jina ambalo haliakisi kwamba chini ya uongozi wa Rais Yoweri Museveni, ambaye mwanzoni alikinasibu kama mwanamapinduzi, demokrasia inaweza kujengeka nchini Uganda. NRM ni chama ambacho bado kina ‘resist’— kina pinga (?) demokrasia, kama kile chama kinacho waaminisha watu kwamba ni cha ‘Mapinduzi Daima’

Bob Wine alizaliwa 1982, miaka mine kabla Museveni hajaingia madarakani, ni mwanamuziki wa kizazi kipya. Yeye na vijana wenzake, hawakuujua utawala wa Iddi Amin wala wa Milton Obote, na hawaelewi kwa nini kwa kipindi chote hicho, mtu mmoja tu yuko madarakani! Wanataka mageuzi, walio madarakani wana-resist!

Bob Wine (36), aliwashtua watawala aliponyakua kiti cha Ubunge wa Kyadondo Mashariki kama mgombea huru—jambo ambalo Tanzania linawaogopesha watawala. Hata Christipher Mtikila (marehemu), alipowashindwa mahakamani, wakauzunguka uwamuzi wa Mahakama kwa kuingiza kifungu kwenye Katiba kinachotaka mgombea sharti atokane na chama cha siasa.

Bob Wine anahubiri injili ambayo inamtisha Rais Museveni—vijana vaeni ujasiri tumwondoe madarakani— injili kama ile ya ‘Arab Spring’ iliyozitikisa nchi za Afrika Kaskazini miaka ya hivi karibuni.

Bob Wine pamoja na Wabunge wengine 30, walishambuliwa na kupigwa walipokuwa katika kampeni za uchaguzi wa marudio mjini Arua. Rais Museveni alikuwa anampigia kampeni mgombea wa NRM. Museveni alijionea mwenyewe kwamba wananchi wa Arua, walikuwa hawamtaki, yeye na chama chake. Arua wamemuaibisha Rais Museveni kwa kumkataa mgombea wa NRM.

Labda ni kutokana na hofu hiyo, Museveni akaona amkomoe Bobi Wine. Akatumia jeshi badala ya polisi, kuzusha tafrani ili akikamatwa ahukumiwa kijeshi. Bob katika sio mwanajeshi—mjeshi akishitakiwa kwa uhaini, anaweza kuhukumiwa kifungo cha muda mrefu au kuuwawa kwa kupigwa risasi (firing squad).

Museveni amekwisha sahau kwamba alitenda uhaini alipoliongoza kundi lake la NRA kutwaa silaha na kuingia mstuni na baadaye kutwaa madaraka kwa nguvu. Bob Wine, hana jeshi, wala hajatangaza kuingia mstuni. Museveni ni kama anaogopa kivuli chake.

Ingawaje Museveni alitangaza kuondoa mashitaka na kuamuru Bob Wine aondolewe Makindye, alipelekwa Gulu kwenye mahakama ya kiraia ambako alisomewa mashitaka mapya ya kumiliki silaha ya kivita na kuingilia msafara wa Rais Museveni.

Makundi ya vijana jijini Kampala na Arua, na yale ya haki za binadamu na jumuia za wanahabari, zimelaani vitendo vya kuwashambulia wanahabari waliokuwa wanafuatilia ghasia za wafuasi wa Bobi Wine.

Haya ya Bob Wine, ni viashiria kwa tawala kandamizi kote Afrika—mwandishi wa Al Jazeera, Mahmoud Hussein wa Misri, kwa miaka miwili sasa, anashikiliwa kwa kosa la kuandika habari za uongo. Misri ni nchi ya tatu duniani kuwakamata na kuwafunga wanahabari.

Mwandishi Sitta Tumma wa Tanzania, alikamatwa na polisi na kushikiliwa kwa muda, kisa? Alikwenda Tarime, mkoani Mara kuripoti habari za kampeni, uchaguzi mdogo wa udiwani. Jones Abiri wa Nigeria, aliachiwa huru mwezi uliopita—baada ya kusota gerezani kwa tuhuma za kuunga mkono harakati za kijeshi na Samuel Ogundipe wa Nigeria pia, aliwekwa ndani, sababu alikataa kutaja vyanzo vya taarifa zake zilizokuwa zinawahusu polisi.

Hali ya hofu Matukio kama haya ni hatua za kuwadhoofisha wanahabari barani Afrika, wawe na hofu na washindwe kufanya kazi kwa utulivu. Mwenendo huu wa ukandamizaji wa uhuru wa habari, unajenga hofu pia miongoni mwa wananchi. Hata viongozi wandamizi, ambao wanatakiwa kukemea vitendo hivyo, nao wanaogopa.

Maofisa usalama waliwavamia na kuwapiga wandishi wa NTV, Herbert Zziwa na Ronald Muwanga walipokuwa wanatangaza ‘live’ kutoka mijini Arua, tukio la kupigwa risasi na kuuliwa Yasin Kawuma, dereva wa Bobi Wine. Wandishi hao wakafunguliwa mashitaka ya kuchochea vurugu na uharibifu wa mali.

Mwandishi wa Televisheni ya NBS, John Kibaliza, alikamatwa kwa nguvu na kupelekwa kusikojulikana. James Akena, mpiga picha wa shirika la Reuters, ambaye alikuwa anafuatilia maandamano ya ‘FreeBobWine’ jijini Kampala na Arua, alikamatwa na wanajeshi na kuzuiliwa kwa muda na kunyang’anywa vitendea kazi vyake.

Vitendo hivyo kunyang’anya wanahabari kamera, au kuwalazimisha kufuta taarifa zao kwenye kamera na simu, vimeendelea kushamiri katika nchi za Kiafrika. Polisi huwatisha wadishi kuwafungulia kesi ya uhalifu wa kimtandao.

Wandishi waliokuwa wanafuatilia tukio la la kupigwa na kuwekwa rumande kwa Wabunge Bobi Wine na Francis Zaake, walipokea vitisho na kuambiwa waache kuandika habari hizo la sivyo wawe tayari

Museveni amekwisha sahau kwamba alitenda uhaini alipoliongoza kundi lake la NRA kutwaa silaha na kuingia mstuni na baadaye kutwaa madaraka kwa nguvu. Bob Wine, hana jeshi, wala hajatangaza kuingia mstuni. Museveni ni kama anaogopa kivuli chake.Ingawaje Museveni alitangaza kuondoa mashitaka na kuamuru Bob Wine aondolewe Makindye, alipelekwa Gulu kwenye mahakama ya kiraia ambako alisomewa mashitaka mapya ya kumiliki silaha ya kivita na kuingilia msafara wa Rais Museveni.

kwa lolote.

Franklin Draku, mwandishi wa gazeti la Daily Mirror, alipigiwa simu akiwa nyumbani siku aliyo rejea kutoka Arua na kuambiwa akabidhi picha alizopiga Arua pamoja na za video zinazo husu tukio la Bobi Wine.

Anasimulia kwamba msichana aliyejitambulisha kwa jina la Zafra alimwambia kuwa wanajua alipo, na ‘tutakupata’. Baada ya dakika chache, akaanza kusikia usingizi mzito. Anasema akiwa katika hali hiyo, alimwona mwamke aliyekuwa amevalia gauni fupi jeupe, akifungua mlango na kuwasha taa.

Anasema mwanamke huyo, alikwenda moja kwa moja kwenye begi lake na kuanza kupakua kilakitu. Hakuwaweza kunyanyuka au kusema lolote na akapoteza fahamu. Hofu?

Anasema alizinduka kesho yake saa 11 afajiri. Kamera yake aina ya Nikon, kompyuta mpakato aina ya Dell, I-pad, Tecno tab na pawa banki, kitambulisho, simu na chaja za ‘laptop’ na Shs373,000 taslimu, vilikwisha chukuliwa.

Derrick Wandera, wa gazeti la ‘Daily Monitor, ambaye alihudhuria mkutano wa wanafamilia ya Bobi Wine na wanahabari, kuzungumzia kukamatwa kwa Mbunge huyo, alipokea simu ya kumtisha.

“Tunajua wewe ni kijana mdogo hujafikisha hata miaka 26, na unajiingiza katika masuala mazito ya nchi. Tafadhali acha kuandika habari za Bobi Wine. Tunakuangalia. Bado ni mapema sana kwako kufa,” anasimulia Derrick.

Wandishi wa habari ni macho na masikio ya umma, wanatishwa ili wasiripoti mabaya yanayotokea kwenye nyanja za kisiasa. Serikali za Kiafrika, ambazo katiba zao zinatoa uhuru wa habari, na zimesaini mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamu, hazizingatii matakwa ya mikataba hiyo.

Ukiwanyamazisha wanahabari, umeikatili jamii. Uhuru wa kutoa maoni ukifinywa (curtailed), aina nyingine zote za uhuru, haziko salama na demokrasia inakuwa hatarini.

Wandishi walishambuliwa na na wanajeshi nyumbani kwa mpinzani mkuu wa Museveni, Dk. Kiiza Besigye. Jeshi la Uganda baadaye likaomba radhi kwamba wanajeshi wake walikiuka maadili ya kazi yao. Ni kawaida kwa serikali zinazowaogopa wananchi, kuwavika wanajeshi sare za polisi kuwatisha. Wanajeshi hawajasomea mambo ya uraia ndio maana hutumia nguvu hata ambapo haihitajiki.

Jacob Oulanyah, Naibu Spika wa Bunge la Uganda, alimtembelea Bobi Wine akiwa Makindye, mahali pengine Wabunge na viongozi wa Bunge, hawathubutu kumtembelea Mbunge kutoka upinzani akiwa mgonjwa au gerezani. Hofu!

Wabunge vijana wa Kenya pekee ndio walivaa ujasiri. Waliitisha mkutano na wandishi wa habari jijini Nairobi, na kutamka kwamba hawakupenda mambo aliyotendewa Bob Wine na yaliyokuwa yanajiri nchini Uganda.

Waliweka wazi kuwa kuminywa kwa haki sehemu moja (Uganda), ni kuminywa kwa haki kila mahali Afrika.

“Sisi kama Wabunge vijana, kazi yetu ni kulinda haki za binadamu,” walitamka na kutishia kwenda Kampala kuongoza maandamano.

Ni kawaida kwa watawala kuwafungulia kesi za kisiasa viongozi wa upinzani, ili kuwakomoa. Kiongozi mmoja alinukuliwa akisema: “Nitampiga mchungaji na kondoo wake watatawanyika.”

Museveni anadhani akimfunga Bobi Wine, wafuasi wake watatawanyika. Kukamatwa kwa Bobi Wine, pamoja na watu wengine 34, kuliunganishwa na kisingizio kwamba wapinzani waliitupia mawe gari ya Rais.

Usiku tarehe 18, Agosti, mwaka huu, kabla hajakamatwa Bobi, dreva wake inadaiwa alipigwa risasi na kuwawa na walinzi wa Museveni. Watu wengine wapatao 30, wakiwamo Wabunge na wanahabari, walikamatwa.

Bobi Wine ana wafuasi wengi vijana nchini Uganda

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.