Mwen ge wa uhuru umeacha kitanz i kwa wakurugenzi Simiyu

Rai - - MAKALA - NA DERICK MILTON, SIMIYU

Agosti 19, 2018 Mwenge wa Uhuru umehitimisha mbio zake katika Mkoa wa Simiyu ambapo ulikimbizwa katika halmashauri sita za Mkoa ambazo ni Meatu, Busega, Bariadi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi pamoja na Maswa.

Licha ya kuhitimisha mbio hizo, mambo siyo mazuri mpaka sasa kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa halmashauri husika kutokana na miradi yao kukataliwa kuzinduliwa na kuwekea jiwe la msingi.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi na watendaji walionekana kutoka kijasho wakati wakijibu maswali ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka huu, Charles Kibeho katika miradi ambayo aliitilia shaka.

Ukiwa katika Mkoa wa Simiyu, Mwenge huo ulitarajiwa kuzindua, kuweka mawe ya msingi pamoja na kutembelea miradi 36 yenye thamani ya Sh bilioni 8.4 kwenye halmashauri zote sita.

Hata hivyo, Kabeho alikataa kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika baadhi ya miradi kwenye halmashauri.

Halmashauri ambazo zilikataliwa baadhi ya miradi yake ni Meatu, Bariadi Mji, Busega pamoja na Maswa, ambapo sababu kubwa ya kukataliwa ni miradi hiyo kutoendana na thamani halisi ya fedha iliyotumika.

Umahiri wa kiongozi huyo wa kuuliza maswali ya kitaalamu hasa kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu ambayo aliitilia mashaka, ni mambo ambayo yaliwapa wakati mgumu baadhi ya viongozi kutoa majibu sahihi.

Mbali na hilo kiongozi huyo hakufurahishwa na kitendo cha baadhi ya watendaji na viongozi kwenye halmashauri kuudanganya mwenge pale alipobaini kuwa wamedanganya, ambapo baadhi aliwataka kujitathmini katika utendaji kazi wao.

Ni halmashauri mbili peke yake ambazo ni Itilima pamoja na halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, ambazo miradi yake yote ya ujenzi ilizinduliwa na kuwekewa mawe la msingi.

Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

Mwenge huo wa Uhuru ulianza mbizo zake katika halmashauri ya Wilaya hiyo ambako hali haikuwa nzuri kwa viongozi na watendaji wa halmashauri, kwani kati ya miradi yake mitatu ni mmoja tu ambao ulikubaliwa.

Katika mradi wa kwanza, ujenzi wa miundombinu katika hospitali wilaya, wodi ya wazazi, maabara, nyumba ya mtumishi, pamoja jengo la upasuaji ambapo majengo hayo yalikuwa yanawekewa jiwe la msingi.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Fabian Manoza, wakati akisoma taarifa mbele ya Kiongozi huyo kuhusu ujenzi huo, alisema kuwa majengo yote manne yametumia kiasi cha Sh milioni 450.

Licha ya Mkurugenzi huyo na Mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Joseph Chilongani kujitetea na kueleza gharama zilizotumika ni nafuu, Kiongozi huyo alisema katika wilaya nyingine wametumia kiasi hicho kujenga majengo zaidi ya sita.

Hata hivyo, Mwenge ukiwa katika eneo hilo, ilibainika kuwa kuna baadhi ya vifaa (saruji) viliibiwa na watuhumiwa kupelekwa mahakamani, lakini Kiongozi huyo alishangaa kupewa taarifa kuwa kesi ilifutwa na Mkurugenzi huku kukiwa hakuna na taarifa za kutosha.

“Inashangaza kabisa mwenye kesi ni Mkurugenzi, lakini mwenendo wa kesi hajui na hana taarifa kuwa kesi hiyo imefutwa baada ya upande wa mashtaka kukosa ushahidi, ni jambo la ajabu sana,” alisema Kabeho.

Mbali na kukataa kuweka jiwe la msingi kwenye majengo hayo, Kiongozi huyo aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi, huku akitaka wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Hali iliendelea kuwa mbaya zaidi kwa viongozi na watendaji wa halmashauri, baada ya kiongozi huyo kubaini kuwa moja ya mradi ambao ulitakiwa kutembelewa na Mwenge umeondolewa kinyemela kweye ratiba.

Mradi huo ni wa ufugaji ng’ombe wa kisasa, ambao unamilikiwa na halmashauri, ambao lengo lake ni kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa kiwanda cha maziwa cha meatu (Meatu milk).

Hata hivyo, Kiongozi huyo alitaka kupelekwa kwenye mradi huo, jambo lililotekelezwa ambapo alisema watendaji na viongozi wa wilaya hiyo waliuondoa kinyemela.

Baada ya kufika katika mradi huo, Kiongozi huyo alisikitishwa na hali ambazo ngo’mbe hao walionekana kukonda, huku akitaka majibu ya kwanini mradi huo uliondolewa kinyemela.

Mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Chilongani alikiri mradi huo kutolewa kwenye ratiba baada ya kubainika kuwa haufai kutembelewa na Mwenge wa Uhuru kutokana na ngo’mbe kuonekana wamekonda sana.

“Ni kweli mradi huu ulikuwemo kwenye ratiba na ulitakiwa kutembelewa na Mwenge lakini tulilazimika kuutoa kutokana na hali za Mifugo hawa kutoridhisha, wamekonda sana,” alisema Chilongani.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri wa halmashauri alisema tatizo kubwa la ngo’mbe hao kukonda ni uhaba wa nyasi ambao ulisababishwa na ukame.

“Tulikuwa na ukosefu wa Nyasi nzuri zenye maji, nyasi nyingi ambazo tunazo zimekauka, hivi karibuni tulilazimika kwenda kwenye Hifadhi Pori la Akiba Maswa kwa ajili ya kutafuta Nyasi wenye maji,” alisema Manoza.

Hata hivyo Kiongozi huyo hakukubalina na majibu ya Mkurugenzi huyo, ambapo alieleza Ngo’mbe hao wameshambuliwa na Minyoo hali ambayo imesababisha waweze kukonda.

“Yawezekana na hapa kuna mikono ya watu, wanapewa pesa kwa ajili ya kuhudumia mifugo hii wao wanakula, hizo sababu wala hazina msingi, hawa wanaonekana kabisa kuwa wana minyoo, lazima

Yawezekana na hapa kuna mikono ya watu, wanapewa pesa kwa ajili ya kuhudumia mifugo hii wao wanakula, hizo sababu wala hazina msingi, hawa wanaonekana kabisa kuwa wana minyoo, lazima watendaji wawajibike katika hili,” alisema Kibeho. Haikuishia hapo mambo yaliendelea kuwa mabaya, baada ya Kiongozi huyo kukataa kwa mara nyingine kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa mahakama ya mwanzo SangaItinje.

watendaji wawajibike katika hili,” lisema Kibeho.

Haikuishia hapo mambo aliendelea kuwa mabaya, baada a Kiongozi huyo kukataa kwa mara yingine kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa mahakama ya mwanzo SangaItinje.

Hatua ya kutoweka jiwe la Msingi kwenye jengo hilo, ni utokana na kukosekana kwa majibu sahihi ya gharama za ujenzi wa mradi huo, huku viongozi wa mahakama wakitafutwa kutoa maelezo hayo bila ya mafanikio.

Katika taarifa iliyosomwa mbele a kiongozi huyo juu ya gharama a ujenzi wa jengo hilo, ilielezwa utumia zaidi ya Sh milioni 109 kiwemo na nguvu za wananchi waliojenga hadi kufikia usawa wa uezeka.

“Jengo bado halijakamilika na mpaka sasa limetumia gharama

a Sh Milioni 109, naomba kupata maelezo ya gharama hizi, ni jinsi ani jengo halijakamilika ujezi wake akini limetumia kiasi kikubwa cha esa,” alihoji Kibeho.

Maswali ya Kiongozi huyo alionekana kuwa magumu kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi,

aada ya kueleza kuwa hawana majibu sahihi ya mchanganuo wa

harama hizo huku watendaji wa mahakama wakitafutwa bila ya mafanikio.

‘’Tumepewa taarifa kuwa wamekuja hapa asubuhi wakafungua milango ya jengo ili mwenge ufike kuwawekea jiwe a msingi, kisha wakakimbia, atuwezi kuweka jiwe la msingi wakati kuna ukakasi wa gharama juu ya fedha zilizotumika kwenye ujenzi huu, na hapa hakuna mwenye majibu sahihi’’ alisisitiza Kabeho.

Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi licha ya kumbembeleza kiongozi huyo aweke jiwe la msingi kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi kupatiwa huduma za kimahakama kwa karibuni bado jambo hilo lilishindikana.

Hatua ya kiongozi huyo kugoma kuweka jiwe la msingi kwenye jengo hilo ilionekana kuungwa mkono na wananchi wa Kijiji hicho walifika eneo hilo, kwa kushangilia mara baada ya kusikia amegoma kuweka jiwe la msingi.

“Tunampongeza Kiongozi huyu wa Mwenge kwa uamuzi wake, sisi wenyewe wananchi kila siku tunalalamika kuwa kuna matumizi mabaya ya pesa kwenye ujenzi huu, sisi tumefurahi sana sasa tunataka uchunguzi ufanyike,” alisema Mchama Marwa.

Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mwenge huo ukiwa katika halmashauriya Mji wa Bariadi, mambo yalianza kuwa magumu kwa watendaji na viongozi wa halmashauri hiyo baada ya kiongozi huyo kukataa kuzindua jengo la wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Jengo hilo lenye vyumba vitatu ambalo limejengwa katika shule ya Msingi Sima ‘A’ lilileta utata kwenye gharama za ujenzi wa vyoo matundu manne ambavyo vilidaiwa kutumia kiasi cha Shilingi Milioni 15.

Akiwa kwenye mradi huo Kiongozi huyo wa Mwenge alisema kuwa gharama zilizotumika kujenga matundu manne vya vyoo ni kubwa sana, hivyo alitaka kufanyika uchunguzi ya gharama hizo na kuwa hawezi kufungua jengo hilo.

Baada ya Mradi huo Kiongozi huyo alilazimika kutembelea duka la dawa kwenye hospitali ya teule ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu (Somanda), ambalo liko chini ya halmashauri, ambapo mambo yalikuwa magumu zaidi kwa viongozi na watendaji hao.

“Tulipata taarifa kuwa hili jengo lilizinduliwa na Mwenge mwaka jana, sasa leo nimeona mwenge uje kulitembelea na tulipata taarifa kuwa viongozi na watendaji mliudanganya Mwenge katika kuzindua duka hili,” alisema Kibeho…

“Watalaamu hawa walidanganya mwenge ili uweze kulizindua baada ya kuazima dawa kutoka uongozi wa hospitali, na mara baada ya mwenge kuondoka duka hili halijawahi kufanya kazi,” alieeza Kiongozi huyo wa Mwenge.

Kiongozi huyo alisema kuwa viongozi wa halmashauri hiyo licha ya kuudanganya mwenge mwaka jana, wameamua kudanganya tena kwa kile alichoeleza alipata taarifa kuwa duka limewekewa dawa hivi karibuni baada ya kusikia mwenge unakuja kwenye halmashauri hiyo.

Kabeho alisema Halmashauri ya mji wa Bariadi inawadanganya viongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, kuwa duka hilo lilikuwa likitumika, badala yake lilikuwa halifanyi kazi na halitoi huduma kwa wananchi hospitalini hapo.

“Hapa mmeegesha tu, inawezekana dawa mmetegeshea mwenge, tunafahamu na siku mliyoanza kutoa huduma, lakini tangu mmepanga dawa dukani juzi, hamjapata mteja hata mmoja,’’ alisema Kabeho.

Hata hivyo, kiongozi huyo aliutakauongoziwahalmashauri kumpatia risiti zinazoonyesha wapi wamenunua dawa, kumbukumbu za mauzo kwa wananchi, maswali ambayo yalikosa majibu kutoka Mkurugenzi wa halmashauri Merkzedeck Humbe na watalaamu wa Afya.

“Tumeomba risiti halali ya mauzo na kumbukumbu za kila siku za mauzo hamjatupatia, wala hazionekani, mmeagiza mtu azifuate ameenda kimoja, wakati mkijua serikali inasisitiza matumizi na utoaji wa risiti kuwa katika mfumo wa EFD’’ Alisema Kabeho.

Aliwataka viongozi wa wilaya na halmashauri kujitathimini kwa sababu wanaonekana kumdanganya Rais Magufuli kwa mara ya pili.

Halmashauri ya Busega na Maswa.

Hali iliendelea kubaki vile vile katika baadhi ya miradi ambayo Kiongozi huyo aliweza kutilia mashaka, kwa kutaa kuweka jiwe la msingi pamoja na kuizundua, ambapo katika Wilaya ya Busega aligoma kuzindua jengo la maabara.

Jengo hilo ambalo liko kwenye shule ya sekondari Masanza, chanzo cha kutozinduliwa ni kutofautiana kwa taarifa za gharama za halmashauri pamoja na Mkoa juu ya kiasi sahihi kilichotumika kujenga.

Hivyo hivyo, katika halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Kiongozi huyo aligoma kuzindua bweni la wanafunzi wa kiume katika shule ya sekondari Malampaka kwa madai kuwa gharama zilizotumika ni kubwa.

Mbali na hilo katika halmashauri ya Wilaya hiyo, alikataa kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana baada ya kueleza kuwa kuna ubaguzi katika kutoa mikopo kwa vikundi hivyo ikiwa pamoja na kuonekana vyote vinatoka Mjini.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge mwaka huu, aliwataka watendaji wa serikali na viongozi kuwajibika katika kuhakikisha wanamsaidia Rais kuweza kuwahudumia wananchi ambao wengi ni maskini.

Aliwataka watumishi wa serikali kutambua kuwa Mwenge wa Mwaka huu siyo wa kula chakula, chai, na Pilau bali ni Mwenge wa kufanya kazi na kuchukua hatua kwa watumishi ambao hawawajibiki.

“Mwenge huu siyo kama ule ambao ummezoa wa kula pilau, kucheza mziki na ngoma, au kukimbia kimbia, mwenge huu ni mwenge wa kazi, ni lazima watendaji kubadilika katika uwajibikaji,” alisema Kibeho.

Mkuu wa Mkoa

Agosti 20, 2018 akikabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka alimpongeza kiongozi huyo wa Mwenge kwa kazi ya kutembelea na kuweza kuonyesha mapungu katika baadhi ya miradi.

Mtaka alisema kuwa kama Mkoa utaweza kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo yaliyotolewa na Kiongozi huyo wa Mwenge ikiwa pamoja na kufanya marekebisho kwenye maeneo yote ambayo yalioneka kuna matatizo.

Katibu Tawala wa Mkoa (RAS)

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini alisema kuwa tayari amewaandikia barua wakurugenzi wote ambao maeneo yao Kiongozi wa Mwenge alikataa kuzindua au kuweka jiwe la msingi kwenye miradi yao.

Sagini alisema kuwa wakurugenzi hao wametakiwa kutoa maelezo juu ya kwanini miradi yao ilikatiliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge na wao wamechukua hatua gani kwenye maeneo yao.

Sagini alisema kuwa haiwezekani Mkoa wa Simiyu ikiwa na ajenda ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, huku baadhi ya watendaji wa serikali wanarudisha nyuma juhudi huzo za viongozi wa mkoa.

“Nimewaandikia barua za maelezo na kueleza ni kwa nini nisiishawishi mamlaka yao ya uteuzi, kuwaondoa katika nafasi zao kutokana na kushindwa kuwajibika katika miradi ya serikali,” alisema Sagini.

Hatua ambayo ameanza kuchukua katibu tawala huyo inaonyesha kuwa viti havikaliki kwa wakurugenzi na watendaji wa halmashauri kutokana na miradi yao kuonekana kuwa na mapungufu makubwa wakati wa mbio za Mwenge.

Mkuu wa mkoa wa Singida (kushoto) Dk, Reheme Nchimbi akimkabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Simyu, Anthony Mtaka. Picha Derick Millton

Kibeho akizindua moja ya miradi ya maji mkoani Simiyu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.